Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu aina za data ambazo hutumika kwenye javascript
AINA ZA DATA ZINAZOTUMIKA KWENYE JAVASCRIPT
Aina za data ambazo javascript inatumia ni sawa na zile ambazo zinapatikana kwenye programming language nyingine kama php. Javascript inatumia aina zifuatazo:-
Namba
javascript ni tofauti na programming language zingine kama php ambapo namba kuna zenye desimali na zisizo. Kwenye javascript namba ni namba iwe na desimali ni namba ama isiwe na desimali.
Mfano 1:
<script>
let x1 = 3.04; // desimali
let x2 = 5; // bila ya desimali
document.write(x1, '<br>', x2);
</script>
Itakupa matokeo haya:
String
String ni mkusanyiko unaojumuisha namba, herufi na alama. Aina hii inachukuwa amala zote, namba zote na herufi zote. Mfano ukisema “bongoclass” hii ni string. Au ukisema “admin5@bongoclass.com” hii pia ni string ambayo ina namba, 5 alama @ pamoja na herufi. Kumbuka string siku zote inakaa ndani ya alama za kufunga na kufungua semi, kama ilivyo mifano hapo juu.
Mfano 2
<script>
let a = "bongoclass";
let b = ".com";
document.write(a, b);
</script>
Hii itakupa matokeo haya:-
Boolean
Kama ilivyo kwenye programming language zingine, bulean inabeba matokeo mawili tu true au false. Ainahii ya data pia hutumika kwenye javascript. Tulishaona mifano kadhaa katika somo lililotangulia wakati tunajifunza namna ya kutumia logic.
Mfano 3
Tunaelewa kuwa 3 ni kubwa kuliko 2. Hivyo tunatarajia itupe jibu la true kuwa ni kweli tatu ni kubwa kuliko mbili.
<script>
document.write(3 >2);
</script>
Mfano 4
Tunaelewa kuwa 5 ni kubwa kuliko 4 sasa endapo tutaandika 4 ni kubwa kuliko 5 inatakiwa itupe majibu false yaani sio kweli kuwa 4 ni kubwa kuliko 5.
<script>
document.write(4 >5);
</script>
Array
Array ni mkusanyiko wa data za aina moja ambazo huweza kufikiwa kwa jina moja. Katika javascript pia tunatumia array. Siku zote array huanzia na 0. Kwa kuwa ni mkusanyiko wa data, basi ile ya kwanza kutajwa hupewa namba 0. Na pia array siku zote hukaa ndani ya mabano [], na kila moja inakuwa ndan ya alama ya kufunga semi kama zilivyo string. Na kama list ina item nyingi kila moja hutenganishwa kwa alama ya koma ( , ). Angalia mifano hapo chini
Mfano 5:
<script>
let mti = ["mpapai", "muembe", "muarobaini"]
document.write(mti);
</script>
Kama nilivyokueleza kuwa array huanzia na 0 hivyo basi katika array hapo juu 0 ni mpapani, 1 ni muembe, na 2 ni muarobaini. Na endapo unataka kuisoma array ya 2 basi baada ya kutaja array utaweka mapbano na kuweka 2.
Mfano 6:
<script>
let mti = ["mpapai", "muembe", "muarobaini"]
document.write(mti[2]);
">...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu javascript events. Event ni neno la Kiingereza lenye maana tukio wingi wake events kumaanisha matukio. Natumia ni kila ambacho kinatokea kwenye javascript.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza khusu while loop na do while loop.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia logical operator kwenye javascript. Katika somo hili tutakwenda kutumia mahesabu.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function kwenye javascript. Utajifunz apia namna ya kuitumia function hiyo
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu historia ya javacsript pamoja na kazi za javascript. Pia utayajuwa makampuni makubwa yanayotumia javascript.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza ku display matokeo ya code za javascript.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu user input. Somo hili litaangalia html form na attribute zake na jinsi zinavyohusiana na user input. Mwisho wa somo hili utaweza kutengeneza simple Calculator kwa kutumia javascript.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutumia forOfLoop. Hii ni aina ya loop ambayo yenyewe inahusisha item zote kwenye array.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika variable. Hapa utajifunza sheria zinazohusu variable katika javascript
Soma Zaidi...Katika project hii utakwenda kufunza jinsi utakavyoweza kutengeneza keyboard ya online kwa kutumia javascript
Soma Zaidi...