Vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba

Posti hii inahusu zaidi vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba,ni vipimo vya moja kwa moja kutoka maabara na vingine sio vya maabara.

Vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba.

1.Wachumba na akina Mama kabla ya kubeba mimba wanapaswa kupima vipimo ili kuweza kuangalia kama kuna Magonjwa yoyote ambapo akibeba mimba atapata shida kwake na kwa mtoto.

 

2.Kwanza kabisa Mama anapaswa kupima kama ana Magonjwa yoyote ya zinaa kama vile kaswende kisonono na Magonjwa mengine kama hayo kwa sababu Mama akibeba mimba akiwa nayo mimba inaweza kutoka au Mama anaweza kupata mtoto mfu kwa hiyo ni lazima kupima magy hayo kabla ya kubeba mimba.

 

3.Pia mama na wachumba wanapaswa kupima temperature, msukumo wa damu, mapigo ya moyo, na upumuaji, Magonjwa ya moyo, sukari kwa kufanya hivyo ni maandalizi mazuri ikitokea kuna ugonjwa wowote unatibika mara moja na Mama akija kubeba mimba anakuwa salama na mtoto atakuwa salama kabisa.

 

4.Pia Mama anapaswa kupima kundi la damu yake na kulijua wazi na pia kupima kiwango cha damu na pia kupima kama kuna mambukizi ya virus vya ukimwi kwa kufanya hivyo ataweza ikiwa mama siku ya kujifungua akiishiwa damu ni rahisi kujua damu yake au akikutwa na Maambukizi ni njia nzuri ya kumkinga mtoto kwa hiyo ni vizuri kabisa kupima Mama kabla ya kubeba mimba.

 

5.Kwa hiyo tumeona wazi faida za kupima kabla ya kubeba mimba kwa akina mama na wachumba kwa sababu tunaepuka madhara mbalimbali kwa watoto na kuwakinga na Magonjwa kabla hawajazaliwa ili wazaliwa kabisa kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa mtoto ukimweka kwenye mazingira mazuri ya kuzaliwa atazaliwa salama.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/02/21/Monday - 04:12:37 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 697


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-