image

nguzo za uislamu: Kutoa zaka, lengo la kutoa zaka na faida zake

Kutoa Zakat.

nguzo za uislamu: Kutoa zaka, lengo la kutoa zaka na faida zake

NGUZO YA TATU YA UISLAMA: KUTOA ZAKA

Kutoa Zakat.
Umuhimu wa Zakat na Sadakat katika Uislamu.
i.Zakat ni nguzo ya tatu ya Uislamu.
Baada ya shahada mbili na kusimamisha swala nguzo muhimu sana katika uislamu ni kutoa zakat kama ilivyoainishwa katika hadithi.

ii.Kutoa zakat na Sadaka ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Kutoa zaka na vile tulivyoruzukiwa katika mali na huduma au misaada mbali mbali ni wajibu kwa waislamu wanaovimudu.
Rejea Qur’an (14:31) na (2:254).

iii.Kutoa Zakat ndio kitambulisho cha Uislamu na Ucha-Mungu wa mtu.
Muislamu akiacha au kukataa kutoa zakat kwa makusudi ni ishara ya kuritadi na kutoka katika Uislamu.
Rejea Qur’an (9:11) na (2:2-3).

iv.Kutoa Zakat na sadaka ni sababu ya mtu kufaulu Duniani na Akhera.
Miongoni mwa sifa za waumini na wacha-Mungu ni kutoa katika vile walivyoruzukiwa na muumba wao.
Rejea Qur’an (2:2-3), (23:1-4), (22:34-45) na (2:262,274).

v.Kutotoa Zakat na Sadaka ni sababu ya kuangamia mtu Duniani na Akhera.
Kutotoa katika vile tulivyoruzukiwa hupelekea mtu kustahiki adhabu hapa Duniani na Akhera pia.
Rejea Qur’an (9:34-35), (92:8-10) na (3:180).

Namna lengo la zakat linavyofikiwa.
Zakat na sadaka zinalengo la kutakasa mali na nafsi ya mtoaji na mpokeaji kama ifuatavyo;
i.Zakat na sadaka inavyotakasa mali ya mtoaji.
Zakat hutolewa 2.5% ya mali na kuwapa wanaostahiki, hivyo kuitakasa mali ya mtoaji kutokana na chumo la haramu na haki za watu.

ii.Zakat na sadaka zinavyotakasa nafsi ya mtoaji.
Utoaji mali kwa wanaostahiki huitakasa nafsi ya mtoaji kutokana na ubakhili, kuabudu mali, kibri, n.k katika kumiliki mali na kuwa na upole, huruma, n.k.
Rejea Qur’an (61:10-12) na (9:102-103).

iii.Zakat na sadaka inavyotakasa nafsi ya mpokeaji.
Utoaji wa zaka na sadaka kwa wanaostahiki huondoa chuki, husuda, uadui, unyonge kwa wasionacho na kuleta udugu, upendo, shukurani na ushirikiano.
Rejea Qur’an (9:60).

iv.Zakat na sadakat huitakasa jamii ya waislamu.
Utoaji wa zakat na sadaka hujenga jamii yenye udugu wa kweli, kujenga uchumi wa halali na kuondoa chuki na uadui baina ya masikini na matajiri.
Rejea Qur’an (61:4).


Kwa nini lengo la Zakat na Sadaka halifikiwi katika jamii yetu?
Pamoja na zakat na sadaka kutolewa na baadhi ya waislamu lakini malengo yake hayafikiwi, zifuatazo ni baadhi ya sababu;
i.Wengi watoao zakat na sadakat hawajui lengo lake halisi.
Waislamu wengi wanatoa zaka na sadaka kwa lengo la kupata thawabu na kufutiwa madhambi tu na sio utakaso.

ii.Waislamu wengi hawatoi zakat kabisa.
Waislamu wengi licha ya kuwa na mali na uwezo wa kutoa zakat na sadaka lakini hawatekelezi au kuhimiza wengine katika kutoa mali zao pia.
Rejea Qur’an (2:2-3).

iii.Wengi watoao zakat na sadakat hawatekelezi masharti ya utoaji.
Pamoja na matajiri wachache kutoa zakat na sadaka, lakini bado hutoa kwa ria, masimbulizi, adha na kuleta uadui na fitna katika jamii.
Rejea Qur’an (2:264).

iv.Zakat na sadaka haikusanywi na kugawanywa kijamii.
Utoaji na ugawaji wa zakat na sadaka umekuwa unafanywa kila mtu kivyake, bila mpango maalumu wa kukusanya na kugawa kwa wanaostahiki.

v.Wengi watoao zakat na sadakat chumo lao ni la haramu.
Ingawa waislamu wengi hutoa zakat na sadaka, lakini lengo na matunda yake hayafikiwi kutokana na chumo lao kuwa haramu.



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1005


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Jinsi ya kushona sanda ya maiti na kumvisha yaani kumkafini
Hapa utajifunza taratibu za kumkafini maiti wa kiislamu. Yaani kushona sanda yake na kumvisha. Soma Zaidi...

Ni upi umuhimu wa kufunga katika uislamu
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kufunga kiroho, kiafya na kijamii. Soma Zaidi...

Aina za tawafu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mtazamo na Msimamo wa Uislamu Juu ya Kudhibiti Uzaz (uzazi wa mpango) na hukumu yake
Soma Zaidi...

Jinsi ya kiswali swwla ya dhuha na faida zake
Post hii inakwenda kukufunza kuhusu swala ya dhuha, faida zake wakati wa kuiswali swala ya dhuha na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

Vipi utapata uchamungu kupitia funga
Vipi lengo la funga litafikiwa na kumfanya mfungaji awe mchamungu. Soma Zaidi...

Faida za funga
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sharti za kusihi kwa funga
Soma Zaidi...

hukumu na taratibu za biashara ya ushirika na hisa katika uislamu
Soma Zaidi...

Swala za sunnah na faida zake
Soma Zaidi...

Njia za kuzuia na kupunguza zinaa katika jamii
(ii) Hatua za Kuzuia Uzinzi JamiiUislamu pamoja na kutoa mafunzo ya maadii yanayomuwezesha mtu binafsi ajiepushe kwa hiari yake na kitendo kibaya cha zinaa, umechukua hatua mbali mbali ambazo huifanya zinaa isiwe kitendo chepesi katika jamii. Soma Zaidi...

Uzuri wa Benki za kiislamu
Kwa nini benki za kiislamu ni bora kuliko benki nyingine? Soma Zaidi...