Somo Hili linaeleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form2: dhana ya elimu ya uislamu)
Udhaifu wa Mtazamo wa Makafiri juu ya Dini dhidi ya Mtazamo wa Uislamu.
Katika Uislamu dini maana yake ni mfumo, utaratibu, mila kamili wa maisha unaofuatwa na wanaadamu.
Rejea Quran (3:83), (3:85), (18:20), (9:33) na (16:9).
Tofauti na Makafiri, Uislamu unatazama dini kama ifuatavyo:
Maana ya Dini.
Chimbuko, Chanzo au Asili ya Dini.
Kazi ya Dini katika jamii.
Maana ya Dini.
- Dini ni mfumo, utaratibu kamili wa maisha unaofuatwa na wanaadamu. Kinyume na mtazamo wa makafiri kuwa dini ni imani juu ya kuwepo Mungu Muumba.
- Hivyo, dini ni utaratibu wowote ule wa maisha wanaofuata watu (mtu) katika kuendesha maisha yake, sio lazima kuamini kuwepo wa Mungu Muumba.
Rejea Quran (109:1-6), (9:31), (25:43), (61:8-9) na (17:81).
Chimbuko, Asili au Chanzo cha Dini.
Dai la makafiri kuwa chimbuko la dini limetokana na fikra finyu na uduni wa maendeleo ya sayansi na teknolojia wakati wa ujima, sio sahihi kwa sababu;
Hakuna kipindi chochote cha maisha, mwanaadamu aliishi katika ujima na fikra finyu, kwani tangu mwanaadamu wa mwanzo alipewa elimu na fani juu ya kuyamudu mazingira yake.
Pia mwanaadamu kila zama aliletewa mwongozo sahihi wa maisha kupitia mafundisho ya mitume unaotoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Quran (2:31) na (2:38-39).
- Hivyo katika Uislamu, chanzo na asili ya dini ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa ushahidi wa aya na hadith mbali mbali.
Kazi ya Dini katika jamii.
Mtazamo wa Makafiri, dini ni chombo cha unyonyaji, dhuluma na kujenga matabaka katika jamii, dai hili ni la kweli au sio la kweli kama ifuatavyo;
Ukweli wa dai hili ni sahihi kwa dini zote za wanaadamu kama Ushirikina, Utawa na Ukafiri.
Udhaifu wa dai hili, ni kuwa dini sahihi ilikuwa na kazi ya kuikomboa jamii kutokana na aina zote za ukandamizaji, utabaka, dhuluma, n.k.
- Hivyo katika Uislamu, dini ina kazi ya kuiongoza jamii katika maisha ya haki, uadilifu na usawa na kupigana na aina zote za dhuluma na ukandamizaji.
Rejea Quran (57:25), (28:4) na (7:103-105).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Soma Zaidi...Allah hutumia maandishi kuwafundisha wanadamu. Mfano mzuri ni nabii Musa ambaye alipewa vibao vya maandishi.
Soma Zaidi...Kwa mtazamo wa kikafiri elimu imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Elimu ya dunia na Elimu ya akhera.
Soma Zaidi...Yale tunayoamrishwa kushikamana nayo ni haya yafuatayo: (i)Kumuabudu Allah (s.
Soma Zaidi...Hii ni njia ambayo mwanaadamu huongeleshwa moja kwa moja na Allah (s.
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hichi titajifunza maana ya uislamu,na maana nyingine tofauti.
Soma Zaidi...