Amri ya Kumfuata Mtume (s.
Amri ya Kumfuata Mtume (s.a.w)
Sema, "Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni, (hapo) Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye maghufira (na) mwenye rehema." (3:31) "Na anachokupeni Mtume basi pokeeni na anachokukatazeni jiepusheni nacho". (57:7)
Amri ya Kumfanya Mtume (s.a.w) Kiigizo "Bila shaka mnao mfano mwema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na kumtaja Mwenyezi Mungu sana." (33:21) Kutomfuata Mtume (s.a.w) ni Uasi Na anayemwasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kuiruka mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamwingiza Motoni, humo atakaa milele, na atapata adhabu zifedheheshazo. (4:14)
Siku hiyo wale waliokufuru na kumwasi Mtume watatamani ardhi isawazishwe juu yao (yaani lau kuwa wamefukiwa tu kaburini bila ya kufufuliwa). Wala hawataweza kumficha Allah Hadith yo yote (katika ammbo waliyoyafanya). (4:42) “Je, hawajui ya kwamba anayeshindana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwa yeye atapata moto wa Jahannam kukaa humo daima? Hiyo ndiyo hizaya kubwa." (9:63)Â
“… Na watakao muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi bila shaka watapata moto wa Jahanam, wakae humo milele." (72:23)
Aya hizi zote kwa ujumla zinatuonyesha wazi kuwa kufuata sunnah, ya Mtume (s.w) si jambo la hiari kwa Muislamu. Hivyo ule uoni walionao baadhi ya Waislamu kuwa sunnah ni jambo la hiari, ukilifanya unapata thawabu na ukiliacha hupati dhambi ni uoni potofu kama tutaizingatia pia aya ifuatayo:
"Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika wamepotea upotofu ulio wazi (kabisa). (33:36)
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 197
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya
👉2 Simulizi za Hadithi Audio
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 kitabu cha Simulizi
NASAHA ZANGU NNE KWAKO KUHUSU QURAN, MAUTI, DUA NA MENGINE
Soma Zaidi...
nmna ya kufanya istikhara na kuswali swala ya Istikhara
Soma Zaidi...
Ni nini maana ya ndoa?
Soma Zaidi...
Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo
Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo. Soma Zaidi...
Utoaji wa zaka katika Dhahabu, fedha ama silva na pesa
Soma Zaidi...
kusai yaani kukimbia kati ya mlima swafa na marwa mara saba
4. Soma Zaidi...
KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...
Kafara ya mwenye kuvunja masharti ya ihram
Soma Zaidi...
Kitabu Cha Dua 120
Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe vyote. Soma Zaidi...
SIRA (HISTORIA YA ) MTUME MUHHAMAAD (S.A.W) KUZALIWA KWAKE, VITA ALIVYOPIGANA, SUNNAH ZAKE NA MAFUNDISHO YAKE
Soma Zaidi...
swala ya witri na namna ya kuiswali
3. Soma Zaidi...
Swala ya kupatwa kwa jua na mwezi na namna ya kuiswali
11. Soma Zaidi...