image

magonjwa na lishe

DARASA LA AFYA MAGOJWA YANAYOHUSIANA NA VYAKULA 1.

magonjwa na lishe

DARASA LA AFYA

MAGOJWA YANAYOHUSIANA NA VYAKULA
1.UGONJWA WA KISUKARI
kisukari ni ugonjwa unaotokea pale ambapo mwili unashindwa kuzalisha kabisha homon ya insulin au kushindwa kuzalisha homon hii kwa kiwango kinazotosha. Wakati mwingine kisukari kinatokea pale mwili unaposhindwa kutumia insulin inayozalishwa mwilini. Hii ni homon ambayo inakazi ya kuthibiti kiwango cha sukari ndani ya mwili kisiwe kikubwa au kuwa kidogo. Homoni hii huzalishwa na kongosho (pancreas.

Homoni ya insulin huakikisha kuwa kiwango cha sukari ndani ya mwili kikiwa kikubwa hubadilishwa kuwa glucagon na huhifadhiwa kwenye ini. Na kiwango cha sukari kikiwa kidogo glucagon hubadilishwa na homon hii kuwa glucose (sukari) ambayo husambazwa sehemu zinazohotaji kuzalisha energy

Kuna aina kuu mbili za kisukari ambazo ni TYPE 1 DIABETS na TYPE 2 DIABETS. Hii aina ya kwanza ambayo ni type 1 diabets hutokea pale ambapo mwili unashindwakabisa kuzalisha homon ya insulin. Hii hotokea pale ambapo mfumo wa afya unaposhambulia na kuuwa homoni ya insulin. Maranyingi aina hii ya kisukari huwapata watoto na walio na umri kati ya miaka 10-20. Watu wazima huenda kuwa na kisukari aina hii ila ni kwa uchache. Aina hii ya kisukari husababishwa na gene (genetic mutationr), au katika mazingira kama mashambulizi ya virusi.

Aina ya pili ya kisukari type 2 diabets hutokea pale ambapo mwili unazalisha insulin ambayo si yenye kutosheleza. Au hutokea pale seli za mwili zinapowacha kutumia hmon ya insulin (insulin resistance). Aina hii ya kisukari huwapata watu wakubwa ila kwa uchache hueza pia ukawapata watoto. Aina hii ya kisukari huweza kusababishwa na kuwa na uzito usio wa kawaida (over weight), umri (kuanzia miaka 45), kurithi kutoka katika familia/ukoo rangi (race/ethinick background), kutokufanya mazoezi, vyakula,.

Dalili za kisukari hutofautiana japo wataalamu wa afya wanataja hizi;-kuhisi njaa kali, kuhisi kiu kikali sana, ngozi kukauka, kupunguwa kwa uzito bila ya sababu, kukojoakojoa, kutokuona vizuri, kuchelewa kupona majeraha, kuchoka sana(kuhisi uchovu usio wa kawaida).na kupata ganzi. Japo kuwa ugonjwa wa kisukari ni hatari kwa afya lakini mtu anaweza kuishi vizuri kama atafata utaratibu na kanuni nzuri za kuishi na ugoonjwa huu. Kwa mfano nchini marekani zaidi ya watu milioni 23 wanasumbuliwa na kisukari lakini wanaishi maisha mazuri tuu. Hivyo kama mgonjwa atafata kanuni na masharti pamoja na kubadilisha fife style yaani namna anavyoishi anaweza kupunguza athari za uginjwa huu. Hapo chini utaona ushauri juu ya mwenye kisukari aishi

Chakula; mgonjwa wa isukari anatakiwa ale chakula kisicho na mafuta mengi, ckisicho na chumvi wala sukari nyingi. Kuala matunda na mboga za majani. Hakikisha unakula katika muda maalumu siku zote pia angalau upate chakula mara tatu kwa siku kula chakula kisicho kobolewa. Pia hakikisha unakunywa maji mengi zaidi kwa siku

Mazoezi; hakikisha unafanya mazoezi si chini ya mara tatu kwa wiki. Hii huenda ikasaidia kupunguza usito na kuthibiti kiasi cha sukari ndani ya mwili wako. Pia kufanya mazoezi ni muhimu kwa afya yako kwa ujumla. Mazoezi yanaweza kupunguza mlundikano wa mafuta kwenye ngozi na mishipa yta damu. Hali hii itakusaidia kupunguza uwezekano wa kuapata strock na shambulio la moyo.

Dhibiti uzito wako; hakikisha kuwa hauna uzito usio wa kawaida. Yaani hakikisha kuwa unapunguza uzito kama uzito wako ni mkubwa. Pata ushauri wa daktari kuhusu uzito wako kama unakufaa au umezidi kulingana na afya yako. Zipo njia nyingi za kupunguza uzito kupitia vyakula, mazoezi na nyinginezo. Muone daktari au pata ushauri kwa walio na ujuzi wa njia salama ya kupunguza uzito.

Tumia dawa; kama kisukari kimeshindikana kuthibitiwa kwa nyia hizo hapo juu anza kutumia dawa. Zipo dawa maalumu kwa wagonjwa wa kisukari. Pia inashauriwa kuwa mtu aanze kutumia dawa za kumeza kabla ya zile za sindano. Muone daktari atakupatia dawa hizo kulingana na afya yako. Watu wengi wanakuwa wavivu wa kunywa dawa lakini kwa baadhi ya magonjwa uvivu huu ni hatari zaidi kwa afya zao.

Ugonjwa wa kisukari usipopata matibabu mapema au usipo fata ushauri jinsi ya kuishi na ugonjwa huu matatizo mengi yanaweza kutokea ikiwemo presha, shambulio la moyo na kupapalaiz (strock), matatizo ya macho na upofu pia na matatizo ya meno na finzi. kwa ujumla afya ya mtu inaweza kuwa katika hali mbaya zaidi na pia huenda ikamsababishia kifo. Hutokea wakati mengine mgonjwa mwenye kisukari sukari inashuka chini kabisa, hapa mgonjwa anaweza kuonesha dalili mbalimbali zikiwemo;- kutoka na jasho jisngi,kupiga myayo mara kwa mara, kushindwa kuzungumza na kushinda kufikiri vizuri, kukosa fahamu, kukosa nguvu hata kidogo, kupata uchovu usio wa kawaida pia mtu anaweza kujihisi kama ndo anataka kufa vile.

Hali ikiwa hivi kuna huduma ya kwanza ambayo anatakiwa afanyiwe kama kupewa juisi ya matunda nusu kijombe. Glucose vijiko 3, maziwa kikombe kimoja, Katika magonjwa yanayosumbuwa leo kisukari ni moja wapo japo halichangii kuuwa watu wengi kama magonjwa mengine. Ni vizuri kujuwa kama unakisukari au huna ili uweze kuchukuwa hatuwa mapema. Pia kwa wale wanaovuta sigara kisukari ni hatari na tabia hii, ni vizuri kuacha uvutaji wa sigara na kuacha kabisa pombe kwa ni yote haya ni hatari zaidi kwa mwenye kisukari


                   







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 755


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Faida za mchaichai/ lemongrass
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za mchaichai Soma Zaidi...

FAIDA ZA MAJI MWILINI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Faida za kula asali
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula asali Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kisamvu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kisamvu Soma Zaidi...

Faida za kula Tangawizi
tangawizi ni katika viungio vya mboga vyenye faida, pia ni kinywaji, zijuwe leo faida za tangawizi Soma Zaidi...

Vyakula muhimu kwa afya ya uzazi wa mwanaume
Vyakula vya kuongeza Nguvu za kiume Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamini A na kazi zake
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kungumanga
Soma Zaidi...

Faida za majani ya mstafeli
Posti hii inahusu zaidi faida za majani ya mstafeli,ni majani ambayo utibu magonjwa mbalimbali hasa saratani, kwa hiyo tunapaswa kuyatumia ili tuweze kupata matibabu ya kansa mbalimbali. Soma Zaidi...

ijuwe namna ya kufanya ihram na Vazi la ihram
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula tangawizi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za tangawizi Soma Zaidi...

Faida za kiafya za topetope (accustard apple/sweetsop)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula topetope Soma Zaidi...