Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza ku display matokeo ya code za javascript.
JAVASCRIPT OUT PUT
Hapa tutajifunza namna ambavyo unaweza kuonyesha matokeo ya code javascript. Yaani ilikwamba hizo code ulizoandika zionyeshe matokeo yanayotarajiwa. Kama umejifunza kuhusu PHP tunatumia print ama echo. Sasa vipi kwenye javascript nini tutatumia. Endelea na somo hili hadi mwisho.
Kabla hatujaendelea na somo zaidi, naamini unatumia text editor. Kama unatumia simu unaweza kutumia trebEdit. Kama unatumia komputa unaweza kutumia sublime text. Unaweza pia kutumia notepad, notepad plus, ama text editor yeote. Hakikisha pia una ufahamu kuhusu html angalau basic level.
Ni njia zipi javascript hutumia kuonyesha output
Kuna njia 4 ambazo hutumika kwenye javascript kuonyesha output. Njia hizo ni:-
Kwa kutumia innerHTML
Kwa kutumia document.write()
Kwa kutumia window.alert()
Kwa kutumia console.log()
Kwa kutumia innerHTML propert
Property hii hutumika kwa ajili ya ku badili maudhui ya kwenye html element, ama ku modify maudhui, ama kuweka maudhui mapya kwenye elemeny ya html. Mara nyingi hutumika kwenye element <p> lakini inawekza pia kutumika kwenye <div> na maeneo mengine.
Hii hutumika katika kufikia element za HTML. kwanza utahitajika element husika kuipa id, kisha utatumia hiyo id ili uweze kuifikia kwa kutumia javascript.
Mafano:
<!DOCTYPE html>
<html lang="swa">
<body>
<p id="mfano"></p>
<script>
document.getElementById("mfano").innerHTML = 'haloo javascript';
</script>
</body>
</html>
Kwanza element p tumeipa id ya mfano <p id="mfano"></p> Hii inamaanisha maudhui ya kwenye element p yatapatikana baada ya id ya mfano kufikiwa kwenye javascript. Ili kuweka id kwenye html element ni kama unavyotaka kuweka html attributes. Utaanza kuweka tag ya element mafano <p kisha itafata attribute id <p id itafuatiwa na alama ya = <p id = thamani ya id yaani value itakuwa ndani ya alama hizi “” kisha funga element yako <p id="mfano"></p> Baada ya hapo kinachofuawata ni kuweka code za javascript.
Tambuwa kuwa code zote za javascript huwekwa ndani ya tag za javascript. Tag za javascript ni <script> hii ni ya kufungua na </script> hii ni ya kufunga. Sasa kinachofuwata ni kuitumia id ili kuweza kupata matokeo ya javascript.
Hapa tutatumia document.getElementById() ili kuweza kuifikia id ya element yetu. Kwenye mabano hapo weka id yetu ambayo ni mfano document.getElementById("mfano") baada ya hapo kinachofuata ni kytumiaproperty ya innerHTML ili kuweza kuipa maudhui mapya elemebt yetu. Inafuata alama ya = kisha maudhui yako utaweka hapo. Kama ni string yaani mkusanyiko wa herufi na namba ama herufi tupu maudhui hayo yatakuwa ndani ya funga na fugua semi “”. Mfano wetu juu hapo tunataka kuonyesha maneno haloo javascript. Hivyo itakuwa document.getElementById("mfano").innerHTML = 'haloo javascript'; Kma ingelikuwa namba tungeweka document.getElementById("demo").innerHTML = 5 + 6;
Angalia mfano:-
<!DOCTYPE html>
<html lang="swa">
<body>
<p id="mfano"></p>
<div id="mfano2"></div>
<script>
document.getElementById("mfano").innerHTML = 'haloo javascript';
document.getElementById("mfano2").innerHTML = 5 + 6;
</script>
</body>
</html>
...
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utajifunza jinsi ya kupangilia muonekano wa maandishi (text) wakati wa ku out put matokeo ya code
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutumia forOfLoop. Hii ni aina ya loop ambayo yenyewe inahusisha item zote kwenye array.
Soma Zaidi...Katika somo hilibtutakwenda kujifunza kuhusu loop. Katika programming tunaposema loop tunamaanisha ile hali ya program ku excute code zaidi na zaidi. Tofauti na kurudia rudia kuandika statement moja kwa ajili ya kupata matokeoa hayohayo basi unapotumia lo
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function kwenye javascript. Utajifunz apia namna ya kuitumia function hiyo
Soma Zaidi...Hii ni game ambayo utafikiria namba, ambayo inatakiwa iwe sawa na namba ambayo game imeiweka.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza baadhi ya function maaumu zinazotumika kwenye string yaani string method.
Soma Zaidi...Katika project hii utakwenda kufunza jinsi utakavyoweza kutengeneza keyboard ya online kwa kutumia javascript
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza kutumia javascript kutengeneza kikokotoo cha hesabu yaani calculator
Soma Zaidi...Kwa kutumia mfano huu na iliyotangulia unaweza kuweka masharti kadiri uwezavyo. Tukutane somo linalofuata tutajifunza kuhusu switch statement.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu array pamoja na method zinazohusiana na array. Pia nitakujuza tena kuhusu array ni nini. Utajifunza pia jinsi ya kutengeneza array.
Soma Zaidi...