Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia logical operator kwenye javascript. Katika somo hili tutakwenda kutumia mahesabu.
Katika somo hili tutajifunza ulinganivu wa thamani (value) kwa kutumia logic operator. Somo hili ni muhiimu sana kwa wanaotarajia kujikita zaidi kwenye matumizi ya javascript.
Kwa wale wanaokumbuka hesabu hapa tutaangalia matumizi ya alama zifuatazo kwenye javascript. Alama hizo ni kama zinazoonyehswa hapo chini.
Kwa wale ambao tumepita shule zamani alama hizo zinamaanisha hivi
Pia kuna hizi
Hebu tuone maana yake kila moja wapo. Pia tutajifunza zaidi kila tutakavyokwenda mbele ya somo hili. kwa sasa tutajifunza kwa ufupi maana zake tu.
Tutatumia mifano kama ifuatavyo:-
alama ya ==
Tunajuwa kuwa 4 sio sawa na 5. Sasa kama kweli tunataka itupe jibu la false. code hizo hapo chini zinamaanisha 4 ni sawa sawa na 5, ambapo ni uwongo yaani false.
<script>
let x = 4;
let b = 5;
//alama ya sawa sawa ==
document.write( x == b)
</script>
Kwa kuwa 100 ni sawa sawa na 100 tunahitaji tuone majibu kuwa true yaani kweli
<script>
let x = 100;
let b = 100;
//alama ya sawa sawa ==
document.write( x == b)
</script>
Alama ya ===
Katika mfano hapo chini 5 == ‘5’ hii ni true kwa kuwa thamani zao wote ni sawa ni 5.
<script>
//alama ya sawa sawa ==
document.write( 5 == '5')
</script>
Lakini 5===’5’ itatupa majibu false kwa sababu 5 ya kwanza ni namba na 5 ya pili ni string kwa sababu ipo ndani ya alama za string. Hivyo thamani zao ni saswa lakini aina zao sio sawa moja ni namba na nyingine ni string.
<script>
//alama ya sawa sawa ==
document.write( 5 === '5')
</script>
lakini hii 5===5 itatupa majibu ya true kwa sababu thamani zao ni sawa na zote ni data za aina moja yaani namba.
<script>
//alama ya sawa sawa ==
document.write( 5 === 5)
</script>
Alama ya != (sio sawa na)
kwa kuwa 5 sio sawa na 2 basi code hii tunatarajia itupe jibu la true 5 !=2 kwa sababu alama != inamaanisha sio sawa na. Yaani 5!=2 ina maana 5 sio sawa na 2
<script>
//alama ya !=
document.write( 5 != 2)
</script>
Au 2 != 2 hii itatupa jibu false yaani sio kweli kwa sababu 2 ni sawa na 2.
<script>
//alama ya !=
document.write( 2 != 2)
</script>
Alama ya !== (sio sawa kwa thamani au sio sawa kwa aina)
3 na 2 sio sawa kwa thamani hivyo 3 !== 2 itatupa jibu la true
<script>
//alama ya !==
document.write( 2 !== 3)
</script>
Lakini 2 !== ‘2’ hii pia itatupa jibu la true kwa sababu 2 sio sawa na ‘2’ kwani mbili ya kwanza ni namba na mbili ya pili ni shtring, ndio maana ipo kwenye alama za semi.
<script>
//alama ya !==
document.write( 2 !== '2')
</script>
...
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutumia forOfLoop. Hii ni aina ya loop ambayo yenyewe inahusisha item zote kwenye array.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu condition statemant. Darasa hili ni moja katika madarasa muhimu programming. Katika somo hili tutajifunza kwa vitendo zaidi. Tutatumia mifano ya somo lililo tangulia.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kupangilia muonekano wa maandishi (text) wakati wa ku out put matokeo ya code
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza baadhi ya function maaumu zinazotumika kwenye string yaani string method.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu matendo ya hesabu ambayo ni kugawanya, kujumlisha, kuzidisha na kutoa
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu historia ya javacsript pamoja na kazi za javascript. Pia utayajuwa makampuni makubwa yanayotumia javascript.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifundisha jinsi ya kutengeneza game ya tic toc ya wachezaji wawii kwa utumia html, css na javascript
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza khusu while loop na do while loop.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function kwenye javascript. Utajifunz apia namna ya kuitumia function hiyo
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunz kuhusu baadhi ya function ambazo hutumika kwenye namba
Soma Zaidi...