Huduma kwa mama mwenye kifafa cha mimba.

Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo wajawazito wanaweza kuzipata wakiwa na Dalli au tayari wana kifafa cha mimba.

Huduma kwa wanawake wenye kifafa cha mimba.

1. Kwanza kabisa Mama anapaswa kuhakikisha anahudhuria mahudhurio ya mara kwa mara ili kupima kiwango cha presha na pia kuangalia kiwango cha protini kwenye mkojo na pia kuzingatia mda wa kujifungua na ajitahidi kujifungulia hospitalini ili kuweza kuwa na uhakika wa huduma wakati wa kujifungua, akijifungua mitaani anaweza kupatwa na matatizo ambayo wahudumu wa pale wanaweza kushindwa kuyafanyia kazi na kulingana na tatizo.

 

2. Pia Mama anapaswa kupata mda wa kutosha kupumzika, pia huduma zota anapaswa kuzipata akiwa kitandani kwa hiyo akikaribia kujifungua aepukane na kutembea huku na huko bila sababu ya msingi na pia anapaswa kufundishwa jinsi ya kulala kwenye kitandani ili kuhakikisha kubwa damu inatembelea kwenye mfuko wa uzazi kwa kiwango cha kutosha pia kuhakikisha kubwa na miguu kama imevimba inatoka na kuwa kwenye hali ya kawaida.

 

3. Vile vile mkojo wa Mama unapaswa kuangaliwa kila mara ili kuweza kutambua kama kiwango cha protini kwenye mkojo kimepungua au kinaendelea kuongezeka na kuweza kutoa huduma za msingi ili kupunguza kiwango cha protini kwenye mkojo.

 

4. Kwa mama mjamzito kiwango cha vimiminika vinavyoingia na kutoka vinapaswa kupimwa, ikionekana kwamba  kiwango cha kimiminika kinachotoka ni kikubwa tunajua wazi figo linafanya kazi vizuri ila kama ni kidogo tunajua wazi kubwa kuna tatizo kwenye figo.

 

5. Kupima mara kwa mara kiasi cha presha kwa sababu ili kuweza kutambua kuwa kiwango kinaongezeka au kina pungua kupima mara nne kwa saa.

 

6. Kuendelea kuangalia tumbo mara kwa mara walau mara mbili kwa siku moja ili kuweza kuangalia kama kuna maumivu kwenye tumbo au kitu chochote kisicho cha kawaida.

 

7. Kuangalia mara kwa mara mapigo ya mtoto kama yapo sawa kwa sababu tatizo hili kama halijaangaliwa vizuri usababisha matatizo makubwa kwa mtotoJe! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/04/10/Sunday - 07:33:33 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 968


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-