AFYA YA UZAZI
Afya ya uzazi huweza kufungamana na mambo mengi sana. Maradhi na mtindo wa maisha wa mtu huweza kuchukuwa nafasi kubwa katika kuzungumzia afya ya uzazi. Wazazi wengi wamekuwa wakilalamika kkuhusu swala na kushika mimba, maradhi ya kizazi pamoja na wanaume kulalamika kutokuwa na nguvu za kutosheleza haja zao. Afya ya uzazi imekuwa ikichukuwa kundi kubwa la watu pindi inapozungumziwa. Kizazi kilicho salama kinategemea ubora wa afya hii pamoja na malezi yaliyo bora kutoka kwa wazazi.
Katika makala hizi tutakwenda kuona mengi katika hayo yanayohusiana na afya ya uzazi kwa wanaume, wanawake pamoja na watoto ambao ndio kwa kiasi kikubwa afya zao. Makala hii imeandikwa kwa kuangalia tafiti za kiafya zilizofanya katika maeneo mbalimbali duniani.
Tunaheshibu na kuthamini afya ya mtu. Katu hatuthubuthu kuandika kitua bila ya marejeo, hivyo basi ukigundua chochote ambacho hakiposawa kwenye makala hii basi wasiliana nami kwa haraka zaidi