Mwanamume mzinifu hafungamani ila na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina; na mwanamke mzinifu hafungamani naye ila mwanamume mzinifu au mshirikina; na hayo yameharamishwa kwa waumini" (24:3)
Wanawake habithi (wabaya) ni wa wanaume habithi na wanaume habithi ni wa wanawake habithi; na wanawake wema ni wa wanaume wema na waume wema ni wa wanawake wema ….. " (24:26)
Aya hizi zinatuweka wazi kuwa ili kujenga jamii iliyoinukia kimaadili, waumini hawanabudi kuwa macho katika uchumba. Waumini wahakikishe kuwa katika ndoa ya kwanza binti muolewaji ni bikra na kijana muoaji ni bikra vile vile. Kadhalika katika ndoa ya pili, waumini wasiidhinishe ndoa mpaka wawe na uhakika pasina tone la shaka, kuwa waoanaji wawili ni watwaharifu na wacha-Mungu. Mwanamume mzinifu ni mshirikina kwa mujibu wa Qur'an kwa kuwa ameyafanya matamanio ya nafsi yake kuwa Mungu badala ya Allah (s.w)
"Je, umemuona yule aliyefanya matamanio (ya nafsi) yake (kila anachokipenda), kuwa Mungu wake? Basi je, utaweza kuwa mlinzi wake (ukamhifadhi na hayo, na hali ya kuwa hataki)? (25:43)
Kukiukwa kwa maagizo ya Allah (s.w), katika aya hizi (24:3, 26), imekuwa ni sababu kubwa ya mtafaruku katika familia nyingi za Waislamu na jamii kwa ujumla. Familia za waumini zitaishi kwa furaha na amani endapo ujumbe wa aya hizi utafuatwa vilivyo tangu mapema katika kuanzisha familia hizi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Kwenye mada hii tutajifunza shahada mbili,tafsiri ya shahada kstika maisha ya kila siku.
Soma Zaidi...Ni mgawanyo upi wa elimu haukubaliki. Ni ipi elimul akhera na elimu dunia? (Edk form 1 Dhana ya elimu)
Soma Zaidi...Na tukiutafiti Uislamu kwa makini kama mfumo kamili wa maisha tunaona unadhihiri ukweli wa aya hii ya Qur-an.
Soma Zaidi...Katika Uislamu elimu imegawanyika katika Elimu ya muongozo na elimu ya mazingira.
Soma Zaidi...Elimu inaweza kugawanyika katika makundibmrngine mawili ambayo ni elimu yenye manufaa na elimubisiyi na manufaa
Soma Zaidi...Kwa mtazamo wa kikafiri elimu imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Elimu ya dunia na Elimu ya akhera.
Soma Zaidi...Mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mambo ya faradhi kuhusu maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...