Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu ku set time. Yaani tutaweka muda ambao code zinatakiwa ndio zilete matokeo.
Soma wazo hili:
Unatakiwa kutengeneza program ya chemsha bongo, ambapo program itauliza swali kisha mtu atatoajibu ndani ya sekunde 10 endapo hajaweka jibu ataambiwa muda umekwisha.
Sasa hapo ndipo tutahitani function ya ku set muda. Kufanya hivi kwa kutumia javascript tutatumia function unayoitaka setTimeout(). Jambo la kuzingatia ni kuwa muda hapa unahesabiwa kwa kutumia millsecond. sekunde 1 ni sawa na millsecond 1000. Hivyo ukitaka code zi fanye kazi baada ya dakika 5 hapo utaweka 5000. Sasa wacha tuone jinsi ambavyo tutaweza kuandika function yetu hii.
Kwanza utaweka function yako setTimeout() unaweza kuiweka ndani ya variable. Mfano var time = settimeout()
Pili ndani ya hiyo function utaweka statement zalo ukitengenisha na alama ya coma yaani (,) mfano var time = settimeout(function() {Document.write(“Muda umekwisha”)},)
Tatu utaweka muda unaotaka baada ya hiyo koma. Mfano var time = settimeout(function() {Document.write(“Muda umekwisha”)}, 5000).
Angalia mfano wa hapo chini
<html>
<head>
<title>Mafunzo ya javascript</title>
</head>
</html>
<body>
<h2>Jaza kitendawili hiki</h2>
<form>
<label>Haba na haba hujaza _______________</label><br><br><br>
<input type="text" placeholder="Jaza jibu hapa">
</form>
<script>
var myTimeout = setTimeout(function (){ document.write("Muda umekwisha")}, 5000)
</script>
</body>
Sasa endapo hujajaza jibu na muda ukiisha Utaletewa ujumbe huo.
Pia code hizo hapo unaweza kuzigeuza na kuziadika katika mtindo wa kuweka ku call function ndani ya setTimeout(). Matokeo ya code hizo hapo chini ni sawa na matokeo ya code hizo hapo juu.
<html>
<head>
<title>Mafunzo ya javascript</title>
</head>
</html>
<body>
<h2>Jaza kitendawili hiki</h2>
<form>
<label>Haba na haba hujaza _______________</label><br><br><br>
<input type="text" placeholder="Jaza jibu hapa">
</form>
<script>
function quiz (){ document.write("Muda umekwisha")}
var myTimeout = setTimeout(quiz, 5000)
</script>
</body>
setInterval
Sasa ikitokea unahitaji ku excute code kila baada ya muda fulani hapa utatumia setinterval. Somo la hapo juu tumezungumzia ku excute code baada ya muda fuani, lakini hapa ni kila baada ya muda fulani.
Mfano:
Umetakiwa kuweka program ya kuesabu muda yaani sekunde. Kisha uweke kwenye program ya kuuliza swali. Hivyo itakuwa ukihesabu zikitimia sekunde flani in stop.
Kufanya hivi tutatumia function ya setinterval. kwa mfano hapo tutaset program ya kuhesabu kila baada ya millsecond 1000 maana kila baada ya dakika 1.
Kanuni za kuandika setInterval ni sawa na zile za kuandika setTimeout. Kikubwa cha kuzingatio ni kuwa timeInterval itakuwa inaendelea ku excute kila baada ya huo muda ulioweka bila ya kikomo mpaka pale utakapo fanya i stop.
<html>
<head>
<title>Mafunzo ya javascript</title>
</head>
</html>
<body>
<p id="showTime"></p>
<script>
var hesabu = 0;
var muda = setInterval(function (){
hesabu += 1;
document.getElementById("showTime").innerHTML = hesabu;
}, 1000);
</script>
</body>
Unaweza kuweka timeinterval zaidi ya moja kwenye code, pia unaweza kucanganya na setTimeout zaidi ya moja kweye ukurasa mmoja. Sasa kama nilivyo kueleza kuwa code zitaendelea ku excute kila baada ya muda fulani, mpaka utakapo sitisha kufanya hivyo.
Jinsi ya kusitisha timeInterval() na setTimeout():
ili kuweza kusitisha settimeout() tutatumia method hii clearTimeout() na ukitaka kusitisha setinterval() tutatumia method hii clearInterval()
Mfano 1: kusitisa setinterval
<html>
<head>
<title>Mafunzo ya javascript</title>
</head>
</html>
<body>
<p id="showTime"></p>
<button onclick="sitisha()">Sitisha Muda</button>
<script>
var hesabu = 0;
var muda = setInterval(function (){
hesabu += 1... Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu Umeionaje Makala hii.. ? Katika somo hili tutakwenda kujifunza khusu while loop na do while loop. Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function kwenye javascript. Utajifunz apia namna ya kuitumia function hiyo Ksomo hili litakwenda kukufundisha kuhusu object kwenye javascript, kazi zake na sheria zake katika kuiandika. Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza ku display matokeo ya code za javascript. Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza kutumia javascript kutengeneza kikokotoo cha hesabu yaani calculator Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu array pamoja na method zinazohusiana na array. Pia nitakujuza tena kuhusu array ni nini. Utajifunza pia jinsi ya kutengeneza array. Hii ni game ambayo utafikiria namba, ambayo inatakiwa iwe sawa na namba ambayo game imeiweka. Katika somo hili utakwenda kujifunza sheria ama syntax za kuandika javascript. Hii itakuwezesha kuelwa zaidi code za javascript. Katika somo hili utakwenda kujifunza baadhi ya function maaumu zinazotumika kwenye string yaani string method. Kwa kutumia mfano huu na iliyotangulia unaweza kuweka masharti kadiri uwezavyo. Tukutane somo linalofuata tutajifunza kuhusu switch statement.
👉1
Bongolite - Game zone - Play free game
👉2
Tafasiri ya Riyadh Swalihina
👉3
Kitau cha Fiqh
👉4
Kitabu cha Afya
👉5
Madrasa kiganjani
👉6
kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
JAVASCRIPT - somo la 21: Jinsi ya kutumia while loop na do while loop
JAVASCRIPT - somo la 9: Jinsi ya kuandika function kwenye javascript
JAVASCRIPT - somo la 10: Jinsi ya kuandika object na matumizi yake kwenye javascript
JAVASCRIPT - somo la 2: Jisi ya ku print output ya code za javascript.
JAVASCRIPT - somo la 23: Jinsi ya kutengeneza calculator yaani kikokotoo cha hesabu kwa kutumia javascript
JAVASCRIPT - somo la 13: Function zinazofanya kazi kwenye array.
Game 3: Mchezo wa kufikiria namba kwa kutumia javascript
JAVASCRIPT - somo la 3: sheria za uandishi wa code za javascript yaani syntax za javascript
JAVASCRIPT - somo la 11: function maalumu zinazotumika kwenye string yaani string method
JAVASCRIPT - somo la 18: Jinsi ya kutumia switch case kwenye javascript