picha

Faida za kiafya za kula tunda pera

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tunda pera

FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA TUNDA PERA

Pera ni katika matunda yanayopatikana maeneo mengi duniani. Tunda hili ni katika matunda yenye kutia afya zaidi katika miili yetu hasa kwa wale wenye maradhi sugu. Tunda hili hutumika mapaka majani yeke na kuleta faida nyingi sana. Hata wazee wetu wa zamani walikuwa wakitumia mmea huu kwa ajili ya tiba asili. Sasa hebu tuanze kuziona faida hizo:-

 

1.pera huweza kushusha kiwango cha sukari kwenye damu. Ijapokuwa tunda hili lina utamu lakini ni katika matunda ambayo ni mujarabu kwa kushusha kiwango cha sukari. Hii ni habari njema kwa wenye kisukari na wale wenye tatizo la homoni ya insulin. Hapa tunazungumzia majani ya mpera ni si tunda lenyewe.

 

Katika tafiti iliyofanyiwa watu 19 imethibitisha kuwa kunywa majimaji yatokanayo na majani ya mpera husaidia katika kushusha kiwango cha sukari na athari hii huweza kuendelea mpaka masaa mawili. Tafiti nyingine aliyofanyiwa watu 20 wenye aina ya kisukari type 2 diabetes waliligundulika kuwa kunywa majani ya mpera kumeshusha sukari kwa asilimia 10%.

 

1.Pera husaidia katika kuimarisha na kulinda afya ya moyo. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa pera lina mitamini vingi pamoja na antioxdant nyingi. Ambapo kwa pamoja vitu hivi husaidia katika kulinda moyo usiharibiwe na mionz na mambo mengine.

 

Pia kiwango cha madini ya potassium (chumvi) iliyomo kwenye pera pamoja na kambakamba zilizomo kwenye pera husaidia katika kuimarisha afya ya moyo. Pia ulaji wa mapera unaweza kuondoa cholesterol zilizo mbaya (LDL cholesterol) na kuongeza cholesterol nzuri). Hivyo hupunguza nafasi ya kupata maradhi ya shinikizo la damu la juu yaani presha ya kupanda na kupata kiharusi yaani kupalalaizi. (stroke).

 

1.Husaidia kupunguza maumivu ya tumbo la chango kwa wanawake. Wanawake wengi wanapata maumivu makali wakati wa siku zao. Tafiti zinaonesha kuwa kunywa majani ya mpera husaidia katika kupunguza maumivu haya.

 

Tafiti iliyofanyiwa wanawake 197 ambao huwa wanapata maumivu wakati wa kupata sikuzao, tafiti imeonesha kuwa unywaji wa miligram 6 za maji ya majani ya mpera husaidia kupunguza maumivu haya. Pia utafiti zaidi umeonesha kuwa majani ya mpera husaidi kupunguza maumivu haya mara dufu tofauti na kutumia dawa za kupunguza maumivu. Pia tafiti zinaonesha kuwa majani ya mpera hupunguza maumivu wakati wa kukojoa kwa wale wanaopata maumivu haya.

 

1.Husaidia katika mmeng’enyo wa chakula. Pera ni katika matunda yenye kambakamba kitaalamu hufahamika kama fiber. Hizi husaidia katika kuboresha mchakato wa kukimeng’enya chakula uende vyema. Hivyo husaidia kutokupata tatizo la kutokupata choo. Tafiti zinaonesha kuwa pera moja hukusanya asilimia 12% ya fiber zinazohitajika mwilini kwa siku.

 

Pia majani ya pera yakitengenezwa majimaji yake husaidia katika kuboresha afya ya mfumo mzima wa mmeng’enyo wa chakula. Kwa wale wenye tatizo la kuharisha majani ya mpera ni mujarabu sana katika kuondoa ama kupunguza tatizo. Pia kuna tafiti nyingi zinaonesha kuwa pera husaidia katika kuuwa vijidudu vibaya ndani ya matumbo yetu.

 

1.Husaidia katika kupunguza uzito. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa pera husaidia katika kupunguza uzito. Ni kuwa pera lina calory chache na lina fiber nyingi. Kwa pamoja hizi husaidia katika kumfanya mtu ahisi kushiba mapema na hivyo kumpunguzia kula sana. Hali hii husaidia katika kupunguza uzito mwili.

 

1.Husaidia kulinda mwili dhidi ya maradhi ya saratani (cancer). Tafiti zinaonesha kuwa pera lina anticancer effect hizi hisaidi sana miili yetu kuzuia uwezekano wa kupata maradhi ya saratani au kansa, pia husaidia kuuwa seli za saratani ndani ya miili yetu.

 

1.Huboresha mfumo wa kinga mwilini. Pera ni katika matunda yenye vitamini C vingi. Na ijulikane kuwa vitamin C ni katika vitamini ambavyo husaidia kuupa nguvu mwili kwa ajili ya kupambana na maradhi.

 

1.Huboresha afya ya ngozi. Kwa afya njema ya ngozi, pera ni mujarabu katika kuhakikisha ngozi inabakia salama muda wote. Kuondoa mikunyomikunjo kwenye ngozi, na kuuwa baadhi ya bakteria kwenye ngozi na kuondoa chunjua

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2021-10-30 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 2465

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 ai web app    👉2 Dua za Mitume na Manabii    👉3 web hosting    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

VYAKULA VYA FATI, PROTINO NA WANGA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
je ni vipi vyakula vyenye protini kwa wingi?

Makala hii iatakuletea aina kuu tano za vywkula vyenye protini nyingi zaidi. Kama ulikuwa unajiuliza kuwa ni vyakula ipi hasa vinaweza kukupatia protini kwa wingi ni vipi, makala hii ndio majibu yako kwa swali hilo.

Soma Zaidi...
vyakula vya kuongeza damu, dalili zake na sababu za upungufu wa damu

Zijuwe sababu za upungufu wa damu, dalili za upungufu wa damu na kazi za damu mwilini,n avyakula vya kuongeza damu

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula topetope/ accustard apple

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula topetope/ accustard apple

Soma Zaidi...
Kazi kuu tatu za Vitamini C mwilini

Vitamini C tunaweza kuvipata kwenye matuinda kama machunwa vina kazi kuu tatu ambazo ni hizi hapa

Soma Zaidi...
FAIDA ZA MATUNDA

Somo hili linakwenda kukuletea faida za MATUNDA mbalimbali na mboga, upatikanaji wake na faida zake kiafya. Pia utakwenda kuona MATUNDA na mboga ambayo Ni kinga dhidi ya maradhi hatari Kama kisukari, saratani, maradhi ya moyo na mfumo wa fahamu pamoja na

Soma Zaidi...
Vyakula na ugonjwa wa kisukari

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya vyakula vimpasavyo mgonjwa wa kisukari

Soma Zaidi...
Vyakula salama na vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo

Kamala hii inakwenda kufundisha vyakuna na vinjwaji salama anavyopaswa kutumia mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Pia utajifunza vyakula na vinywaji hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Soma Zaidi...