Kwa kutumia mfano huu na iliyotangulia unaweza kuweka masharti kadiri uwezavyo. Tukutane somo linalofuata tutajifunza kuhusu switch statement.
Switch statement haina utifauti na if else ama kiweka if. Chukulia mfano huu hapa
Unatakiwa uandae program ya dictionary, yenyewe utaandika neno kwa kiswahili kisha utaletewa kiongereza chake.
Ili kutengeneza program hii tutakwendabkutumia maneno yafuatayo kama mfano
Father - baba
Mother - mama
Sister - dada
Uncle - mjomba
Aunt - shangazi
Nephew or cousin - mpwa
Cousin - binamu
Brother - kaka
Sasa program hii tutaanza kuitengeneza kwa kutumia if tupu, kama ambavyo tuliona katika somo lililotangaulia. Pia unaweza kutumia else if kama tulivyojifunza.
<html>
<head>
<title>Mafunzo ya javascript</title>
</head>
<body>
<script>
let neno = prompt("weka neno la kiswahili kwa herufi ndogo");
if(neno == 'baba'){
document.write("<b style='color:blue'>Father</b>");
}
if(neno == 'mama'){
document.write("<b style='color:blue'>mother</b>");
}
if(neno == 'dada'){
document.write("<b style='color:blue'>sister</b>");
}
if(neno == 'mjomba'){
document.write("<b style='color:blue'>uncle</b>");
}
if(neno == 'shangazi'){
document.write("<b style='color:blue'>aunt</b>");
}
if(neno == 'mpwa'){
document.write("<b style='color:blue'>nephew or cousin</b>");
}
if(neno == 'kaka'){
document.write("<b style='color:blue'>brother</b>");
}
</script>
</body>
</html>
Hapo utaona kuna changamoto kuu 2
Sasa ili tuweze kupambana na hali hii ndipo tutatumia switch ambapo itaturahisishia kuthibiti changamoto hizo.
Jinsi ya kutengeneza switch
Utaanza na neno switch likifuatiwa na mabano switch () ndani ya mabano utaweka statement katika hii statement utaweka kile ambacho unakwenda kukitest. Inaweza kuwa variable ama chochote kila kitakachokuwepo kwenye statement hio. switch(statement) baada ya hapo itafuatiwa mabano{} kisha ndipo tutaanza kutest condition ambayo tutaiita value kwa kutumia neno case 'condition' utamalizia na nukta pacha : baada ya hapo utafuata kuandika statement yako yaani nini kitokee kwenye hiyo case.
switch(statement){
case value 1:
statement
case value 2:
statement
case value 3:
statement
}
Sasa wacha tuone mfano wetu wa kwanza kwa kutumia switch
<html>
<head>
<title>Mafunzo ya javascript</title>
</head>
<body>
<script>
let neno = prompt("weka neno la kiswahili kwa herufi ndogo");
switch(neno){
case'baba':
document.write("<h1>Father<h1>")
case'mama':
document.write("<h1>Mother<h1>")
case'dada':
document.write("<h1>Sister<h1>")
case'kaka':
document.write("<h1>Brother<h1>")
case'mjomba':
document.write("<h1>Uncle<h1>")
case'shangazi':
document.write("<h1>Aunt<h1>")
case'mpwa':
document.write("<h1>Nephew or niece<h1>")
}
</script>
</body>
</html>
Saaa hapo utaona kuna changamoto mbili kwenye hizo code:-
Kwanza code baada ya kuonyesha matokeo ya inputi zinaendelea kufanya kazi. Utaona hapo nimeweka neno baba sasa ikaniletea jibu father kisha ikaendelea kukaliza na list iliyobaki kutokea kwa baba.
Ili kutatua changamoto hii tutatumia break keyword yaani baada ya matokeo code zinatakiwa zi stop kufanya kazi.
Pili hapo hatukuweza kuthibiti endapo mtu ataandika ambacho hakina mfanano. Kwa mfano hapo uliandika mbuzi haitaleta majibu yeyote.
Ili kutatua tatizo hili tutatumia default keyword ambayo mi sawa na else kama tulivyoona somo lililotangalia. Hivyo basi kanuni nzima itakuwa hivi. Hii default itafanyabkazi endapo mtu ataandika kitu chochote ambacho hakipo kwenye list.
switch(statement){
case value 1:
statement
Break;
case value 2:
statement
break;
case value 3:
statement
break;
}
<html>
<head>
<title>Mafunzo ya javascript</title>
</head>
<body>
<script>
let neno = prompt("weka neno la kiswahili kwa herufi ndogo");
switch(neno){
case'baba':
document.write("<h1>Father<h1>")
break;
case'mama':
document.write("<h1>Mother<h1>")
break;
case'dada':
document.write("<h1>Sister<h1>")
bre">...
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu ku set time. Yaani tutaweka muda ambao code zinatakiwa ndio zilete matokeo.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika variable. Hapa utajifunza sheria zinazohusu variable katika javascript
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu user input. Somo hili litaangalia html form na attribute zake na jinsi zinavyohusiana na user input. Mwisho wa somo hili utaweza kutengeneza simple Calculator kwa kutumia javascript.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza kutumia javascript kutengeneza kikokotoo cha hesabu yaani calculator
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutumia forOfLoop. Hii ni aina ya loop ambayo yenyewe inahusisha item zote kwenye array.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza sheria ama syntax za kuandika javascript. Hii itakuwezesha kuelwa zaidi code za javascript.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza kutengeneza game ya tic toc ya mchezaji mmoja na kompyuta yaani single player
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu aina za data ambazo hutumika kwenye javascript
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza ku display matokeo ya code za javascript.
Soma Zaidi...Katika somo hilibtutakwenda kujifunza kuhusu loop. Katika programming tunaposema loop tunamaanisha ile hali ya program ku excute code zaidi na zaidi. Tofauti na kurudia rudia kuandika statement moja kwa ajili ya kupata matokeoa hayohayo basi unapotumia lo
Soma Zaidi...