Ukweli ni katika sifa za waumini. Siku zote hakuna hasara katika kusema ukweli. Kinyume chake uongo ni katika madhambi makubwa sana.
Ukweli ni uhakika wa jambo. Muislamu wa kweli hana budi kuwa mkweli na kusimamia ukweli. Allah (s.w) anatuamrisha tuwe wakweli katika kuendesha shughuli zetu zote.
“Enyi mlioamini Mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli.” (9:119).
Msema kweli ni mpenzi wa Allah (s.w) . Naye Allah (s.w) amewaandalia wakweli ujira mzuri kabisa kwa hapa duniani na huko akhera kama tunavyobainishiwa katika Qur-an” kuwa Allah (s.w) atasema katika hiyo siku ya hisabu:-
“Hii ndiyo siku ambayo wakweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata bustani zipitazo mbele yake mito. Humo watakaa milele. Allah amewawia radhi nao wanaradhi naye. Huku ndiko kufaulu kukubwa. (5:119)
“... Na wanaume wasemao kweli na wanawake wasemao kweli... Allah amewaandalia msamaha na ujira mkubwa”. (33:35).
Msisitizo wa Muislamu kujipamba na tabia ya kuwa mkweli pia tunaupata katika Hadith ifuatayo:
‘Abdullah bin Mas ’ud (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Utaongea ukweli kwa sababu ukweli unaongoza kwenye Ucha-Mungu na Ucha-Mungu unaongoza kw enye Pepo. Mja ataendelea kusema kweli na kubakia katika ukweli mpaka aorodheshwe mbele ya Allah kuwa ni miongoni mwa wakweli wakubwa.Tahadharini na uwongo! Uwongo unaongoza kwenye uasi na uasi unaongoza kwenye Moto.Mja ataendelea kusema uwongo na kubakia katika uwongo mpaka aorodheshwe mbele ya Allah kuwa ni miongoni mwa waongo wakubwa”.
(Bukhari na Muslim).
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Katika Uislamu imani inanguzo kuu 6.Pia muumini anatakiwa ajipambe na sifa za waumini. Posti hii itakufundisha kuhusu imani katika Uislamu.
Soma Zaidi...Na tukiutafiti Uislamu kwa makini kama mfumo kamili wa maisha tunaona unadhihiri ukweli wa aya hii ya Qur-an.
Soma Zaidi...Waumini wa kweli wa Mitume wa Allah (s.
Soma Zaidi...Mafundisho ya mitume ni eneo lingine linalo thibitisha kuwepo Allah (s.
Soma Zaidi...Ni lipi lengo kuu la Elimu katika uislamu (Edk form 1 Dhanaya Elimu)
Soma Zaidi...