Posti hii inahusu zaidi Maambukizi kwenye kitovu cha mtoto, ni Maambukizi ambayo yanaweza kutokea kwenye kitovu cha mtoto pale ambapo mtoto amezaliwa inawezekana ni kwa sababu ya hali ya mtoto au huduma kuanzia kwa wakunga na wale wanaotumia mtoto.
Maambukizi kwenye kitovu cha mtoto.
1. Kwanza kabisa tunajua kuwa mtoto akiwa tumboni mwa Mama anakuwa ameungana na mama kupitia kwenye plasenta ambapo wakati wa kuzaliwa kitovu ukatwa na plasenta utolewa kwa hiyo hicho kitovu kinapaswa kutunza vizuri ili kisiweze kupata Maambukizi ila kwa wakati mwingine kitovu hicho kinaweza kupata Maambukizi kwa sababu zifuatazo.
2. Pengine kunakuwepo kwa Maambukizi kutoka kwa mama wakati wa kujifungua kwa sababu kuna wadudu ambao wanakaa kwenye nje ya plasenta pale mtoto akitolewa nje na kukata kitovu ili kutenganisha na plasenta wadudu wanaweza kuingia kwenye kitovu na kusababisha maambukizi. Wadudu hao wanaweza kutokana na kuwepo kwa kaswende hasa kwa wamama ambao hawakupima walipogundua kwa na mimba na pia Maambukizi kutokana na Magonjwa mbalimbali.
3. Chupa ya Mama kupasuka wakati wa uchungu na Mama akakaa mda mrefu bila kujifungua.
Kuna kipindi ambapo chupa ya Mama huwa unapaswa na Mama anakaa mda mrefu bila kujifungua kwa kawaida chupa ya Mama ikifungua Mama ukaa mda kidogo na baadae anajifungua ila hadipojifungua wadudu wengine wanaweza kuingia kwenye kitovu na baada ya mtoto kutoka nje ya tumbo la Mama na kitovu kukatwa ili kutenganisha na plasenta wadudu wanaweza kuwa kwenye kitovu na kuleta Maambukizi.
4. Watoa huduma kutumia vifaa vichafu wakati wa kukata kitovu.
Kuna wakati mwingine watoa huduma wanakuwa wazembe katika kutoa huduma kwa sababu wanatumia vifaa ambavyo siyo visafi na wakati mwingine vinakuwa na kutu hatimaye Maambukizi yanaweza kutokea kwenye kitovu.
5.Hasa hasa wale wakunga Jadi wa mitaani utakuta wanatumia wembe mmoja kwa watoto mbalimbali au pengine visu na wanavisafisha kwa njia za kawaida hatimaye wanasababisha Maambukizi kwenye kitovu, kwa hiyo akina Mama wanapaswa kujifungulia hospitalini ili kuepuka hali za kuwepo kwa Maambukizi.
6. Walezi au wazazi kutokitunza vizuri kitovu.
Kuna wakati mwingine wazazi au walezi wa mtoto wanakuwa wazembe katika kutunza kitovu cha mtoto kwa mara nyingine wanatumia mila zao wanazozijua ili kutunza kitovu hali ambayo Usababisha Maambukizi kwa mfano kuna makabila wanaosha kitovu kwa maji yaliyochanganywa naiti shamba hali ambayo Usababisha Maambukizi kwenye kitovu.
7.Kwa hiyo akina Mama wanapaswa kuwatunza watoto wao vizuri na kuepuka madhara yatokanayo na Maambukizi kwenye kitovu kwa kuhakikisha kujua kubwa kitovu hakioshwi na dawa yoyote isiyotolewa hospitalini na kuacha tabia ya kuosha kitovu na miti shamba kwa sababu huwezi kujua kuna nini katika hayo matumizi ya miti shamba.
8 pia akina mama wanapaswa kujifungulia hospitalini hat kama ni mbali siku za kujifungua zikifika wasogee kwa ndugu aliye karibu kwa sababu kwa wakunga wa Jadi kuna shida ya ukosefu wa vifaa kwa hiyo tabia ya kutumia kifaa kimoja na kusafisha Usababisha kuenea kwa magonjwa sio tu Maambukizi kwenye kitovu tu.
9.Pia na wakunga mahospitali wanapaswa kuwa waangalifu katika matumizi ya vifaa ili kuweza kuepuka tatizo la kuwepo kwa Maambukizi kwenye kitovu kwa hiyo vifaa ambavyo vitatumika vinapaswa kuandaliwa vizuri kwa kuwepo kwa watu walio na ujuzi wa kusafisha vifaa kwa utaratibu maalum ili kuweza kuepuka Maambukizi.
10.Vili vile wazazi na walezi wapate elimu maalumu kuhusu namna ya kutunza kitovu cha mtoto na pia wajue wazi madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na kuwepo kwa uzembe wakati wa kutunza kitovu cha mtoto. Vile na wakunga Jadi wapewe vifaa vya kutosha wanapotoa huduma ili kuweza kuepuka madhara ya kuwepo kwa magonjwa maaambukizi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuondoa tatizo la nguvu za kiume
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia upungufu wa damu kwa wajawazito, ni mojawapo ya njia ambazo utumiwa na wahudumu wa afya ili kuweza kuzuia upungufu wa damu kwa wajawazito.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi sababu za kutoshika mimba kwa mwanamke, kuna kipindi ambacho mwanamke hushindwa kushika mimba kuna sababu mbalimbali mojawapo ni kama zifuatazo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo mbalimbali ambayo yanapelekea Mjamzito kutokwa na damu, hizi ni baadhi ya sababu ambazo usababisha Mjamzito kutokwa na damu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi maumivu wakati wa hedhi, haya ni maumivu ambayo utokea wakati wa hedhi kwa wanawake walio wengi, wengine huwa hawayapati kabisa na wengine hutapata na kwa kiwango kikubwa kutegemea na matatizo mbalimbali kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Posti inahusu nzaidi kufunga kwa mishipa ya machozi ya mtoto kwa kawaida mishipa ya mtoto inapaswa kufunguka baada ya mwaka mmoja lakini kwa wengine ubaki imefungwa hata baada ya mwaka mmoja na kusababisha madhara mbalimbali kwa mtoto.
Soma Zaidi...Kuzaa kabla ya wakati ni kuzaliwa ambayo hufanyika zaidi ya wiki tatu kabla ya kuzaliwa kwa mtoto au kuzaliwa mapema ni moja ambayo hutokea kabla ya mwanzo wa wiki ya 37 ya ujauzito. Kawaida, ujauzito hudumu kama wiki 40.
Soma Zaidi...Mdomo kuwa mchungu ni halia mabayo haiashirii ishara mbaya za kiafya. Mdomo unaweza kuwa mchungu kutokana na vyakula. Pia hutokea ikawa ni ishara ya baadhi ya maradhi, ama ni matokeo ya baadhi ya shda za kiafya. Je vipi kuhusu maumivu ya matiti na tumb?
Soma Zaidi...