Kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito

Kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito faida na hasara zake

KUSHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI WA UJAUZITO

 

Hili ni swali ambalo wengi ya wajawazito wanajiulizaga. Kwa ufupi hakuna shida yeyote kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito, bila kujali hatua ya ujauzito. Unaweza kuzungumza na daktari kuhusu swala hili, ila usiwe na shaka kabisa. Tafiti zinaonyesha kuwa endapo mwanamke akifika kileleni akiwa katika ujauzito ni jambo jema kwa afya yake na afya ya mtoto na afya ya ujauzito. Najuwa maneno haya machache hayawezi kumaliza kiu ya maswali yako. Sasa hebu tuone mabo kadhaa.

 

1.Kwa baadhi ya wanawake wanapata maumivu wanaposhiriki tendo hili wakiwa wajawazito. Yes hii huweza kutokea kwani kzunguruko wa damu umeongezeka maeneo ya chini na kufanya maeneo hayo yawe na hisia nyingi sana. Hii inaweza kuleta hali ya kuumia kwa mjamzito wakati wa kuingia kwa uume. Wajitahidi wakati wa tendo hili kutumia muda mwingi kujiandaa, pia spidi upungue, na tendo lisifanyike kwa nguvu kama siku za kawaida.

 

2.Kuna baadhi ya wanawake wanajikuta uke wao umepunguza hali ya kubana yaani wanahisi unabwebwea. Ukweli ni kuwa kutokana na ongezeko la majimaji mwanamke anaweza kuhisi kuwa ule mnato na msuguano aliouzoea haupo. Hali hii inaweza kuwapunguzia hamu ya tendo baadhi ya wanawake.

 

3.Kwa baadhi ya wanawake majimaji yanakuwa mengi kiasi cha kuhisi kumkosesha raha mwenziwake. Hii hutokea baada ya msisimko kuzidi ama kwa sababu kuna mabdiliko ya homoni. Kama hali ni hii hakuna budi kuvumiliana.

 

4.Mkao wowte unaweza kutumika maadamu hautakandamiza tumbo la mama. Hapa wawe makini sana hasa ujauzito ukiwa mkubwa wasijelibana tumbo. Mkao wa ubavu ubavu na inayofanana na namna hiyo inaweza kuwa ni mizuri. Zungumza na daktari atakupa maelekezo vyema

 

5.Je kushiriki tendo kunaweza kusababisha ujauzito kutoka? Hapana si kweli kabisa. Ujauzito hauwezi kutoka eti kwa kushiriki tendo la ndoa.

 

6.Baada ya kushiriki tendo la ndoa kwa mjamzito anaweza kuona damu ama kutokwa na damu. Hii pia sio tatizo. Ila kama itakuwa inatoka kwa wingi vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.

 

7.Kwa baadhi ya wanwake inafikia wakati hahisi chochote anaposhiriki tendo na anakosa hamu kabisa ya kushiriki. Hili sio tatizo kubwa anaweza kumuona daktari kwa maelezo zaidi.

 

8.Kama atahisi dalili zifuatazo ni vyema kumuona daktari:A.Maumivu makali zaidi yasiyovumilikaB.Damu nyingiC.Kushindwa kupumuwa vyema

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views: 5413

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Bongolite - Game zone - Play free game     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Je siku sahihi yakufanya tendo la ndoa niipi ukipata siku zake za hatari?

Swali langu ni hili doktaJe siku sahihi yakufanya tendo la ndoa niipi ukipata siku zake za hatari?

Soma Zaidi...
Sababu za kutangulia kwa kitovu wakati Mtoto anazaliwa

Posti hii inahusu zaidi sababu za kutangulia kwa kitovu wakati wa mtoto anapozaliwa.

Soma Zaidi...
Uhusiano uliopo kati ya Mama Mjamzito na kibofu cha mkojo.

Posti hii inahusu zaidi uhusiano uliopo kati ya Mama Mjamzito na kibofu cha mkojo.ni mwingiliano unaokuwepo ambao usababisha Mama kukojoa sana wakati wa ujauzito.

Soma Zaidi...
Upungufu wa homoni ya cortisol

Posti hii inahusu zaidi upungufu wa homoni hii ya cortisol,hii ni homoni ambayo utokana na tezi glang(adrenal gland) kufanya kazi kupitiliza hali ambayo mara nyingi husababishwa na msongo wa mawazo wa mda mrefu, yaani wale watu ambao mda mwingi huwa wenye

Soma Zaidi...
Tofauti za ute kwa mwanamke

Posti hii inahusu zaidi tofauti mbalimbali za uke, kwa sababu ya kuwepo kwa matatizo mbalimbali kwenye mwili wa binadamu kuna tofauti mbalimbali za ute kutegemea na hali iliyopo.

Soma Zaidi...
Kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa.

Posti hii inahusu zaidi sababu za kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa,ni Dalili ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha estrogen kwenye mwili ukilinganisha na homoni ya projestoren.

Soma Zaidi...