Uislamu umekataza tabia ya kuombaomba kama ndio njia ya kuendesha maisha. Pia ukaweka suluhisho la kukomesha tabia hiyo
5
Suala la omba-omba
Tukiliangalia suala la omba-omba kwa upana kidogo, ambalo hivi sasa linaongelewa katika vikao mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, tutaona kuwa ni Uislamu pekee unaotoa namna bora ya kulishughulikia suala hili. Omba omba ni kitendo kibaya sana kikiwa kimefanywa na mtu binafsi au taifa na kinashusha hadhi ya mtu binafsi na hadhi ya taifa kwa ujumla. Hivyo Uislamu ambao ndio njia sahihi pekee ya maisha, hauwezi kamwe ukapalilia omba omba na wala Zaka na sadaka kazi yake si kupalilia omba-omba, bali kinyume chake zaka na sadaka ni miongoni mwa silaha zinazotumiwa kutokomeza omba omba. Uislamu unawashutumu vikali omba omba kama tunavyojifunza katika Hadithi ifuatayo:
Hubshi bin Junadah ameeleza kuwa Mtume wa Al-lah amesema: Kuomba-omba si halali kwa mwenye uwezo wala kwa mwenye uzima wa afya na mwenye nguvu (za kufanya kazi) ila kwa mwenye kupigwa ufakiri na mw enye deni kubw a (asilow eza kulilipa). Na yule anayeomba watu ili ajiongezee mali yake atakuwa na mkwaruzo usoni mwake katika siku ya Kiyama na atayala kwa ulafi mkubwa mawe ya moto kutoka motoni. Kwa hiyo anayetaka, mwache aombe kidogo, n a m w ache a om be k ingi. (Tirm idh)
Wanaoruhusiwa kuomba kwa mujibu wa Hadith ni:
(i)Mtu aliyesimama kumdhamini mtu mwingine ili kuleta suluhu kati ya wagomvi wawili. huyu anaruhusiwa kuomba hata akiwa tajiri. Kwa mnasaba huu, waumini wa misikitini, madarasa, na shughuli mbali mbali za Kiislamu wanaruhusiwa kuomba michango ya Waislamu ili kufanikisha shughuli hizo.
(ii)Mtu aliyepata ajali na kuharibikiwa kabisa na vitu vyake vyote kama vile ajali ya moto, mafuriko, nakadhalika.
(iii)Mtu ambaye amepigwa na ufakiri na amekosa kabisa mahitaji muhimu ya maisha kama vile chakula, malazi na makazi, lakini mtu akiwa na angalau chakula cha siku moja na malazi mkononi mwake haruhusiwi kuomba kama tunavyofahamishwa katika Hadithi zifu atazo:
Abdullah bin Mas ’ud ameeleza kuwa Mtume wa Al-lah amesema: Anayeomba omba watu na ilhali ana mahitaji muhimu ya maisha atakuja siku ya Kiyama na mikwaruzo, vidonda au majeraha usoni mwake. Iliulizwa: Ee Mtume wa Allah! Ni kiasi gani kinachomtosha mtu? Akajibu: Dirham 50 au thamani yake. (Abu Daud, Tirmidh, Nisai, Ibn Majah).
Sahl bin Haohaliyya ameeleza kuwa Mtume wa Al-lah amesema:Yeyote yule anayeomba na ilihali anajitosheleza kwa mahitaji muhimu, anaomba moto (Jahannam). Nufaili ambaye ni miongoni mwa wasimulizi wa Hadithi hii katika sehemu nyingine aliuliza: Ni yupi mwenye uwezo ambaye kuomba ni haramu? Alijibu (Mtume s.a.w.): Yule mwenye uwezo wa kupata chakula cha asubuhi na usiku. Mahali pengine amesema: Yule mwenye chakula cha siku moja (usiku na mchana) (Abu Daud).
Hivyo ikibidi mtu aombe, basi aombe kwa sababu hizo tatu zilizotajwa katika Hadithi hii. Kuomba omba bila ya sababu za msingi kumeharamishwa kwa sababu kuu tatu zifu atazo:
(i)Kuomba omba kunamfanya mtu apoteze moyoni mwake ile hali ya kumtegemea Allah (s.w.) na atajenga moyoni mwake hali ya kulalamika juu ya neema za Allah zilizomzunguka kila mahali. Kwa msingi huu hatima ya kuomba omba ni kumfanya mja awategemee wengine kwa mahitajio yake badala ya kumtegemea Allah (s.w.) na kumfanya ashindwe kushukuru neema za Allah (s.w.).
(ii)Kuomba omba humfanya mtu awe mnyonge na ajidhalilishe kwa wengine ambapo Muislamu anatakiwa ajidhalilishe kwa Allah (s.w.) peke yake.
(iii)Vile vile kuomba omba kumekatazwa kwa sababu kunamuweka yule anayeombwa katika hali ngumu. Wakati mwingine anayeombwa hali yake si nzuri vile vile lakini kwa kuombwa hulazimika kutoa jambo ambalo linaweza kumuathiri yeye na wale anaowaangalia. Uislamu haukuishia kwenye kukemea tu tabia ya omba omba bali umetoa njia za kutatua tatizo hili kama ifu atavyo:
(i)Kuwasaidia wale wote wenye matatizo na dhiki mbali mbali kwa kuwapa Sadaqa na zakati kabla hawajaomba.
(ii)Njia ya pili, ya kukomesha kuomba omba ni kujitegemea kwa kufanya kazi kwa kutumia juhudi na maarifa.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1032
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Kitau cha Fiqh
Mambo muhimu ya kuzingatia katika kujenga uchumi wa kiislamu
Nazingatio muhimu katika uchumi unaofuata sheria za kiislamu. Soma Zaidi...
Ni zipi siku ambazo ni haramu kufunga? na ni kwa nini hairuhusiwi kufunga katika siku hizo
Soma Zaidi...
Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga. Soma Zaidi...
Haki za muislamu kwa muislamu mwenziwe
Hizi ndio haki kuu tano unazopasa kumpatia Muislamu mwenzio. Soma Zaidi...
namna ya kuswali swala ya msafiri, nguzo zake na hukumu zake
Soma Zaidi...
kwa nini riba ni haramu?
Soma Zaidi...
Mda wa mwisho wa kula daku mwezi wa ramadhani
Post hii fupi itakwenda kukujulisha utaratibu wa kula daku. Soma Zaidi...
Yaliyo haramu kwa mwenye hadathi kubwa.
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ya haramu kwa mwenye hadathi kubwa Soma Zaidi...
Umuhimu wa funga ya ramadhan
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Nini maana ya twahara katika uislamu
Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya twahara katika uislamu. Pia utakwenda kujifunza hukumu za twahara, aina za twahara na mambo mengineyo Soma Zaidi...
IBADA YA HIJA NA NAMNA YA KUITEKELEZA
Soma Zaidi...
Namna lengo la zakat linavyofikiwa
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...