Mdau anauliza ni muda gani mwanamke anaweza kujijuwa kuwa amepata ujauzito.
Habar,, mwanamke anaweza kujijua ni mjamzito baada ya muda gani?
👉 Wanawake wengi wamekuwa wakijiuliza swali hili. Wengine ni kutokana na shauku ya kutaka ujauzito na wengine ni kutokana na woga wa kupata ujauzito.
🤏 Ukweli ni kuwa sio rahisibkujuwa kabla ya kuanza kuona dalili. Kuna wengine dalili huanza kujitokeza ndani ya wiki 2 na wapo wengine ndani ya wiki tatu hadi mwezi baada ya kukosa siku zake. Hata hivyo wapo wengine ndani ya wiki moja.
👍 Miongoni mwa dalili za ujauzito za mwanzoni kabisa ni pamoja na: -
🐦 1. Maumivu ya kichwa, kizunguzungu ama kichwa kuhisi chepesi
🐦 2. Maumivu ya tumbo, haya yanaweza kuwa makali ama ya kawaida. Yanaweza kutokea kwa muda mfupi kisha kukata.
🐦 3. Kutokea na damu, hii inajulikana kama implantation bleending. Yenyewe ni kidogo ama inaweza kutoka vitone tu.
🐔 4. Maumivu ya matiti ama yanaweza kujaa kidogo. Unaweza kuhisi maumivu kidogo unapoyaminya matiti yako.
🐔 5. Kichefuchefu, mara nyingi dalili hii haitokeagi mwanzoni sana. Hata hivyo inaweza kutokea muda wowote ule.
🩸 6. Kutopata siku zako. Hii hutokea pale mwanamke anapozikosa siku zake. Hapo ataanza kuwaza ni ujauzito. Hata hivyo kukosa siku inaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwepo maradhi, hali ya hewa, vyakula, misongo ya mawazo, matatizo ya homoni.
🚑 Ni vyema kwenda kituo cha afya upate vipimo ama uzungumze na daktari. Unaweza kupata hizo dalili na isiwe ni ujauzito.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo mtu anaweza kupata ikiwa mwili utaeweza kutengeneza progesterone ya kutosha.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za mimba ya miezi kuanzia minne mpaka sita kutoka , Kuna kipindi mimba kuanzia miezi mimne mpaka sita utoka kwa sababu mbalimbali.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo chini upande wa kulia
Soma Zaidi...Tofauti na mambo matano yaliyotajwa hapo juu kuwa yanapelekea ujauzito kutoka, kuna mambo mengine ambayo yanaweza kuuweka ujauzito kuwa hatarini.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Faida za Uzazi wa mpango. Uzazi wa mpango ni huduma ambazo hutoa chaguo kwa familia kuwa na idadi ya watoto wanaotaka katika muda maalum, wanahisi na mbinu iliyoamuliwa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, hali hii utokea kwa watoto wadogo wakati wa kuzaliwa kwa sababu maalum kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye ngozi wakati wa ujauzito, ni mabadiliko yanayotokea kwenye ngozi ya Mama wakati wa ujauzito.
Soma Zaidi...DALILI KUU ZA MIMBA (UJAUZITO) Watu wengi sana wamekuwa wakilalamika kuwa mimba zao zinatoka, ama kupotea bila ya kujulikana tatizo wala bila ya kuugua.
Soma Zaidi...Kama na wewe unasumbuliwa na hali ya kupitiliza siku zako post hii itakusaidia.
Soma Zaidi...