kuhusu vitamini K, wapi tutavipata, ni zipi athari zake na ni zipi kazi zake mwilini.
Vitamini K ni moja kati ya vitamini ambavyo miili yetu inavihitaji kwa ajili ya shughuli mbalimbali. Endapo upungufu wa vitamini hivi utatokea basi madhara makubwa ya kiafya yatamkumba mtu. Katika makala hii nimekuandalia somo hili ambalo litakwenda kuangalia zaidi kuhusu vitamini K, wapi tutavipata, ni zipi athari zake na ni zipi kazi zake.
YALIYOMO:
NINI MAANA YA VITAMINI?
Vitamini ni kampaudi ogania ambazo zinahitajika na mwili kwa ajili ya ukuaji wa mwili na utendaji wa michakato ya kibaiolojia ndani ya miili (metabolism), na ni viruubisho ambavyo havitengenezwi ndani ya miili yetu. Vitamini vipo katika makundi makuu mawili ambayo ni fat soluble na water soluble. Pia makundi ya vitamini ni A, B, C, D na K.
Fat soluble ni titamini ambavyo mwili unaweza kuvihifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadaye vitamini hivi ni kama A, D, E na K. Hii ina maana hatuhitaji tule vyakula vyenye vitamin hivi kila siku. Watwer soluble ni vitamini ambavyo mwili hauwezi kuvihifadhi mwilini hivyo baada ya kula chakula mwili hufyonza kiasi cha vitamini hivi na kuvitumia. Hivyo tunahitajika tule vyakula vyenye vitamini hivi kila siku. Vitamini hivi ni kama D na C.
VITAMIN K NI NINI?
Hivi ni vitamini katika kundi la fat soluble ambavyo vimetokana na kampaundi za naphthoquinone. Vitamin hivi vimeitwa K, hii K asili yake ni neno la lugha ya Danish kutoka neno koagulation neno hili ukilileta kwenye lugha ya kiingereza unapata coagulation yaani kuganda. Hasa hapa kunazungumziwa kuganda kwa damu. Kwani vitamin K huhitajika mwilini katika kusaidia mchakato wa kuganda kwa damu pindi mtu anapopata jeraha.
Kwa mara ya kwanza vitamin K vimeanza kuletwa kwenye maandishi na mwanasayansi wa Danish mwaka 1929 Bwana Henrik Dam pindi alipokuwa akifanya tafiti juu ya kazi za Cholesterol kwenye mwili. Wataalamu wa lishe wameigawa vitamin K katika makundi ya K1 na K2. hivi vya K1 kitaalamu huitwa phytonadione huweza kupatikana kwenye mboga za majani na hivi vya K2 kitaalamu huitwa menaquinone hupatikana kwenye nyama, mayai na maziwa.
VYAKULA VYA VITAMIN K
Kama ulivyosoma hapo juu kuwa vitani K vipo katika makundi kma Vitamin K1 na vitamin K2 na pia umeona kwa ufupi vyanzo vya kila vitamini K. Sasa hapa nitakuorodheshea tena vyanzo vya vitamin K
Vitamin K1:
Vitamini hivi unaweza kuvipata kwenye mboga za majani za rangi ya kijani kama
Vitamin K2
Hivi unaweza kuvipata kwenye;-
KAZI ZA VITAMIN K MWILINI
Kama tulivyokwisha kuona maana ya K kweye vitamini K, sasa hebu tuone baadhi tu ya kazi za Vitamin hivi.
Hii ndiyo kazi kuu ya vitamin K, ni kuwa pindi unapopata jeraha lolote ambalo litapelekea damu kutoka, basi ili kuhakikisha damu haitoki zaidi katika jeraha lile,na hatimaye damu hukata, kazi hii yote hufanya na vitamin K hasahasa hapa tunazungumzia K1. vitamini K hutumika katika kutengeneza prothrombin, factors VII, IX, pamoja na X, kwa pamoja huitwa cloting factor na ndizo ambazo huhusika katika kusimamisha damu isiendelee kutoka kwenye jeraha. Upungufu wa vitamin K unaweza kusababisha damu kutokuganda ama utoka hata kama hakuna jeraha.
Kuna ugonjwa unatambulika kama osteoporosis haya ni maradhi ya mifupa kuwa midhaifu, kuuma na kuweza kupasuka kwa urahisi sana. Mara nyingi maradhi haya yanawapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 50, lakini pia unaweza kuwapata watu wenye chini ya hapo.
Wataalamu wa afya wanahusianisha upungufu wa vitamin K na kupata maradhi haya. Tafiti zinaonyesha kuwa vitamin K husaidia katika kuboresha afya ya mifupa, kuthibiti ujazo na tungamo la mifupa pia kuzuia mipasuko kwenye mifupa. Hatahivyo tafiti zaidi zinahitajika kuthibitisha zaidi.
Tafiti zinahusisha uwezo wa kukumbuka na vitamin k. baadhi ya tafiti zilizofanywa zinaonyesha kuwa watu wenye umri wa zaidi ya 70 huwa uwezo wao wa kukumbuka unapungua, ila kwa wale ambao wana vitami K vya kutosha kwenye damu zao uwezo wao wa kukumbuka unakuwa mkubwa. Na hapa pia tunazungumzia sana vitamin K1.
Vitamin K husaidia katika kushusha presha ya damu kwa kuzuia kuganda kwa madini ndani ya mishipa ya damu. Hali hii huweza kusaidia moyo uweze kusukuma damu bila ya matatizo yeyote. Tafiti zinaonyesha kuwa kuwa na vitami K vya kutosha huzuia ama kupunguza athari za kupata stroke yaani kupalalaizi.
Baadhi ya waandishi wanaeleza kuwa vitamin K huweza kusaidia kuondosha ama kulinda mwili zidi ya kupata vimbe za saratani. Lakini bado hakuna ushahidi wa kisayansi wa kutosheleza kuthibitisha madai haya.
ATHARI ZA VITAMIN K
Ijapokuwa vitamin K vinafida kubwa ndani ya miili yetu kama tulivyoona hapo juu. Basi pia itambulike kuwa vitamin K vikizidi zaidi ndani ya miili yetu vinaweza kusababisha madhara ya kiafya kama;-
Kama vitamin K itakuwa ni nyingi ndani ya mwili inaweza kupelekea athari kwenye figo. Pia inaweza kuhatarisha afya ya ini kama itatumika kwa kiwango kikubwa zaidi. Inaweza kuhatarisha ugandaji wa damu kwenye ini. Ni K vinaweza kushusha kiwango cha sukari hivyo kwa wenye kisukari itakuwa ni vyema akiwa chini ya uangalizi wa daktari kama anatumia dozi ya vitamin K.
UPUNGUFU WA VITAMIN K
Kama tulivyoona kazi za vitamin K katika miili yetu sasa hebu tuone ni zipi Athari za upungufu wa vitamin hivi ndani ya miili yetu
Mwisho
Vitamini K unaweza kuvipata kwa njia ya chakula ama kwa kumeza vidonge. Kwa wale ambao wana upungufu na vitamin unaweza kununua vidonge vya vitamin kwa kufuata maelekezo ya daktari. Usiwache kuwa nasi kwa kupata makala nyingine zaidi za afya hapa kwetu.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 4132
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Kitabu cha Afya
👉6 Kitau cha Fiqh
Vyakula vya protini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya protini Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula Maini
Soma Zaidi...
MATUNDA YENYE VITAMINI C KWA WINGI
Matunda yenye vitamni C kwa wingi ni machungwa, maembe, ndimu na limao, endelea kusoma Soma Zaidi...
Ulaji wa protini kupitiliza
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu athari za ulaji wa protini kupitiliza Soma Zaidi...
vitamini B na makundi yake
Makala hii inakwenda kukuletea kazi za vitamini B, pia tutajwenda kuona makundi ya vitamini B na kazi za kila kundi. Pia makala hii inakwenda kukufundisha vyanzo na vyakula vya vitamini B. Utajifunza pia kazi kuu za vitamini B kw Soma Zaidi...
NI ZIPI KAZI ZA PROTINI MWILINI?
Makala hii inakwenda kukuletea kazi kuu za protini na vyakula vya protini katika miili yetu. Mkala hii itakusaiidia kujuwa namna ya kupangilia lishe yako kiusalama zaidi baada ya kujuwa kazi za protini katika miili yetu. Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kunywa maziwa
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kunywa maziwa Soma Zaidi...
Fahamu Vitamini E na nz kazi zake, vyakula vya vitamini E na athari za upungufu wake
Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake Soma Zaidi...
Vyakula anavyopaswa kutumia mwenye matatizo ya uti wa mgongo
Posti hii inahusu zaidi vyakula anavyopaswa kutumia mwenye matatizo ya uti wa mgongo, ni vyakula ambavyo upunguza makali kwenye uti wa Mgongo. Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula maharagwe, njegere, kund na mbaazi
Soma Zaidi...
Faida za kula parachichi
Somo hili litakwenda kukueleza na kukuelimisha kuhusu umuhimu wa kula parachichi kiafya Soma Zaidi...
Faida za kula papai
Posti hii inaonyesha Faida za kula papai.papai Ni tunda na Lina leta afya,nguvu na kuujenga mwili. Soma Zaidi...