image

JAVASCRIPT - somo la 13: Function zinazofanya kazi kwenye array.

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu array pamoja na method zinazohusiana na array. Pia nitakujuza tena kuhusu array ni nini. Utajifunza pia jinsi ya kutengeneza array.

Array ni nini? 

Array ni variable ambayo ina item zaidi ya moja. Array poa ni object.  Mfano unataka kutengeneza variable ambayo itawakilisha aina za magari. Katika hali ya kawaida itakubidi kutengeneza kwa kila aina ya gari na variable yake. Hivyo utasema var a = "Toyota", var b ="benzi", var c = "basi" sasa kupunguza kazi hii ya kuweka kila item na variable yake, hapa tutatumia array. Hivyo tutasema

var gari ={"Toyota", "Benzi", "basi"}

 

Utaona hapo imekuwa rahisi kuwa baada ya kuwa na variable 3 sasa una variable moja tu. 

 

Jinsi ya kutengeneza array

Array inaweza kutengenezwa kwa njia kuu mbili ambazo ni kwa kutumia njia ya mabano [] kisha kila item inatengenishwa na alama ya kima (,) ila item ya mwisho haiwekewi koma. Njia ya pili ni kwa kutumia constructor ambayo ni new Array(). Wataalamu wanapendekea kutumia njia ya kwanza nilitaka kwa kuwa ipo fasta zaidi. 

 

<!DOCTYPE html>

<html>

<head>

   <title> njia ya mabano</title>

</head>

<body>

   <p id="demo"></p>

 

   <script>

      var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

      document.getElementById("demo").innerHTML = magari;

   </script>

</body>

</html>

 

Hiyo hapo juu ni njia ya mabank kama unavyoona hapo. Sasa wacha tuone kwa kutumia constructor. Katika njia hii kumbuka keyword inaanza na A kubwa yaani Array na sio array. 

<!DOCTYPE html>

<html>

<head>

   <title> njia ya constructor</title>

</head>

<body>

   <p id="demo"></p>

 

   <script>

      var magari =new Array ("yoyota", "Benzi", "NoAH");

      document.getElementById("demo").innerHTML = magari;

   </script>

</body>

</html>

 

Jinsi ya ku access array

Hapa tunazungumzia jinsi ya kupata output ya array. Ama jinsi ya kutumia hiyo array. Hapa pia tutaona jinsi ya kuifikia na kuitumia kila item kivyake vyake ama kwa ujumla. Kwa mfano katika mifano miwili hapo juu item zimetumika kwa ujumla ndio maana imepata matokeo ya item zote. 

 

 

Ili kuitumia arry kwanza ujuwe index yake. Index ni Idd ya hiyo array. Kwa mfano kama una array tatu kila moja ina is yake.  Na huhesabiwa kuanzia 0. Ya kwanza hupewa 0, ya pili hupewa 1 na ya tatu hupew 2. 

 

Mfano una array hii var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

Katikabarray hiyo toyota ina index ya 0, Benzi index ya 1 na Noah index ya 2. Hivyo basi kama tunataka ku output benzi tutatumia index namba yake ambayo ni 1. 

Mfano. 

 

<script>

  var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

document.write(magari[1]);

</script>

 

Baadhi ya method zinazotumika kwenye array: 

Kwa kuwa tunaelewa maana ya array,  na jinsi ya kuitengeneza pia tunajuwa jinsi ya ku access array sasa hapa tutakwenda kuona baadhi ya Method (functions) zinazotumika kwenye array. 

 

push()

Hii hutumika kuongeza item mwisho wa array. Unaweza kuongeza item zaidi ya moja, utazitenganisha kwa alama ya (;).

Mfano kwenye array yetu ya magari tunakwenda kuongeza magari mawili ambayo ni BMW na Bugati kufanya hivi tutatumia method ya push()

 

<script>

  var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

magari.push("BMW", "Bugati");

document.write(magari);

</script>

 

unshift()

Hii hutumika katika kuongeza item mwanzoni mwa array. Unaweza kuongeza item moja ama zaidi. Sasa wacha tuiongeze BMW na Bugati mwanzoni mwa array yetu. 

<script>

  var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

magari.unshift("BMW", "Bugati");

document.write(magari);

</script>

 

pop()

Hii hutumika katika kuondoa item ya mwisho katika array. Kwa mfano array yetu ya magari item yavnwisho ni  NoAH.  Hivyo kwa kutumia Method hii unaweza kuondoa kabisa item hiyo. 

<script>

var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

magari.pop();

document.write(magari);

</script>

Pia unaweza kutumia hiyo pop() method kupata item ya mwisho. Kwa mfano

<script>

var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

document.write(magari.pop());

</script>

 

shift()

Hii hutumika katika kuondoa item ya kwanza kwenye array. Kwa mfano katika array yetu ya magari tutakwenda kuondoa Toyota 

<script>

var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

magari.shift();

document.write(magari);

</script>

 

Pia kwa kutumia Method hiyo hiyo unaweza kupata item ya kwanza kwenye array. 

Mfano

<script>

var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

document.write(magari.shift());

</script>

length property

Hii hutumika kupata length of arry yaani kujuwa je hiyo array ina item ngapi. Inafanya kazi sawa na ile length of the string. Tutatumia array yetu ya magari kujuwa ina item ngapi? 

<script>

var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

document.write(magari.length);

</script>

 

Kwa kutumia length property pia unaweza kupata array ya mwisho yaani last array. 

<script>

var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

document.write(magari[magari.length -1]);

</script>

 

 

forEach()

Hii hutumika ku access item zote kwenye array. Method hii ina parameter 3 ambazo ni: 

i kumaanisha array index

val kumaanisha array value

arr hii ni array yenyewe. 

 

Kwa kutumia Method hii unaweza kupata index ya kila item au array. BPia value zake. 

 

<script>

var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

magari.forEach(function(val, i, arr) {

document.write(i + ": " + val + "<br>");

      });

</script>

 

join()

Hii hutumika kubadili array kuwa string, kisha huubganisha item katika namna utakayitaka. Kwa mfano unaweza kutenganishabkwa kma (,) au kwa slash (/) ama kwa hyohen (-) ama  anaomba yeyote utakayitaka. Utakachofanya ni kuweka hiyo alama kwenye join(). Mfano join("-") au join("/") au join(;)

Mfano: 

<script>

var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

document.write(magari.join("-"));

</script>

 

<script>

var magari = ["yoyota", "Benzi", "NoAH"];

document.write(magari.join(" "));

</script>

 

split()

Hii hutumika kubadili string kuwa array. Itakachofanya ni kuangalia katika hiyo string kila ambako kunewachwa nafasi itakuwa ni string. Kitu cha muhimu ni kuwacha nafasi kwenye method. Mfano Kama web imetumika sana utalipa kikubwa na kama umetumia kidogo utalipa kidogo. split(" ") hapo itagawa kila kwenye nafasi kuwa array item. Mfano hii sentensi mama na baba wanalima hapa utapata array item 4. Ila ka kwenye split hukuacha nafasibumeandika hivi split("") hapo kila herufi iitahesabika ni item ya string. 

<script>

var str = "mama na baba wanalima";

document.write(str.split(" "));

</script>

 

Hiyi hapo ni array ambayo unaweza fanya kila kitu kinachohusu array. Kwa mfano tunataka ku access array yenye index 2

<script>

var str = "mama na baba wanalima";

var arr =str.split(" ");

document.write(arr[2]);

</script>

 

concat()

Hii hutumika katika kuunganisha array zaidi ya moja kuwa array moja. Mfano una list tatu za array ambazo ni

array1 ["viazi", "mihogo", "magimbi"]

array2 ["nyanya", "ndimu", "pilipili"]

array3 ['nazi", "karanga", "maharagwe"]

 

Sasa list hizi tatu utaweza kupata list moja kwa kuziunganisha. Tunapounganisha hapo tunaunganisha hiyo ya jwanza na hizo za pili mbili. 

Mfano: 

<script>

var array1 =["viazi", "mihogo", "magimbi"];

var array2 =["nyanya", "ndimu", "pilipili"];

var array3 =["nazi", "karanga", "maharagwe"];

var arr = array1.concat(array2,array3);

 

document.write(arr);

</script>

 

indexOf()

Hii hutumika kutafuta array kuwa je ipo na kama ipo ina index gani. Kama jina linavyo jieleza indexOf maana yake unatafuta index ya hiyo array ambayo utaitaja. Kama hapa kama array hiyo imejirudia zaidi hapa utapata index ya ile ya kwanza ilioanza kutajwa kwenye list. 

 

Kwa mfano tuna lita hapa inahusu vinywaji.  soda, juisi, maziwa, asali, na maji sasa mfano tunataka kutafuta je katika list maziwa yapo na kama yapo ni index ya ngapi. 

<script>

var vinywaji =["soda", "juisi", "maziwa", "maji"];

 

document.write(vinywaji.indexOf("maziwa"));

</script>

Utaona hapo inetoa jibu 2 kumaanisha kuwa maziwa yapo na index yake ni 2.endapo hayatakuwepo ama kitu unachokitafuta hakipo italeta -1.

 

lastIndexOf()

Hii ni kinyume cha indexOf hii yenyewe endapo zimejirudia zaidi ya mara moja itakupa matokeo ya ile ya mwisho kutokea. Rejea method ya indexOf na lastIndexOf kwenye string zinafanana matumizi yake. 

<script>

var vinywaji =["soda", "juisi", "maziwa", "fanta", "maji", "maziwa"];

 

document.write(vinywaji.lastIndexOf("maziwa"));

</script>

Utaona hapo imekupa jibu 5 kwa k">...           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2023-10-20 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 171


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

JAVASCRIPT - somo la 15: Jinsi ya kukusanya user input
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu user input. Somo hili litaangalia html form na attribute zake na jinsi zinavyohusiana na user input. Mwisho wa somo hili utaweza kutengeneza simple Calculator kwa kutumia javascript. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 22: Jinsi ya ku set time na tarehe
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu ku set time. Yaani tutaweka muda ambao code zinatakiwa ndio zilete matokeo. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 18: Jinsi ya kutumia switch case kwenye javascript
Kwa kutumia mfano huu na iliyotangulia unaweza kuweka masharti kadiri uwezavyo. Tukutane somo linalofuata tutajifunza kuhusu switch statement. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 5: Jinsi ya kupangilia maandishi wakati wa ku output kwenye javascript
Katika somo hili utajifunza jinsi ya kupangilia muonekano wa maandishi (text) wakati wa ku out put matokeo ya code Soma Zaidi...

Game 1: Jinsi ya kutengeneza game ya tic toc ya wachezaji wawili kwa kutumia html, css na javascript
Katika post hii utakwenda kujifundisha jinsi ya kutengeneza game ya tic toc ya wachezaji wawii kwa utumia html, css na javascript Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 19: Jinsi ya kutumia loop kwenye javascript
Katika somo hilibtutakwenda kujifunza kuhusu loop. Katika programming tunaposema loop tunamaanisha ile hali ya program ku excute code zaidi na zaidi. Tofauti na kurudia rudia kuandika statement moja kwa ajili ya kupata matokeoa hayohayo basi unapotumia lo Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 3: sheria za uandishi wa code za javascript yaani syntax za javascript
Katika somo hili utakwenda kujifunza sheria ama syntax za kuandika javascript. Hii itakuwezesha kuelwa zaidi code za javascript. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 24: Jinsi ya kutengeneza online keyboard
Katika project hii utakwenda kufunza jinsi utakavyoweza kutengeneza keyboard ya online kwa kutumia javascript Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 10: Jinsi ya kuandika object na matumizi yake kwenye javascript
Ksomo hili litakwenda kukufundisha kuhusu object kwenye javascript, kazi zake na sheria zake katika kuiandika. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 17: condition statement za if else, else if kwenye javascript
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu condition statemant. Darasa hili ni moja katika madarasa muhimu programming. Katika somo hili tutajifunza kwa vitendo zaidi. Tutatumia mifano ya somo lililo tangulia. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 2: Jisi ya ku print output ya code za javascript.
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza ku display matokeo ya code za javascript. Soma Zaidi...

Game 2: Jinsi ya kutengeneza tic toc game ya single player kwa kutumia javascript, html na css
Katika post hii utakwenda kujifunza kutengeneza game ya tic toc ya mchezaji mmoja na kompyuta yaani single player Soma Zaidi...