Taratibu za kumiliki hisa na mali ya shirika
Katika Uislamu kuwa na hisa kwenye mali inaruhusiwa. Hapa utajifunza taratibu za kumiliki hisa.
Mali yenye kuchangiwa mtaji kwa hisa
Mtu akishaamua kuuza hisa (share) kwa watu wengine kwa ajili ya mali fulani katika sheria ya Kiislamu anapoteza umilikaji wa mali wa mtu mmoja. Kuuza hisa kwa wengine kwa maana nyingine ni kukaribisha watu wengine kushiriki katika umilikaji wa mali ile. Nafasi ya mtu katika kumiliki mali hiyo itategemea idadi ya hisa alizonazo katika mali ile. Wenye hisa inabidi washirikiane katika faida na hasara pamoja na gharama za uendeshaji.
Faida anazopata atakayekuwa mwenye kumiliki mali
Zipo faida kadhaa ambazo atakayekuwa mwenye kumiliki mali huzipata kwa kufuata ushirika katika biashara, mtaji na faida (Shared Equity and rental) badala ya kupata mikopo ya biashara yenye riba. Faida kubwa atakayopata ni fadhila za Allah (s.w.) kwa kule kuepuka kwake kutoa riba kwa mkopo atakaopata. Tunajifunza katika Hadithi za Mtume (s.a.w.) kuwa laana ya Allah (s.w.) huwafikia wote wanaohusika na riba (mtoaji, mpokeaji, shahidi). Hata hivyo kuna faida nyingine ambazo anaweza kuzipata:
(i) Atakayekuwa mwenye kumiliki mali kwa kutochukuwa mkopo wenye masharti ya riba hujiepusha kabisa na hatari ya kunyang’anywa mali yake (aliyoweka rahani) akishindwa kutimiza masharti yake.
(ii)Fedha ambayo angeitoa kama riba kwa ajili ya mkopo atabaki nayo na kutumia kwa shughuli nyingine kuendeshea maisha yake.
(iii)Atakuwa na uhakika wa kupata sehemu halali ya faida inayotokana na mali hiyo (kama ipo). Kadhalika kama ikitokea hasara haitamlazimu kubeba mzigo wote wa hasara kwani ushirika katika biashara huhusisha vile vile umuhimu wa kugawana hasara itokeapo.
Faida kwa wenye kununua hisa
Mwenye kununua hisa huchangia katika mtaji. Naye huepuka ghadhabu za Allah (s.w.) za utoaji mkopo kwa riba. Zaidi ya haya hupata faida zifuatazo:
(i) Hupata sehemu ya faida itokanayo na mali hiyo kulingana na mchango wake kwenye biashara (idadi ya hisa alizonazo).
(ii) Huwa na sauti kwenye mali kwani naye pia ni mwenye kumiliki mali ile mpaka atakapouza hisa zake. Isitoshe hutoa kiwango kidogo kujipatia haki ya kumiliki ukilinganisha na mtaji mzima.
Kwa ujumla jamii nzima itanufaika kwa kuacha mfumo wa mikopo kwa riba na kuhimiza watu kufanya ushirika katika biashara. Ilivyo waliokopeshana kwa riba hawawi katika uhusiano mzuri kiroho. Aliyekopeshwa ilimbidi kufanya hivyo kutokana na shida aliyokuwa nayo. Kutoa kwake riba anakufanya kwa kuwa anafahamu hatari za kutofanya hivyo (kupoteza mali yake) ingawa kitendo hicho kinamuuma sana rohoni. Hivyo urafiki kati ya mkopeshaji na mkopeshwaji huwa ni wa kinafiki. Jambo hili ni wazi sana katika jamii ya dunia ya sasa. Hebu fikiria athari za mikopo hii kwa nchi masikini duniani. Ni mara nyingi nchi masikini zimekuwa zikipiga kelele aidha kupunguziwa au kufutiwa kabisa baadhi ya madeni yao. Sehemu kubwa ya madeni hayo ni limbikizo la riba la miaka mingi.
Hivyo Uislamu unapiga vita riba kutokana na madhara yake kibinafsi, kitaifa na kimataifa. Aidha Uislamu unahimiza ushirikiano katika biashara kama ufumbuzi wa tatizo la riba.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 ai web app 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Kusimamisha swala za Sunnah
Nguzo za uislamu, kusimamisha swala za Sunnah (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...hukumu ya ombaomba katika uchumi wa kiislamu
Suala la omba-ombaTukiliangalia suala la omba-omba kwa upana kidogo, ambalo hivi sasa linaongelewa katika vikao mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, tutaona kuwa ni Uislamu pekee unaotoa namna bora ya kulishughulikia suala hili.
Soma Zaidi...Hukumu ya kufinga kwa kifuata kuandama kwa mwezi
Ni muda gani unatakiwa ufunge ramadhani, je kuandama kwa mwezi kwa kiona ama hata kusiki.
Soma Zaidi...Aina 12 za swala za sunnah na idadi ya rakaa zake wakati wa usiku na mchana
Aina za Swala za Sunnah.
Soma Zaidi...Zijuwe nguzo tano za uislamu na maana zake katika sheria ya uislamu
Hili ni somo letu la kwanza kwenye mtiririko huu wa darsa za fiqh. Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya uislamu na nguzo zake.
Soma Zaidi...