Navigation Menu



MALI ZISIZORUHUSIWA KUTOLEWA ZAKA

*Suala la kumilikiwa binaadam (utumwa), japokuwa linaendelea kutajwa kwenye Sharia (katika vitabu), ni suala ambalo haliko.

MALI ZISIZORUHUSIWA KUTOLEWA ZAKA

HAIRUHUSIWI ZAKA

*Suala la kumilikiwa binaadam (utumwa), japokuwa linaendelea kutajwa kwenye Sharia (katika vitabu), ni suala ambalo haliko. Uislam tangu siku za Mtume s.a.w. umehimiza kwa kila hali kuwacha huru, kama vile kuwa ni kafara ya makosa tafauti, pia kuwa ni miongoni mwa sadaqa. Yote haya yamebainishwa wazi kabisa kwa Qauli za Mwenyezi Munguna Hadithi za Mtume s.a.w. Uislam ulifanya hivi ili kuondoa binaadam kummiliki binaadam.
Hatakiwi kutoa Zaka kafiri, hata ikiwa ni kafiri wa tangu asili; haya ni kutokana na qauli ya Amir-l-Muuminiina Sayyidna Abu Bukar Al Siddiq r.a.;

 

.
"Hii sadaqa ya fardhi alioifaridhisha Mtume s.a.w. juu ya Waislam". Kafiri, wakati ni kafiri haitakiwi Zaka kutoka kwake. Ama murtadi, yaani yule aliekuwa Islam kisha akaacha Uislam na kuingia ukafirini; yeye inamlazim juu yake yote yale ya Sharia yaliokuwa yakimlazim haliyakuwa ni Muislam, miongoni mwayo ni Zaka. Vilevile haimlazim Zaka mtu anaemilikiwa, kwani mwenye kumilikiwa hawezi kumiliki; hivi ni kwa Qauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:    "……mtumwa aliemilikiwa, asiye weza kitu, ..........". ( Annahal : 75).

 

Aliemilikiwa, yeye na anachomiliki yeye ni cha bwana wake. Wala hakuna kutolewa Zaka kwa mali ya kwiba au kughusubiwa (kunyan'ganya), au mali iliowekwa amana na mwenyewe amekanusha kutoa Zaka, mali ya aina hii haujuzu kutolewa Zaka; hivi ni kwa vile haijuzu kutumiwa mali haya (hayakumilikiwa kihalali). Lakini basi, itabakia juu yake, yaani juu ya yale mali waajibu wa kutolewa Zaka, lakini haitalazimika kutolewa Zaka mpaka mali hayo yarejee kwa mwenyewe wa halali. Ikiwa mali yataharibika kabla ya kurejea kwa mwenyewe, itaondoka waajibu wa kutolewa Zaka mali hayo.

 

Vilevile mali ambayo iko deni (rahani) kwa mtu mwengine, mali hii hailazimiki Zaka yake mpaka irejee kwa mwenyewe. Mali ilio okotwa, (iliompotea mwenyewe) ikipitiwa na mwaka bila ya kujuulikana mwenyewe; Zaka ya mali hii itatolewa na mwenyewe pale atapoipokea hii mali yake, baada ya kuonekana (kuokotwa) na akakabidhiwa mwenyewe. Ama akijuulikana mwenyewe, na akaimiliki yule alieiokota basi yeye ndie ataeitolea Zaka mali hii kwa mujib wa shuruti na kutaanguka kulazimika kutolewa Zaka na yule mwenye mali wa asli.

 

Akiwa mtu atamiliki mali iliofikia kiwango cha kutolewa Zaka, haitafanywa hivyo mpaka mali hayo yapitiwe na mwaka; hivi ni kwa qauli ya Mtume s.a.w.:  .  Maana ya Hadithi hii ni kama hivi:
"Hakuna Zaka katika mali mpaka ipitiwe na mwaka". (Imehadithiwa na Abu Daud)
Vilevile wanyamahoa wanaofugwa na kulishiwa kwa majani na vyakula vya kulishiwa, si wenye kulishiwa machungani; hawa hawatolewi Zaka.
Hili limetolewa dalili kwa qauli ya Sayyidna Abu Bakar r.a.:

 

"Katika kondoo/mbuzi Zaka, na katika kondoo/mbuzi wenye kulishia machungani, wakiwa arubaini mpaka mia na ishirini hutolewa mbuzi mmoja". (Imehadithiwa na Al Bukhary).
Na hawa wanyamahoa wenye kujuzu kutolewa Zaka wenye kulishia machungani iwe ni katika machunga ya halali, si yenye haraam ndani yake; kama vile kuchungwa katika ardhi ilioghusubiwa, yaani ilionyan'ganywa; wanyama hao hawatafaa kutolewa Zaka.



                   

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 500


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu
3. Soma Zaidi...

NGUZO ZA UISLAMU: SWALA NA SHAHADA NA FAIDA ZAKE
NGUZO ZA UISLAMU. Soma Zaidi...

hizi ndizo sharti za swala
Soma Zaidi...

Mifumo ya benk na uchumi wa kiislamu
7. Soma Zaidi...

kuletewa ujumbe
(c)Kuletewa Ujumbe na Malaika kutoka kwa Allah (s. Soma Zaidi...

Vituo vya kunuia hijjah au umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Lengo la kufunga ramadhani, na faida zake, nguzo za kufunga na sharti zake
Saumu (Funga). Soma Zaidi...

Swala za sunnah na faida zake
Soma Zaidi...

Umuhimu na nafasi za hijjah katika uislamu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

nguzo za uislamu: Kutoa zaka, lengo la kutoa zaka na faida zake
Kutoa Zakat. Soma Zaidi...