jamii muongozo

Haja ya Mwongozo kutoka kwa Allah (s.

Haja ya Mwongozo kutoka kwa Allah (s.w)

Haja ya Mwongozo kutoka kwa Allah (s.w)


Mwanaadamu pamoja na elimu aliyotunukiwa, hana uwezo pasina msaada wa muumba wake, kupata majibu sahihi ya maswali ya msingi ya maisha yake hapa duniani na huko akhera. Maswali haya ya msingi ni:



1 Nani chanzo cha maumbile yote?



2 Ni lipi lengo la mwanaadamu hapa ulimwenguni?



3 Atalifikiaje lengo hilo?



4 Ni ipi nafasi halisi ya mwanaadamu hapa ulimwenguni?



5 Ni ipi hatma yake baada ya kufa, je kufa ndio mwisho wa maisha yake?
Mwanaadamu bila ya mwongozo kutoka kwa muumba wake hana uwezo wa kutoa majibu sahihi ya maswali haya. Elimu ya mazingira aliyonayo mwanaadamu ni finyu mno kiasi kwamba haimuwezeshi hata kuijua roho yake kama tunavyokumbushwa katika Qur-an:
โ€œNa w anakuuliza habari ya roho. Sema: โ€œRoho ni jambo lililohusika na Mola wangu. Nanyi hamkupewa katika elim u ila kidogo ka b isa.โ€ (17:85)
Maana ya Kuamini Vitabu vya Allah
Imani ya kweli katika Uislamu haishii moyoni tu bali ni lazima idhihirishwe katika matendo ya kila siku. Hivyo, waumini 162wa kweli wa vitabu vya Allah (s.w) ni wale wanaoendesha maisha yao ya kila siku katika kila kipengele kwa kufuata bara bara maongozi ya vitabu vya Allah (s.w). Kabla ya Qur-an kushushwa, waumini wa kweli wa vitabu vya Allah vilivyotangulia, vikiwemo Taurat, Injili, Zaburi, n.k. ni wale walioishi kwa mujibu wa maongozi ya vitabu hivyo kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


โ€œHakika tuliteremsha Taurati yenye uw ongozi na nuru; ambayo kwayo Manabii waliojisalimisha (kwa Allah) waliwahukumu Mayahudi; Watawa na Maulamaa pia (walihukumu kwa hiyo Taurat); kwa sababu walitakiwa kuhifadhi kitabu hicho cha Allah; Nao walikuwa mashahidi juu yake. Basi, msiwaogope w atu, bali niogopeni (Mimi). Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache (ya maslahi ya dunia).Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Allah, basi Hao ndio m akafiri.โ€ (5:44)


โ€œWatu wa Injili wahukumu kwa yale aliyoteremsha Allah ndani yake. Na wasiohukumu kwa (kufuata) yale aliyoteremsha Allah, basi hao ndio mafasiki (maasi)โ€ (5:47)


Baada ya Qur-an kushushwa kupitia kwa Mtume Muhammad (s.a.w) kwa ajili ya walimwengu wote, Waumini wa kweli wa vitabu vya Allah (s.w) ni wale wanaoishi kwa kufuata maongozi ya Qur-an na Sunnah ya Mtume Muhammad (s.a.w) katika maisha yao yote. Si muumini yule anayeikataa Qur-an na Mtume aliyeshushiwa hatakama anadai kuwa anaiamini Taurat, Zabur, Injili, n.k. na Mitume walioshushiwa vitabu hivyo kwa mujibu wa aya ifuatayo:


โ€œEnyi mlioamini! Mwaminini Allah na Mtume wake na kitabu alichokiteremsha juu ya Mtume wake,na vitabu alivyoviteremsha zamani. Na mwenye kumkanusha Allah na Malaika wake na vitabu vyake, na Mitume wake na siku ya mwisho, basi bila shaka amepotea upotofu uliombali (na haki)โ€ (4:136)
Hivi sasa, katika vitabu vya Allah (s.w) vilivyoshushwa hapa ulimwenguni, ni Qur-an pekee iliyobakia katika lugha yake ya asili (Kiarabu fasaha) na katika usahihi wake wa asili. Vitabu vilivyoitangulia Qur-an vinakabiliwa na matatizo makubwa mawili yafu atayo:
1. Lugha zilizotumika katika vitabu hivyo zimekufa (zimetoweka). Kwa mujibu wa Qur-an kila Mtume aliletewa wahay kwa lugha ya watu wake



โ€œNa hatukumpeleka Mtume yeyote isipokuwa kwa lu gha ya watu wake ili ap ate kuwaba in is hia...โ€ (14:4).
Tunajua kutokana na historia kuwa lugha hukua na kufa. Hivi sasa kwa mfano Allah (s.w) akituletea kitabu alichoshushiwa Nabii Adam (a.s) katika lugha aliyozungumza Adam (a.s) na wanawe wa karibu wa wakati ule, hatuwezi kupata ujumbe wake.2. Vitabu vilivyoitangulia Qur-an viliingizwa mikono ya watu, vikabadilishwa na kupotoshwa ili kukidhi matashi ya watu waliodai kufuata vitabu hivyo kinyume na Allah (s.w). Taurat, Zabur, Injili, n.k. Vilikumbwa na tatizo hili.
Qur-an imeepukana na matatizo haya kwani hivi leo, Lugha ya Kiarabu, ni miongoni mwa lugha kubwa zinazokua kwa kasi; pia Kiarabu ni lugha fasaha na tajiri kwa maneno kuliko lugha zote duniani. Pia Qur-an tofauti na vitabu vingine vya Allah (s.w), haitaingiliwa na mkono wa mtu, kwani imepewa hifadhi na Allah (s.w) mwenyewe:Hakika sisi ndio tulioteremsha mawaidha haya (hii Qur-an) na hakika Sisi ndio tutakao yalindaโ€ (15:9).


โ€œHaitakifikia batili mbele yake wala nyuma yake; kimeteremshwa na Mwenye Hikma โ€ (41:42).Hivyo hivi sasa, Muumini wa kweli wa vitabu vya Allah (s.w) ni yule:



1. Anayeamini pasi na tone la shaka kuwa Qur-an yote kama msahafu ulivyo kuanzia sura ya kwanza (Al-Faatiha) mpaka sura ya mwisho (An-Naas) ni maneno kutoka kwa Allah (s.w). Muumini anayakinisha kuwa:โ€œHiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake, ni uwongozi kwa wamchao Allahโ€ (2:2).



2. Anayaongoza maisha yake ya kila siku kwa kufuata Qurโ€™an na mwenendo au sunnah ya mfasiri wa Qur-an, Mtume Muhammad (s.a.w). Qur-an yenyewe inasisitiza:


โ€œHaiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenyekumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi (kabisa).โ€ (33:36)โ€œ... Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mw enyezi Mungu, basi hao ndio m akafiriโ€. (5:44)โ€œ... Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimuโ€ (5:45)โ€œ... Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio mafasiki (maasi) โ€œ (5:47)




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 359

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰2 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰4 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰5 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu

Faradhi kwa maiti ya muislamu (edk form 2:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Nguzo za Imani kwa mujibu wa mafunzo ya kiislami.

Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu nguzo sita za imani katika Uislamu.

Soma Zaidi...
(c)Vipawa vya Mwanaadamu

Vipawa vya mwanaadamu ni sababu nyingine inayomfanya mwanaadamu asiweze kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine.

Soma Zaidi...
Kina Cha uovu wa shirk

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mambo muhimu anayofanyiwa muislamu kabla ya kufa

Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
zijue Nguzo za uislamu, imani, ihsani pamoja na dalili za qiyama

ุนูŽู†ู’ ุนูู…ูŽุฑูŽ ุฑูŽุถููŠูŽ ุงู„ู„ู‡ู ุนูŽู†ู’ู‡ู ุฃูŽูŠู’ุถู‹ุง ู‚ูŽุงู„ูŽ: " ุจูŽูŠู’ู†ูŽู…ูŽุง ู†ูŽุญู’ู†ู ุฌูู„ููˆุณูŒ ุนูู†ู’ุฏูŽ ุฑูŽุณููˆู„ู ุงู„ู„ูŽู‘ู‡ู ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆ ุณู„ู… ุฐูŽุงุชูŽ ูŠูŽูˆู’ู…ูุŒ ุฅุฐู’ ?...

Soma Zaidi...
Sifa za waumini zilizotajwa katika surat As-Sajida

Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya?

Soma Zaidi...
mitume

Labda itaulizwa: Kwanini Mtume Muhammad (s.

Soma Zaidi...