Katika somo hili utajifunza kuhusu matendo ya hesabu ambayo ni kugawanya, kujumlisha, kuzidisha na kutoa
MATENDO YA KIHESABU
Somo hili litakwenda kukujulisha namna ya kutumia matendo ya kihesabu katika javascript. matndo ya kihesabu ni muhimu sana katika kutengeneza program za kikompyuta.
Katika program za kihesabu alama za matendo ya kihesabu huitwa operator na namba ambazo hutumika kwenye hesabu huitwa operand.
Matendo ya kihesabu (operator) ni kama:-
Kujumlisha +
kutoa -
kigawanya /
kuzidisha *
modulus % hii hutumika kwenye kugawanya na kubakia
increment ++
decrement –
1. Kujumslisha
Kama tulivyoona hapo juu kujumlisha namba tunatumia alama ya jumlisha ambayo ni +.
Mfano 1
<script>
var a = 4
var b = 5
var c = a + b
document.write(c)
</script>
hii itatupa matokeo ya 9
Pia unaweza kutumia alama hii ya kujumlisha kuunganisha string zaidi ya moja. String ni mkusanyiko wa namba na herufi ama herufi tupu. Angalia mfano wa hapo chini
Mfano 2
<script>
var a = 'juma';
var b = 'Ali'
var c = a + b
document.write(c)
</script>
hii itakupa matokeao haya
Utaona neno juma na Ali yameungana kutengeneza jumaAli. Katika hali ya kawaida ya kiuandishi yanatakiwa yasomeke juma Ali kwa kuacha nafasi katikati yao. katika javascript ktatuwa changamoto hii tutatumia alama ya kujumlisha +” “ + angalia mfano hapo chini:-
Mfano 3
<script>
var a = 'juma';
var b = 'Ali'
var c = a +" "+ b
document.write(c)
</script>
Hii itatupa matokeo haya
Pia unaweza kujumlisha string na namba. Angalia mfano hapo chini
Mfano 4
<script>
var a = 'bongo';
var b = 5;
var c = a + b;
document.write(c)
</script>
Hi itatupa matokeo haya:
Mfano 5
<script>
var a = '7';
var b = 5;
var c = a - b;
document.write('Jibu ni' + " "+ c)
</script>
Hii itakupa matokeo haya
Katika mfano huo hapo juu jibu 75 yaa ni 7 na 5 na sio namba sabini na tano. Ni kwa sababu namba 7 imetumika kama string na ndio maana utaiona ipo ndani ya alama hizi '7'
2. Kutoa
Ili kutoa namba tunatumia alama ya - kama inavyotumika kwenye hesabu. Utaweza kutoa namba kubwa kutoa ndogo, ama nndogo kutoa kubwa na jibu litakuja kwenye negative yaani hasi. Angalia mifano hapo chini
Mfano 6
<scri">...
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza ku display matokeo ya code za javascript.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutumia forOfLoop. Hii ni aina ya loop ambayo yenyewe inahusisha item zote kwenye array.
Soma Zaidi...Kwa kutumia mfano huu na iliyotangulia unaweza kuweka masharti kadiri uwezavyo. Tukutane somo linalofuata tutajifunza kuhusu switch statement.
Soma Zaidi...Ksomo hili litakwenda kukufundisha kuhusu object kwenye javascript, kazi zake na sheria zake katika kuiandika.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza baadhi ya function maaumu zinazotumika kwenye string yaani string method.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu historia ya javacsript pamoja na kazi za javascript. Pia utayajuwa makampuni makubwa yanayotumia javascript.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function kwenye javascript. Utajifunz apia namna ya kuitumia function hiyo
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kupangilia muonekano wa maandishi (text) wakati wa ku out put matokeo ya code
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu array pamoja na method zinazohusiana na array. Pia nitakujuza tena kuhusu array ni nini. Utajifunza pia jinsi ya kutengeneza array.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunz kuhusu baadhi ya function ambazo hutumika kwenye namba
Soma Zaidi...