Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake
Vitamini E ni moja kati aya vitamini ambavyo vinapatikana kwenye vyakula, matunda na mboga. Pia unaweza kuvipata kwa njia ya vidonge kutoka kwenye maduka ya madawa. Kama vilivyo vitamini A, B, C, D na K vitamini E navyo endapo vitapungua mwilini kutakuwepo na madhara kiafya. Ijapokuwa upungufu wa vitamini hivi ni aghalabu sana kutokea. Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake.
YALIYOMO:
Maana ya Vitamini E
Mnamo mwaka 1922 wanasayansi wawili kwa majina ya Herbert Mclean Evans na mwenzie Katharine Scott Bishop waligundua vitamini E. baada ya ugunduzi wa vitamini E tafiti mbalimbali ziilifanywa katika kuonyesha ni zipi kazi za vitaini E mwilini. Kwa mfano Mwaka 1946 wanasayansi walikuwa wakifanya tafiti juu ya nadharia inayodai kuwa vtamini E husaidia dhidi ya maradhi ya moyo na mishipa ya damu (coronary heart diseases). mwaka 1949 tafiti zilifanywa kuhusu nadharia ya kuwa vitamini E huweza kusaidia watoto njiti kuwakinga na maradhi kadhaa.
Kazi za vitamini E mwilini
Vitamini E katika miili yetu zina kazi kuu zifuatazo:
Vitamini E bi antioxidant, ndani ya miili yetu husaidia katika kuzuia athari za kemikali mbaya zifiharibu miiliyetu.
Husaidia katika utengenezwaji wa utando wa seli,na kulinda seli dhidi ya uharibifu wa kemikali.
Husaidia katika ukuaji mzuri wa misuli.
Husaidia katika utengenezwaji wa utando maeneo mbalimbali ya mwili kama kwenye neva, mapafu, na maeneo mengine
Upungufu wa vitamini E
Upungufu wa vitamini E hutokea nadra sana lakini tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E vikipungua mwilini vinaweza kusababisha matatizo kwenye mfumo wa fahamu., ukuaji mzuri wa misuli na udhaifu wa misuli. Pia upungufu wa vitamini E unaweza kuathiri macho na hivyo kupelekea mtu kutoona vizuri.
Vyakula vya vitamini E
Tafiti mbalimbali kuhusu vitamini E
Tafiti hizi zilifanya lakini zinahitaji kuendelea zaidi maana bado majibu ya uhakika hayajapatikana juu ya matokeo ya tafiti hizo. Ijapokuwa maneno ni kama hivyo lakini ukweli ni kuwa vitamini E vina faida katika afya zetu:-
1. Mwaka 2017 tafiti zilifanya na kuonyesha kuwa vitamini E husaidia katika kupunguza udhaifu wa misuli wakati wa kuzeheka
2. Tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E husaidia katika kulinda mtu dhidi ya maradhi ya ubongo kama kusahausahau na kuchanganyikiwa.
3. Tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E mwilini husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya figo, kibofu, mapafu na korodani.
4. Husaidia kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo na mishipa ya damu
5. Husaidia kwa wajawazito
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 4259
Sponsored links
👉1
Kitau cha Fiqh
👉2
kitabu cha Simulizi
👉3
Kitabu cha Afya
👉4
Madrasa kiganjani
👉5
Simulizi za Hadithi Audio
👉6
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Karanga (groundnuts)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula karanga Soma Zaidi...
Orodha ya vyakula mbalimbali na kazi zake mwilini na virutubisho vyake
Soma Zaidi...
Faida za kula ndizi
Somo hiki linakwenda kukueleza faida za kiafya za kula ndizi Soma Zaidi...
Matunda yenye vitamini C kwa wingi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu matunda yenye vitamin C kwa wingi Soma Zaidi...
Vyakula salama na vilivyo hatari kwa mwenye kisukari, na vipi atajikinga na kisukari
Makala hii inakwenda kukupa elimu juu ya vyakula na vinywaji vilivyo salama kwa mtu mwenye kisukari, na ni vyakula vipi ni hatari kwa mwenye kisukari. Pia utajifunza njia za kujilinda na kupata kisukari. Soma Zaidi...
Faida za kula papai
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula papai Soma Zaidi...
Vyakula vya vitamin K
Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya vitamin K Soma Zaidi...
Kazi za tunda la papai katika kurekebisha homoni imbalance
Posti hii inahusu zaidi kazi za tunda la mpapai katika kurekebisha homoni.ni tunda ambalo ufanya kazi yake kwa sababu ya kuwepo kwa virutubisho muhimu ndani ya tunda hili. Soma Zaidi...
Vyakula vya vitamini C na faida zake
Soma Zaidi...
Aina za vyakula ambayo huongeza damu kwa wajawazito na watoto
Hizi ni aina za vyakula ambavyo husaidia katika kuongeza damu kwa wajawazito na watoto. Soma Zaidi...