Hapa utajifunza siku nzuri kushoriki tendo la ndoa kupata ujauzito, dalili za siku hiyo na kuitafuta kwa mahesabu
Swala la kupata ujauzito limekuwa likikabiliwa na imani nyingia ambazo sio sahihi. Watu wengi wamekuwa wakipoteza muda na fedha kujaribu kutatua maswali yao. Leo nitakusaidia kutatua swali hili Je..! ni zipi dalili za mimba changa. Swali hili ni la msingi kwani kuna watu wengi wamekuwa wakichanganya dalili za ujauzito na shida nyingine za kiafya. Hapa nitajaribu kukufahamisha utofauti wa dalili hizi na nyingine ili upate kufahamu vyema.
Imani potofu kuhusu dalili za ujauzito:-
1.Mimba inaingia siku yeyote ile. Hii sio sahihi kabisa mimba inasiku maalumu ambazo huweza kutungwa. Kitaalamu siku hizi zinafahamika kama fertile window
2.Siku yya 14 ndio siku ambayo mimba hingia. Hii pia sio sahihi, kwani wanawake sio wote wanaingia siku 28, kuna wengine ni kati ya 21 mpaka 35
3.Unaweza kupima mimba kwa ktumia sukari, chumvi, mafuta, sabuni, delto. Hizi zote sio sahihi kabisa.
Ni siku gani mimba huingia.
Mimba huweza kuingia siku ambayo yai litakutana na mbegu ya kiume kwenye mirija ya falopia kwenye tumbo la uzazi la mama. Yai la mwanamke kuzalishwa kwenye ovari. Mwanamke ana ovari mbili, moja upande wa kulia na nyingine kushoto. Hizi mbili hupeana zamu ya kutoa mayai. Yaani kama mwezi huu limetoa hili na nyingine itatoa mwezi ujao.
Tafiti zinaonyesha kuwa yai huweza kuanza kukomaa kuanzia siku ya 10 toka kupata hedhi mpaka siku ya 14. hii ni kwa wanawake wengi. Ila si wote. Kikawaida yai hutolewa (ovulation) kwa makadiria ya siku 12 mpaka 16 kabla ya kupata hedhi nyingine. Yaani unaweza kuhesabu kabla ya kuingia hedhi siku 12 nyuma, kisha toa siku 4 mnyuma ndani ya siku nne zizi ndizo yai hutolewa. siku hizi ndizo moja wapo yai hutolewa. Kwa mfano:--
1.Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21, sasa tunatoa siku 12 nyuma kabla ya kuingia hedhi (21 - 12 = 9) kisha toa nne nyuma (9-4=5) basi mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 5 na 9 katika siku zake.
2.Mwanamke mwenye mzunguruko wa siku 32: tunaanza kutoa siku 12 nyuma kabla ya kupata hedhi yake (32-12=20) tonatoa siku nne tena nyuma (20-4=16) kwa hiyo mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 16 mpaka 20.
4.Mwanamke mwenye siku 28: 28-12 = 16 kisha toa siku 4 nyuma 16 - 4 = 12. hivyo siiku ambazo yai hukomaa kwa mwenye siku 28 ni kati ya 12 mpaka 16.
Sasa baada ya kuzijua siku hizi ambazo yai hukomaa, inabidi ufahamu kuwa yai la mwanamke huweza kuishi kati ya masaa 12 mpaka 24 toka kukomaa (ovulation). kwa upande mwingine mbegu za kiume huisho kati ya siku 3 mpaka 5. hivyo ujauzito unaweza kutungwa kwa mbegu ambayo ilikuwepo toka siku tatu zilizopita.
NI IPI HASA SIKU AMBAYO NITAFUTE UJAUZITO?
Kama ulipojifunza hapo juu kuwa zipo siku maalaumu ambazo yai hukomaa. Katika siku hizo mojawapo yai huletwa kwenye mirija ya falopia. Baada ya kukokotoa siku zako hapo juu sasa itakubidi kuongeza siku moja ama mbili nyuma. Hii ni kwa sababu makadirio ya siku hutofautiana. Na si lazima kkutafuta toto katika siku zote hizi. Unaweza kuruka kwa siku moja moja.
Jitahidi kufanya tendo la ndoa hasa katika siku hizo nne ulizozipata baada ya kukokotoa. Katika siku hizo jitahidi kufanya tendo siku ambayo itakuwa na sifa zifuatazo:-
1.Majimaji ya mwanamke ukeni yatakuwa ni mengi kuliko siku zilizopita. Mwanamke mwenyewe anaweza kujichunguza hali hii na kuigundua ila taabu. Anaweza kutumia kidole ama kitambaa safi kuchunguza uwepo wa majimaji haya katika ukeni kwake. Kumbuka hali hii isiambatane na shida nyingine za afya kama PID. Wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kuchunguza hasa kwa wale wanaotumia uzazi wa mpango hasa hasa kwa kutumia vidonge vya homoni.
2.Joto la mwanamke litakuwa ni kubwa kuliko siku nyingine. Joto hili sio homa, na lisiambatane na sababu nyingine kama maumivu ya kichwa, ama kutokana na kulala sana, ama misongo ya mawazo. Kikawaida siku ambayo yai hutolewa joto la mwanamke linakuwa kubwa hivyo akishiriki siku hii ujauzito ni rahisi kuingia.
3.Siku ambayo mwanamke atakuwa na hamu sana ya kushiriki tendo. Wakato ambapo yai hutolewa kuna homoni huzalishwa kwa wingi. Homoni hizi zinaweza kusababisha mwanamke kutamani sana kushiriki tendo zaidi ya siku nyingine.
Pindi mwanamke atakapojigundua kuwa siku hii ameipata basi ni vyema kushiriki tendo ndani ya siku hii ama siku itakayofata haraka iwezekanavyo, maana yai la mwanamke linaweza kufa ndani ya muda mchach masaa 12 mpaka 24.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 5179
Sponsored links
👉1
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2
Kitau cha Fiqh
👉3
Kitabu cha Afya
👉4
Madrasa kiganjani
👉5
kitabu cha Simulizi
👉6
Simulizi za Hadithi Audio
Utaratibu kwa wajawazito na wanaonyonshesha wakiwa na virusi vya ukimwi na ukimwi
Je kuna madhara kwa mwenye virusi vya ukimwi kunyonyesha ama kubeba mimba, na nini afyanye kama ameshabeba mimba ama kama ananyonyesha Soma Zaidi...
Maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa Soma Zaidi...
Maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa
Utajifunza sababu za kuweo kwa maumivu ya uume wbaada ya tendo la ndoa na wakati wa tendo la ndoa. Soma Zaidi...
Namna ya kutibu ugumba kwa Mwanaume.
Posti hii inahusu zaidi namna ya kutibu tatizo la ugumba kwa Mwanaume, ni njia ambazo utumiwa na wataalam mbalimbali Ili kuweza kutibu tatizo la ugumba kwa wanaume. Soma Zaidi...
SIKU HATARI ZA KUPATA UJAUZITO KWA MWENYE MZUNGURUKO WA SIKU KIDONGO AU NYUNGI
SIKU YA KUPATA UJAUZITO Kawaida wanawake walio wengi mzunguruko wa siku zao ni siku 28 lakini wapo ambao ni zaidi ya hapo na wapo ambao ni chini ya hapo. Soma Zaidi...
Siku za kupata mimba
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata mimba Soma Zaidi...
Sababu za kutangulia kwa kitovu wakati Mtoto anazaliwa
Posti hii inahusu zaidi sababu za kutangulia kwa kitovu wakati wa mtoto anapozaliwa. Soma Zaidi...
Kuwashwa pumbu ni dalili ya fangasi?
Habari. Soma Zaidi...
Nini husababisha uke kuwa mkavu
Post hii inakwenda kukupa sababu zinazoweza kupelekea uke kuwa mkavu yaani kukosa majimaji wakati wa kufanya tendo la ndoa. Soma Zaidi...
Maumivu wakati wa tendo la ndoa na baada
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maumivu wakati wa tendo la ndoa na baada Soma Zaidi...