Lengo la kufunga ramadhani, na faida zake, nguzo za kufunga na sharti zake

Saumu (Funga).

Lengo la kufunga ramadhani, na faida zake, nguzo za kufunga na sharti zake

NGUZO YA FUNG (SAUMU) LENNGO LA FUNGA NA FAIDA ZAKE

Saumu (Funga).
Umuhimu wa swaumu (Funga) katika Uislamu.

i.Funga ya mwezi wa Ramadhani ni nguzo ya nne katika Uislamu.
Funga ya mwezi wa Ramadhani ni faradhi kwa waislamu wote na ni miongoni mwa nguzo za Uislamu baada ya shahada, swala na zakat.
Rejea Qur’an (2:183).

ii.Kufunga mwezi wa Ramadhani ni utambulisho wa Uislamu wa mtu.
Mtu akiacha nguzo hii kwa makusudi ni sababu na ishara tosha ya kutoka katika Uislamu.

iii.Kufunga mwezi wa Ramadhani ni utambulisho wa Ucha-Mungu wa mtu.
Funga ya Ramadhani na sunnah zingine ni kielelezo cha Ucha-Mungu wa muislamu zikitekelezwa vilivyo.
Rejea Qur’an (2:183).

iv.Kutofunga mwezi wa Ramadhani makusudi hupelekea kukosa msamaha.
Muislamu asipofunga mwezi wa Ramadhani makusudi basi, hukosa msamaha, na rehma na hustahiki adhabu za Mwenyezi Mungu (s.w).

v.Kufunga mwezi wa Ramadhani ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Kufunga mwezi wa Ramadhani ni faradhi (amri) kwa waislamu wote isipokuwa wenye udhuru.
Rejea Qur’an (2:183).


Lengo la Funga linavyofikiwa.
Lengo kuu la funga ni kumuandaa mja (muislamu) kuwa mcha-Mungu (2:183). Na lengo hili hufikiwa kama ifuatavyo;
i.Funga humzidishia mfungaji imani na uadilifu.
Kufunga ni ibada ya siri, anayejua ni mfungaji na Muumba wake tu, hivyo hufunga ili apate radhi na malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu peke yake.

ii.Funga humzidishia mja nidhamu na utii kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Mja akiwa amefunga huwa mtiifu kwa kufuata amri na kuacha makatazo ya Mwenyezi Mungu na kuchunga vilivyo masharti na nguzo zote za funga.
Rejea Qur’an (2:168) na (2:172).

iii.Funga humzoesha mja kudhibiti matashi ya nafsi na kimwili.
Funga humuepusha mja na tabia za kinyama kama kula, kunywa, kujamii bila sababu ya msingi, na kumjenga kiroho na kiutu ili kuwa na hadhi yake.
Rejea Qur’an (25:43-44) na (2:30-31).

iv.Funga humuwezesha mja kuwahurumia wanaadamu wenzake.
Funga hujenga huruma na mapenzi kwa kule mfungaji kukaa na njaa na adha yake, hivyo hujifunza kuwahurumia wasiokuwa nacho na wenye matatizo.
(34:12-13) na (49:13).

v.Funga humpatia mfungaji afya (siha).
Kwa mfungaji kukaa na njaa muda mrefu, huuwezesha mwili kupumzika na kuondoa malimbilkizo ya vyakula tumboni ambayo ni sumu kwake.

vi.Funga huwafanya Waislamu kuwa Ummah mmoja.
Hii ni kwa sababu funga imefaradhishwa kwa waislamu wa rika na jinsia zote, maskini na matajiri pia, wote hutekeleza amri hii bila ubaguzi wowote.
Rejea Qur’an (49:13).


Faida za Funga.
- Huleta huruma, upendo na mapenzi baina ya wanajamii.
- Huleta utii na nidhamu kwa mfungaji kwa Mola wake na wanaadamu pia.
- Huimarisha afya ya mfungaji.

Kwa nini Lengo la Funga halifikiwi na Wafungaji wengi?
Pamoja na waislamu wengi kujizatiti katika kufunga mwezi wa Ramadhani na funga zingine za sunnah, lakini wengi wao hafikii lengo la funga kwa sababu zifuatazo;
i.Wengi wafungao hawajui lengo la funga.
Wafungaji wengi hufunga kwa lengo la kupata thawabu na kufutiwa madhambi tu na sio kuwa wacha-Mungu kama lilivyo lengo la funga.
Rejea Qur’an (2:183).

ii.Wafungaji wengi chumo lao ni la haramu.
Waislamu wengi wafungao chakula chao, futari yao na daku zao zinatokana na chumo la haramu ambalo ni sababu ya kutopata matunda ya funga zao.

iii.Kutofahamika lengo la maisha na uhusiano na lengo la funga.
Waislamu wengi hutekeleza ibada maalumu kama swala, funga, n.k na kuona kuwa ndio lengo kuu la maisha yao na kuacha nyanja zingine za maisha yao.
Rejea Qur’an (51:56).

iv.Wengi wafungao hawazingatii miiko na sharti za funga zao.
Waislamu wengi wafungao huishia kushinda njaa na kiu bila kupata faida ya funga zao kwa kutojizuilia na mambo maovu, machafu, laghawi, upuuzi, n.k.

v.Wengi wafungao hawatekelezi nguzo na sunnah za funga ipasavyo.
Pamoja na waislamu wengi kufunga, lakini wengi wao hawaswali kabisa swala za faradh na sunnah na kubakia kufuata mkumbo kwa kushinda na njaa.





                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 4833

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Mgawanyo wa mirathi kutoka kwenye Quran

Quran imegawanya mirathi katika haki. Mgawanyo huu ndio unaotakiwa utumike na si vinhinevyo.

Soma Zaidi...
Msimamo wa Uislamu juu ya Utumwa

- Watumwa walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na ubinaadamu wao.

Soma Zaidi...
namna ya kuswali 6

Lugha ya Swala Lugha ya swala,kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni Kiarabu.

Soma Zaidi...
Warithi wasio na mafungu maalumu katika uislamu

Hapa utajifunza watu wanaorithi bila ya kuwekewa mafungu maalumu au viwango maalumi vya kurithi.

Soma Zaidi...
Namna ya kurithisgha hatuwa kwa hatuwa.

Hspa utajifunza sasa jinsi ya kugawa mirathi kutokana na viwango maalumu.

Soma Zaidi...
Kumkafini (kumvisha sanda maiti)

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...