Elimu imepewa kipaumbele kikubwa kwenye uislamu. Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu nafasi ya Elimu katika uislamu.
Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo:
Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.Tunajifunza katika Qur-an kuwa jambo la kwanza alilotunukiwa Adam (a.s) mara tu baada ya kuumbwa kwake ni kupewa elimu.
“Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha Adam majina ya vitu vyote...” (2:3 1)
“Majina ya vitu vyote” katika aya hii inaashiria fani zote za elimu ambazo anahitajia mwanaadamu hapa duniani ili afikie kwa ufanisi lengo la kuumbwa kwake. Pia tunajifunza katika Quran kuwa mwenye elimu na hekima amepewa kheri nyingi.
(Mungu ) humpa hikma amtakaye, na aliyepewa hikma bila shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili. (2.269).
Kutafuta elimu (kusoma) ni amri ya kwanza kwa mwanaadamu. Tunajifunza kutokana na historia ya kushushwa Qur-an kuwa Wahay wa kwanza kumshukia Mtume (s.a.w) ambao ndio ulimtawazisha rasmi kuwa mtume ni ule unaopatikana katika aya tano za mwanzo za Suratul-’Alaq:
“Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba.Ambaye amemuumba mwanaadamu kwa ‘Alaq (kitu chenye kuning’inia). Soma na Mola wako ni karimu sana. Ambaye amemfundisha mwanaadamu kwa kalamu. Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya) mambo aliyokuwa hayajui”.(96:1-5)
Kutokana na aya hizi, kwa muhtasari, tunajifunza yafu atayo:
1. Kusoma kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni jambo la kwanza waliloamrishwa wanaadamu na Mola wao.
2. Kusoma kwa jina la Mola wako ni kusoma kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu au ili kuweza kumwabudu Allah(s.w) inavyostahiki na kusimamisha Uislamu katika jamii.
3. Radhi za Mwenyezi Mungu zitapatikana pale mwanaadamu atakapoweza kufikia lengo la maisha yake la kumuabudu Allah (s.w) kwa kuzingatia maamrisho na mipaka ya Mwenyezi Mungu katika kila kipengele cha maisha.
4. Amri hii ya kusoma hailengi fani maalum tu ya elimu; bali kila fani itakayomuwezesha mwanaadamu kufikia lengo la maisha yake kwaufanisi.
5. Chanzo au chimbuko la fani zote za elimu ni Allah (s.w). Hivyo kwa Muislam mlango wa kwanza wa elimu ni kusoma kwa mazingatio Qur-an na hadithi sahihi za Mtume (s.a.w) na kusoma maarifa ya Uislamu kwa ujumla kutokana na vyanzo hivi viwili.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Mtazamo wa uislamu juu ya ibada (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya Mitume wa Allah (s.
Soma Zaidi...Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...βNa wasiape wale wakarimu na wenye wasaa miongoni mwenu, kujizuia kuwasaidia jamaa zao, maskini na wale waliohama kwa ajili ya Dini ya Allah; na wasamehe na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita).
Soma Zaidi...Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Soma Zaidi...