Post hii itakufundisha kuhusu nguzo kuu sita za udhu.
Nguzo za Udhu
Allah (s.w) anatufunza kutia udhu katika aya ifuatayo:
Enyi mlioamini! Mnaposimama ili mkaswali, basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na (osheni) miguu yenu mpaka vifundoni...” (5:6)
Kutokana na aya hii na kutokana na mafundisho ya Mtume (s.a.w) nguzo au faradhi za udhu ni hizi zifuatazo
1. Kutia nia moyoni kuwa unatawadha.
2. Kuosha uso kwa ukamilifu kwa kufikisha maji mpaka kwenye mipaka yote ya uso.
3. Kuosha mikono miwili mpaka vifundoni.
4. Kupaka maji kichwani.
5. Kuosha miguu, mpaka vifundoni.
6. Kufuata utaratibu huu kwa kuanza (1) hadi (5) katika mfuatano huu.
Umeionaje Makala hii.. ?
- Watumwa walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na ubinaadamu wao.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha kuhusu swala ya haja na jisi ya kuiswali.
Soma Zaidi...Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake.
Soma Zaidi...