MAJIMAJI YANAYOTO KA KWENYE UKE


MAJIMAJI YA UKENI (CERVICAL MUCUS)

Kuna mabadiliko yanayotokea kwenye mwili wa mwanamke katika mzunguruko wa siku zake. Cervical mucus ni majimaji yenye sifa tofauti tofauti yanayopatikana kwenye njia ya uzazi yaani uke. Majimaji haya yanabadilika kulingana na siku ama maradhi. Miongoni mwa sifa hizi ni kama kinata, kuteleza, kufutika, ukavu na rangi yake.



Majimaji haya yanasaidia katika kutujulisha siku ambazo ni mujarabu kwa wale ambao wanatafuta ujauzito. Pia majimaji haya ni taarifa kuwa yai lipo karibu ktolewa hivyo ni vyema kujiandaa. Majimaji haya pia yanaweza kutujulisha kama mimba imeingia ama laa. Tofauti na kazi hizi majimaji haya yana kazi zifuatazo:-

1.Kuzuia bakteria na wadudu wengine wasiingie ndani kwenye tumbo la uzazi
2.Kusafirisha mbegu za kiume (sperm) kuelekea ndani
3.Kulainisha njia ya uke na kuwa katika hali iliyo bora zaidi.



Majimaji haya huweza kutofautiana muonekano kutokana na mabadiliko ya siku. Siku hizi huanza kuhesabiwa punde tu baada ya kumalizika kwa hedhi. Ili kuchunguza majimaji haya inahitaji muda na ni vyema kutokukutana kimwili kama unataka kuchunguza mabadiliko haya katika mwezi wote hii husaidia kwani kukutana kimwili kunaweza kuathiri muonekano wa majimaji haya.



Kama unataka kuchunguza kwa baadhi ya siku tu kama kutaka kujua kama yai linakaribia basi unaweza kukaa mkao wowote ambao utafanya uke uwe wazi, kisha tumia kitambaa laini cheupe na kiingize ndani na fanya kama unapangisa kitu kwa ndani ili kuweza kuyapata majimaji haya kwa wingi. Ia unaweza kutumia kidole, baada ya hapo chunguza vyema rangi na muinekano wa majimaji haya kama kuteleza, kunata, kuvutika na uzito.