Uovu wa kumzulia Muumini Uzinifu na Maovu mengine na Hukumu dhidi ya Wazuaji

Kumzulia mtu mtwahirifu kuwa amefanya tendo la zinaa pasina kuleta ushahidi stahiki ni tendo ovu mno mbele ya Allah (s.

Uovu wa kumzulia Muumini Uzinifu na Maovu mengine na Hukumu dhidi ya Wazuaji

(d) Uovu wa kumzulia Muumini Uzinifu na Maovu mengine na Hukumu dhidi ya Wazuaji



Kumzulia mtu mtwahirifu kuwa amefanya tendo la zinaa pasina kuleta ushahidi stahiki ni tendo ovu mno mbele ya Allah (s.w). Kina cha Uovu wa tendo hili la kuwasingizia uzinifu watu watwahirifu kinadhihirishwa na adhabu kali inayotolewa dhidi ya wazushi hawa:


'Na wale wanaowasingizia wanawake watahirifu (kuwa wamezini), kisha hawaleti mashahidi wanne, basi wapigeni mijeledi, (bakora) thamanini, na msiwakubalie ushahidi wao tena, na hao ndio mafasiki." (24:4)



"Bila shaka wale wanaowasingizia wanawake waliotakasika wasiojua (maovu), Waislamu; (wenye kuwasingizia watu hawa) wamelaaniwa katika dunia na akhera; nao watapata adhabu kubwa."



'Siku ambayo zitawashuhudia ndimi zao na mikono yao na miguu yao, kwa yale waliyokuwa wakiyafanya."
'Siku hiyo Mwenyezi Mungu Atawapa sawasawa malipo yao ya haki, na watajua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye (Mwenye kulipa kwa) haki iliyo dhahiri."
(24:23-2 5)



Pia aya ifuatayo inakemea kwa ujumla juu ya tabia mbaya ya kuwasingizia (kuwazulia) watu wema kuwa wamefanya uovu, ili tu kuwadhalilisha na kuwaaibisha mbele ya jamii:


'Kwa yakini wale wannnaopenda uenee uovu kwa wale walioamini, watapata adhabu iumizayo katika dunia na akhera; na Mwenyezi Mungu ndiye Anayejua; na nyinyi hamjui." (24:19)



Jambo la kuwasingizia uovu watu wema ni ovu mno mbele ya Allah (s.w) kwa sababu ndiyo silaha wanayotumia wanafiki na washirika wao katika kudhoofisha Uislamu kwa kuwakatisha tamaa wanaharakati na kuisambaratisha jamii ya Waislamu kwa ujumla. Katika historia ya Uislamu, wakati wa Mtume (s.a.w) silaha hii waliitumia wanafiki wakiongozwa na mkubwa wao Abdulllah bin Ubayy, walipomsingizia Bi Aisha (r.a), mkewe Mtume (s.a.w), kuwa amezini na Swafan bin Mu'attal Sulami, miongoni mwa maswahaba wema aliyeshiriki katika vita vya Badr. Allah (s.w) aliwatakasa waja wake hawa na uzushi wa wanafiki kwa kushusha Sura hii hasa katika aya zifuatazo:


Hakika wale walioleta uwongo huo (wa kumsingizia Bibi Aisha - mkewe Mtume -kuwa amezini) ni kundi miongoni mwenu, (ni jamaa zenu). Msifikiri ni shari kwenu, bali hiyo ni heri kwenu. Kila mtu katika wao atapata aliyoyachuma katika madhambi hayo. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao, atapata adhabu kubwa (zaidi)
Mbona mliposikia (habari) hii, wanaume Waislamu na wanawake Waislamu hawakuwadhania wenzao mema, na kusema "huu ni uzushi dhahiri?"



Mbona hawakuleta mashahidi wanne? Na walipokosa kuleta mashahidi, basi hao mbele ya Mwenyezi Mungu ni waongo.
Na kama isingalikuwa juu yenu fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema Yake katika dunia na akhera, bila shaka ingalikupateni adhabu kubwa kwa sababu ya yale mliyoyashughulikia.



Mlipoupokea (uwongo huo mkawa mnautangaza) kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyoyajua, na mlifikiri ni jambo dogo, kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa. Na mbona, mliposikia, hamkusema: "Haitujazii kuzungumza haya: Utakatifu ni Wako (Mola wetu!) Huu ni uwongo mkubwa." Mwenyezi Mungu Anakunasihini msirudie kabisa kufanya mfano wa haya, ikiwa nyinyi ni Waislamu kweli. Na Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya (zake); na Mwenyezi Mungu ndiye Ajuaye, Mwenye hikima.' (24:11-1 8)



Kutokana na aya hizi tunajifunza yafuatayo:


(i) Waumini watakaposikia habari za uzushi dhidi ya watu wema,wasizikubali bali wadai ushahidi ulio wazi unaothibitisha tuhuma hizo.
(ii)Wazushi wakishindwa kuleta ushahidi, wachukuliwe moja kwa moja kuwa ni waongo na Waislamu wote wawe dhidi yao na kuwepo adhabu inayostahiki.
(iii)Ni marufuku kwa waumini kudaka na kutangaza mambo ya uzushi dhidi ya watu wema ambayo hawana hakika nayo. Katika kusisitiza hili Allah anatuasa:
'Enyi mlioamini! Kama fasiki, (asiyekuwa wa kutegemewa) akikujieni na habari (yoyote ile msimkubalie tu) bali pelelezeni (kwanza), msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyoyatenda. '(49:6)
(iv)Waislamu wanahimizwa wajenge tabia ya kuwa na dhana njema juu ya waumini wenzao kuwa haiwezekani kwa muumini kufanya tendo hilo chafu.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 83

Post zifazofanana:-

Uanzishwaji wa Makundi mbalimbali ya Harakati za Kuhuisha Uislamu Ulimwenguni
8. Soma Zaidi...

Je mahari inashusha hadhi ya mwanamke?
Je, Mahari inashusha hadhi ya mwanamke? Soma Zaidi...

SIKU HATARI ZA KUPATA UJAUZITO KWA MWENYE MZUNGURUKO WA SIKU KIDONGO AU NYUNGI
SIKU YA KUPATA UJAUZITO Kawaida wanawake walio wengi mzunguruko wa siku zao ni siku 28 lakini wapo ambao ni zaidi ya hapo na wapo ambao ni chini ya hapo. Soma Zaidi...

DUA 11 - 20
11. Soma Zaidi...

NJIA AMBAZO MARADHI HUAMBUKIZWA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Welcome to Online School
Soma Zaidi...

maana ya Eda na aina zake
Ni kipindi au muda wa kungojea mwanamke aliyepewa talaka (aliyeachwa) au kufiwa na mumewe kabla ya kuolewa na mume mwingine. Soma Zaidi...

Nini Chanzo
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

AINA KUU ZA VYAKULA: vyakula vya protini, wanga, fat na mafuta, vitamini, madini na maji
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

DALILI ZA KUTOKA AU KUHARIBIKA KWA MIMBA
Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka. Soma Zaidi...

Ni ipi siku ya kupata ujauzito, na nitajuwaje kama nimepata ujauzito?
Hapa utajifunza siku nzuri kushoriki tendo la ndoa kupata ujauzito, dalili za siku hiyo na kuitafuta kwa mahesabu Soma Zaidi...

HUKUMU ZA MIIM YENYE SAKINA
SURA YA NNE HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA HUKUMU ZA MIYM SAKINA: Mym sakina ni miym ambayo haina i'rab ( '). Soma Zaidi...