Namna ya Kutayamam hatua kwa hatua, suna zake nguzo za kutayamam na masharti ya kutayamam
Kutayammamu
Kutayammamu ni kujitwaharisha kwa kutumia udongo safi. Waislamu huruhusiwa kujitwaharisha kwa kutayammamu katika hali ya dharura ya:
(i)Ugonjwa usioruhusu kutumia maji.
(ii)Kuwa safarini na kukosa maji ya kutumia au kuwa katika mazingira ya safari yasiyoruhusu kutumia maji.
(iii)Kukosa maji.
Tunajifunza haya katika aya ifuatayo:
“Na mkiwa wagonjwa au mumo safarini au mmoja wenu ametoka chooni au mmeingiliana na wanawake, na hamkupata maji, basi, kusudieni udongo ulio safi (tayammamuni) kwa kuzipaka nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mw enyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru”. (5:6)
Katika aya hii tunajifunza kuwa kutayammamu kumeruhusiwa kwa wakati wa dharura tu. Funzo hili tunalipata katika maneno ya Allah kuwa, “Hapendi Allah kukutieni katika taabu”
Masharti ya Kutayammamu
Tayammamu haitaswihi mpaka yatakapozingatiwa masharti yafuatayo:
1. Ipatikane dharura inayompelekea mtu kuruhusiwa kutayammarnu.
2. Pawe na hitajio la tayammamu kama vile kuswali, kutufu n.k.
3. Kama kusudio la kutayammarnu ni kutekeleza swala ya faradh, tayammamu hiyo ifanyilce baada ya kuingia wakati wa swala hiyo.
4. Pawe na udongo safe (ulio twahara na ulio katika asili yake) ulio mkavu na wenye vumbi vumbi.
Nguzo za Tayammam
Nguzo za tayammam zinabainishwa na aya ifuatayo:
`... Basi kusudieni udongo ulio safi na kupaka nyuso zenu nn mikono yenu..." (4:43)
Aya hii inabainisha kuwa nguzo za tayammam ni:
(i)Nia (kukusudia udongo).
(ii)Kupaka uso.
(iii)Kupaka mikono.
(iv)Kufuata utaratibu huu.
Nampa ya Kutayammamu
(i)Kutia nia. Nia huwekwa pale Muislamu anapokusudia udongo na kuutayarisha kwa ajili ya tayammamu.
(ii)Kupaka uso. Piga udongo uliokusudia kwa viganja vyote viwili vya mikono, kisha puliza viganja iii takataka na vijiwe jiwe vilivyo juu yake vitoke. Kisha paka uso wako kwa kutumia viganja viwili kwa pamoja.
(iii) Kupaka mikono. Anza kupaka mkono wa kulia kwa kiganja cha kushoto. Weka kiganja cha kushoto nyuma ya kiganja cha kulia. Paka mkono wa kulia kuanzia hapo kwa kurudisha kiganja cha kushoto kinyume nyume mpaka kwenye fundo kisha kupaka sehemu ya juu ya mkono wa kulia na kuishia kwenye kidole gumba bila ya kuugusa kiganja mkono wa kulia. Utarudia zoezi hilo kupaka mkono wa kushoto.
Kutumia Ukuta kwa Ajili ya Tayammamu
Mtume (s.a.w) aliwahi kutayammamu kwa kutumia ukuta wa nyumba kama inavyobainika katika hadith ifuatayo:
“Abu Juhaim Al-A nsary (r.a) amehadithia kuw a Mtume w a Allah (Rehema na amani ziwe juu yake) alikuja kutoka upande wa Bir-al-Jamal. Mtu mmoja alimuona akamsalimia. Lakini Mtume hakumjibu, bali alienda kwenye ukuta wa nyumba akapakaza viganja vyake vumbi la ukuta kisha akapaka uso wake wote, kisha mkono wa kulia na wa kushoto, ndipo akamrudishia salamu ”. (Bukhari na Muslim).
Kutokana na hadithi hii tunajifunza kuwa vumbi kwa ajili ya tayammamu si lazima liwe la ardhini tu bali ukuta au jiwe au sehemu yoyote yenye vumbi vumbi iliyotwahara inafaa kutumika kwa ajili ya tayammamu. Kwa mfano wakati wa mvua ambapo udongo umelowana ukuta wa nyumba au ukuta wa chombo cha usafiri au sehemu yoyote yenye vumbi vumbi au iliyokavu na twahara, itakuwa aula kuitumia kwa tayammamu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 web hosting 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Haki za muislamu kwa muislamu mwenziwe
Hizi ndio haki kuu tano unazopasa kumpatia Muislamu mwenzio.
Soma Zaidi...Yajuwe masharti ya udhu yaani yanayofanya udhu kukubalika
Posti hii itakufundisha masharti yanayohitajika kwa mwenye kutaka kutia udhu.
Soma Zaidi...Ni nini maana ya swala
Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu maana halisi ya ibada ya swala.
Soma Zaidi...Makosa Yanayofanywa Wakati wa Swala
Swala ni nguzo ya pili ya Uislamu baada ya Shahada na ni ibada ya kwanza ambayo mja atahisabiwa nayo Siku ya Kiyama. Kwa sababu ya umuhimu wake mkubwa, Muislamu anatakiwa kuiswali kwa usahihi kulingana na mafundisho ya Mtume Muhammad (Swalla Allahu Alayhi Wasallam). Hata hivyo, watu wengi hufanya makosa mbalimbali wakati wa swala, mengine kwa kutokujua na mengine kutokana na uzembe. Makosa haya yanaweza kupunguza thawabu za swala au hata kuifanya swala kuwa batili. Katika makala hii tutajifunza makosa ya kawaida yanayofanywa wakati wa swala, madhara yake, na namna ya kuyarekebisha.
Soma Zaidi...haki ya kutaliki: kuacha na kuachwa katika ndoa ya kiislamu
Haki ya KutalikiKatika jamii nyingi za kjahili haki ya kutoa talaka iko kwa mwanamume tu na mwanamke hana haki yoyote ya kumtaliki mumee.
Soma Zaidi...Waislamu wanaolazimika kufunga
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...