image

hukumu ya ombaomba katika uchumi wa kiislamu

Suala la omba-ombaTukiliangalia suala la omba-omba kwa upana kidogo, ambalo hivi sasa linaongelewa katika vikao mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, tutaona kuwa ni Uislamu pekee unaotoa namna bora ya kulishughulikia suala hili.

hukumu ya ombaomba katika uchumi wa kiislamu

5

Suala la omba-omba
Tukiliangalia suala la omba-omba kwa upana kidogo, ambalo hivi sasa linaongelewa katika vikao mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, tutaona kuwa ni Uislamu pekee unaotoa namna bora ya kulishughulikia suala hili. Omba omba ni kitendo kibaya sana kikiwa kimefanywa na mtu binafsi au taifa na kinashusha hadhi ya mtu binafsi na hadhi ya taifa kwa ujumla. Hivyo Uislamu ambao ndio njia sahihi pekee ya maisha, hauwezi kamwe ukapalilia omba omba na wala Zaka na sadaka kazi yake si kupalilia omba-omba, bali kinyume chake zaka na sadaka ni miongoni mwa silaha zinazotumiwa kutokomeza omba omba. Uislamu unawashutumu vikali omba omba kama tunavyojifunza katika Hadithi ifuatayo:Hubshi bin Junadah ameeleza kuwa Mtume wa Al-lah amesema: Kuomba-omba si halali kwa mwenye uwezo wala kwa mwenye uzima wa afya na mwenye nguvu (za kufanya kazi) ila kwa mwenye kupigwa ufakiri na mw enye deni kubw a (asilow eza kulilipa). Na yule anayeomba watu ili ajiongezee mali yake atakuwa na mkwaruzo usoni mwake katika siku ya Kiyama na atayala kwa ulafi mkubwa mawe ya moto kutoka motoni. Kwa hiyo anayetaka, mwache aombe kidogo, n a m w ache a om be k ingi. (Tirm idh)Wanaoruhusiwa kuomba kwa mujibu wa Hadith ni:
(i)Mtu aliyesimama kumdhamini mtu mwingine ili kuleta suluhu kati ya wagomvi wawili. huyu anaruhusiwa kuomba hata akiwa tajiri. Kwa mnasaba huu, waumini wa misikitini, madarasa, na shughuli mbali mbali za Kiislamu wanaruhusiwa kuomba michango ya Waislamu ili kufanikisha shughuli hizo.(ii)Mtu aliyepata ajali na kuharibikiwa kabisa na vitu vyake vyote kama vile ajali ya moto, mafuriko, nakadhalika.(iii)Mtu ambaye amepigwa na ufakiri na amekosa kabisa mahitaji muhimu ya maisha kama vile chakula, malazi na makazi, lakini mtu akiwa na angalau chakula cha siku moja na malazi mkononi mwake haruhusiwi kuomba kama tunavyofahamishwa katika Hadithi zifu atazo:Abdullah bin Mas ’ud ameeleza kuwa Mtume wa Al-lah amesema: Anayeomba omba watu na ilhali ana mahitaji muhimu ya maisha atakuja siku ya Kiyama na mikwaruzo, vidonda au majeraha usoni mwake. Iliulizwa: Ee Mtume wa Allah! Ni kiasi gani kinachomtosha mtu? Akajibu: Dirham 50 au thamani yake. (Abu Daud, Tirmidh, Nisai, Ibn Majah).Sahl bin Haohaliyya ameeleza kuwa Mtume wa Al-lah amesema:Yeyote yule anayeomba na ilihali anajitosheleza kwa mahitaji muhimu, anaomba moto (Jahannam). Nufaili ambaye ni miongoni mwa wasimulizi wa Hadithi hii katika sehemu nyingine aliuliza: Ni yupi mwenye uwezo ambaye kuomba ni haramu? Alijibu (Mtume s.a.w.): Yule mwenye uwezo wa kupata chakula cha asubuhi na usiku. Mahali pengine amesema: Yule mwenye chakula cha siku moja (usiku na mchana) (Abu Daud).
Hivyo ikibidi mtu aombe, basi aombe kwa sababu hizo tatu zilizotajwa katika Hadithi hii. Kuomba omba bila ya sababu za msingi kumeharamishwa kwa sababu kuu tatu zifu atazo:(i)Kuomba omba kunamfanya mtu apoteze moyoni mwake ile hali ya kumtegemea Allah (s.w.) na atajenga moyoni mwake hali ya kulalamika juu ya neema za Allah zilizomzunguka kila mahali. Kwa msingi huu hatima ya kuomba omba ni kumfanya mja awategemee wengine kwa mahitajio yake badala ya kumtegemea Allah (s.w.) na kumfanya ashindwe kushukuru neema za Allah (s.w.).(ii)Kuomba omba humfanya mtu awe mnyonge na ajidhalilishe kwa wengine ambapo Muislamu anatakiwa ajidhalilishe kwa Allah (s.w.) peke yake.(iii)Vile vile kuomba omba kumekatazwa kwa sababu kunamuweka yule anayeombwa katika hali ngumu. Wakati mwingine anayeombwa hali yake si nzuri vile vile lakini kwa kuombwa hulazimika kutoa jambo ambalo linaweza kumuathiri yeye na wale anaowaangalia. Uislamu haukuishia kwenye kukemea tu tabia ya omba omba bali umetoa njia za kutatua tatizo hili kama ifu atavyo:(i)Kuwasaidia wale wote wenye matatizo na dhiki mbali mbali kwa kuwapa Sadaqa na zakati kabla hawajaomba.


(ii)Njia ya pili, ya kukomesha kuomba omba ni kujitegemea kwa kufanya kazi kwa kutumia juhudi na maarifa.
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 318


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Sanda ya mtoto
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Ujuwe utaratibu mzima wa funga na kutekeleza ibada ya Swaumu
Soma Zaidi...

Mambo yenye kufunguza swaumu (funga)
Soma Zaidi...

Maneno mazuri mbele ya mwenyezi Mungu
kuna adhkari nyingi sana ambazo Mtume wa Allah ametutaka tuwe tunadumu nazo. lajkini kuna adhkari ambayo imekusanya maneno matukufu na yanayopendwa sana na Allah. Soma Zaidi...

namna ya kuswali
11. Soma Zaidi...

Sera ya uchumi katika uislamu
Hapa utajifunza sera za kiuchumi katika uchumi wa kiislamu. Hapa utajifunza sera kuu tatu za uchumi wa kiislamu. Soma Zaidi...

Ni mali ipi inatakiwa kutolewa zaka?
Soma Zaidi...

Umuhimu wa uchumi katika uislamu
Post hii itakufundisha faida na umuhimu wa kijenga uchumi katika jamii ya kiislamu. Soma Zaidi...

Njia haramu za uchumi
Soma Zaidi...

Je kama maiti imekatika baadhi ya viungo je viungo vyake tunafata utaratibu gani katika kumuosha na kumkafini?
Assalamu Alaykum Warahmatu-llah Wabarakaatuh Naomba kuuliza: Je kama maiti imekatika baadhi ya viungo je viungo vyake tunafata utaratibu gani katika kumuosha na kumkafini? Soma Zaidi...

namna ya kuswali swala ya vitani
Soma Zaidi...

Yajuwe mandalizi ya Ibada ya hija
Soma Zaidi...