Kiungulia kwa wajawazito, dawa yake na njia za kukabilianannacho

Wajawazito wamekuwa wakisumbuliwa sana na kiungulia, makala hii itakujulisha njia za kukabiliana na kiungulia, dalili zake na dawa zake

Kiungulia kwa wajawazito, dawa yake na njia za kukabilianannacho

Dawa ya kiungulia kwa wajawazito.
Kiungulia ni moka katika matatizo yanayotokea katika mfumo wa chakula. Kiungulia si katika mambo ya hatari, ila huwa ni hali sumbufu sana hasahasa kwa wajawazito. Kama na wewe unasumbuliwa sana na kiungulia makala hii ni kwa ajili yako. Hapa tutaoa sababu za kiungulia, matibabu yake na njia za kuepuka kiungulia.Nini husababisha kiungulia cha mara kwa mara kwa wajawazito?
1.Ni kuwa wakati wa ujauzito kuna mabadiliko mengi ya homoni yanatokea kwa mwanamke. Mabadiliko haya yanapelekea misuli ya kooni inayounganisha tumbo na koo, kujiachia mara kwa mara na hivyo kusababisha tindikali iliyopo tumboni kupanda juu, na kusababisha kiungulia. Hali hii huweza ktokea sana pale unapolala baada ya kula chakula kingi.2.Kadiri mtoto anavyoendelea kukuwa na mimba inavyosonga mbele ndivyo mtoto anaongeza mkandamizo kwenye tumbo. Hali hii inapelekea tindikali iliyopo tundoni kusukumwa kupanda juu na hatimaye kusababisha kiungulia.Je ujauzito unasababisha kiungulia?
Hapana, ujauzito hausababishi kiungulia ila unaongeza uwezekano wa kupata kiungulia. Kivipi?, ni hivi mwanzoni mwa ujauzito koo lako linachukuwa chakula kidogokidogo, na kwa kuwa kuna mabadiliko mengi yanatokea husababisha mmeng'enyo wa chakula kufanya kazi kidogokidogo hivyo kuchelewa kukimeng'enya chakula kwa haraka. Hali hii husaidia mwali kupata muda wa kutosha kufyonza chakula na kukipeleka kwa mtoto, ila kwa upande mwingine hali hii husababisha kiungulia.Hata hivyo si kila mjamzito atakuwa anasumbuliwa na kiungulia, ni kwa sababu kuna mambo mengi yanafngamanna na kiungulia. Hali namna ambavyo mjamzito anaishi inaweza kuchangia kupata kiungulia. Namna mtu alivyo, vyakula anavyokula, namna anavyolala na hata mavazi pia yanaweza kuchangia kupata kiungulia.Mjamzito afanye nini kuepuka kiungulia?
1.Kla kidogo kidogo mara kwa mara na hakikisha hunywi maji wakati wa kula
2.Kula kidogo na hakikisha unatafuna kila tonge kwa ufanisi zaidi
3.Wacha kula unapokaribia kulala
4.Punguza kula vyakula kama chokoleti, vyenye mafuta mengi, vyenye pilipili na vyenye uchachu
5.Usilale baada ya kula angalau unaweza kusimama ama kutembea.
6.Wacha kuvaa nguo za kubana sana
7.Unapolala hakikisha kichwa chako kinakuwa juu, unaweza kutumia mto ama mfano wake
8.Unapolala lalia ubavu wa kushoto
9.Tafuna bigji zisizo na sukari baada ya kula
10.Kunywa maziwa kama unayo unapohisi kiungulia
11.Kunywa asali kama unayo unapohisi kiungulia.Dawa za kutibu kiungulia
Unaweza kutibu kiungulia kwa kutumia antacid kama vile Tums, Rolaids na Maalox.dawa ambazo zimetengenezwa kwa madini ya calcium carbonate au magnesium ni nzuri pia. Magnesium si nzuri kama ujauzito upo mwishoni.Madaktari wengi wanakataza matumizi ya antacid ambazo zimechanganywa na sodium, ama zila lebo ya aluminium carbonate kwani zinawza kupelekea kukosa choo. Pia dawa hizi za kiungulia zinakatazwa kwa wajawazito Alka-Seltzer.

                   

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1467


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-