Dalili za Maambukizi kwenye kitovu cha mtoto
Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo ujitokeza kama kuna Maambukizi yoyote kwenye kitovu cha mtoto mdogo, kwa kawaida kitovu cha mtoto kama kiko vizuri kinapona kwa mda mchache na kinakauka mapema iwezekanavyo bila kuwa na tatizo lolote ila kama kuna Dal
Dalili za Maambukizi kwenye kitovu cha mtoto.
1. Kitovu kutoa maji maji.
Kwa kawaida kitovu cha mtoto kikifungwa kwa siku ya kwanza kinaweza kuonyesha tu maji maji kwa siku ya kwanza na ya pili na baadae uendelea vizuri lakini mama au mlezi akiona maji maji kwenye siku ya kwanza ya pili na kuendelea na maji yanaendelea kutoka siku kwa siku ajue wazi kuna Maambukizi na anapaswa kumpeleka mtoto haraka hospitalini ili kuweza kupewa matibabu na kuepuka kuwepo kwa Tetunus kwa mtoto.
2.Pia mama kwa wakati huu ajiepusha na kutumia madawa ya miti shamba kwenye kitovu cha mtoto kwa sababu anaweza kuleta matatizo makubwa au mengine zaidi kwa sababu miti shamba utumia mda mrefu kuponyesha na pengine haiponyeshi kabisa na mda unaenda kwa hiyo mtoto anapoletwa hospitalini hali inakuwa mbaya zaidi.
3. Dalili nyingine ni kubwa kitovu cha mtoto kinavuja damu kupita kiasi.
Hii pia ni Dalili mojawapo ambapo kitovu kinakuwa kinatoa damu inawezekana ni siku chache baada ya kuzaliwa kwa mtoto au siku nyingi kidogo kwa hiyo damu utoka kwa sababu ya kuwepo kwa bakteria ambao ushambulia sehemu za mishipa ambayo iko kwenye kitovu na damu utoka, kw hiyo.Mama au mlezi wanapaswa kumpeleka mtoto hospitalini kwa matibabu zaidi na epuka matibabu ya kienyeji kwa wakati huu.
4. Kuwepo kwa harufu mbaya kwenye sehemu ya kitovu cha mtoto.
Kwa wakati mwingine kunakuwepo na harufu mbaya kwenye kitovu cha mama pakiandamana na usaha ambao unatoa harufu mbaya, kwa sababu ya kuwepo usaha sio vizuri kubinya usaha ili uweze kutoka kwa sababu huwezi kujua kuwa usaha unatokea sehemu gani kwa sababu kuwepo kwa usaha lazima kuwa kuna kitu kimeoza.
5. Ngozi inayozunguka kitovu huwa nyekundu.
Kwa kawaida kama kuna Maambukizi yoyote kwenye kitovu utakuta ngozi inayozunguka kitovu cha mtoto inakuwa nyekundu na pia ukijaribu kugusa utaona mtoto anaumia na kulia kwa hiyo moja kwa moja mzazi au mlezi wa mtoto anapaswa kujua kubwa kuna Maambukizi kwenye kitovu na pia mama hapaswi kufanya chochote kwenye ngozi ya kitovu cha mtoto tofauti na kwenda hospitalini.
6. Kuwepo kwa vipele kwenye ngozi inayozunguka kitovu cha mtoto.
Kwa wakati mwingine ngozi inayozunguka kitovu cha mtoto inakuwa na vipengele, vipengele hivyo kwa wakati mwingine vinakuwa na usaha au pengine vinakuwa havina au kwa wakati mwingine vinakuwa na maumivu kwa sababu ukimgusa mtoto anaanza kulia hivi vipele kwa wakati mwingine vinaandamana na homa.
7. Kwa wakati mwingine mtoto analia sana na kushindwa kunyonya na pengine anasinzia sana kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye kitovu. Kwa hiyo akina mama na walezi wa watoto wanapaswa kujua kubwa hawapaswi kuweka chochote ili kutibu maambukizi au kupasua chochote kwenye kitovu cha mtoto.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 ai web app 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
NAMNA YA KUBORESHA MBEGU ZA KIUME, NA VYAKULA VYA KUBORESHA NGUVU ZA KIUME
Njoo ujifunze vyakula vya kuboresha mbegu za kiume na nguvu za kiume.
Soma Zaidi...mambo ambayo utaulizwa mama mjamzito ukifika kituo cha afya unatakiwa utoe majibu sahihi.
Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo Mama mjamzito anaweza kuulizwa pindi anapokuja kwenye kliniki ya uzazi ,ni mambo muhimu na ya lazima yanayopaswa kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kuona maendeleo yake kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Mimba huonekana katka mkojo baada ya muda gan tangu itungwe
Kipimo cha mimba kwa mkojo kimekuwa kikitumika sana kuangalia ujauzito. Kipimo hiki kinapotumika vibaya kinaweza kukupa majibu ya uongo. Kuwa makini na ujue muda sahihi.
Soma Zaidi...Sababu za Ugonjwa wa kifafa cha mimba.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kifafa cha mimba, kwa kawaida mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu sababu za kuwepo kwa kifafa cha mimba ila kuna visababishi vinavyofikiliwa kama ni Dalili za kifafa cha mimba kama ifuatavyo
Soma Zaidi...Namna ya kumtunza mtoto aliyezaliwa
Post hii inahusu zaidi namna ya kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa, ni njia zitoleeazo na wakunga Ili kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa.
Soma Zaidi...