Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa, suluhisho lako lipo kwenye makala hii
Hii ni hali inayowapata wanawake kwa kiasi kikubwa wakati wanaposhiriki tendo la ndoa. Maumivu haya pia yanaweza kumpata mwanaume ila kwa uchache sana. Hali hii kitaalamu inafahamika kama dyspareunia.
Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa uume unapoingia kwa mara ya kwanza, ama wakati wote wa kuingia na kutoka ama baada ya kumaliza tendo la ndoa. Maumivu ya wakati wa tendo la ndoa yanaweza kutokea kwenye uke, ama uume ama kwenye tumbo kwa kwa wanawake. Makala hii itakwenda kukuorodheshea sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa
1.Uke kuwa mkavu kutokana na maandalizi mabovu kabla ya kuingiza uume. Pia inaweza kuwa ni kutokana na kukosa hamu ya kushiriki tendo.
2.Kuwepo kwa majeraha kwenye uume ama uke. Majeraha haya yanaweza kuwa ni kukeketwa ana ya namna nyingine.
3.Kuwepo kwa uvimbe ama ukawa na matatizo ya ngozi katika sehemu za siri. Haya yote yanaweza kusababisha maumivu wakati wa kuingia kwa uume.
4.Maumbile ya uke. Wakati mwingine jinsi uke ulivyo inaweza kuwa ni tatizo. Kuwa uke mwingine unatabia ya kubana misui yake. Hali hii inaweza kupelekea maumivu wakai wa kupenya kwa uume.
5.Matatizo ya kimaumbile, kwa mfano kuwa na ukilema kwenye uke, ama kuwa na nyama ama ngozi ambayo inaweza kuzuia kupenya kwa uume.
6.Kuwepo kwa maradhi katka mfumo wa uzazi wa kike. Matatizo haya ya kiafya yanaweza kuwa kwenye ovari, ama kukawa na uvimbe ndani ya kizazi ama kukawa na shida katika mirija ya uretas.
7.Kufanyiwa baadhi ya matibabu katika maeneo ya siri. Kwa mfano baadhi ya matibabu ya saratani katika sehemu za siri, matibabu haya yanaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa
8.Matatizo ya kisaikolojia na misongo ya mawaso. Wakati mwingine uoga, kuwa na msongo wa mawazo ama kukumbuka maumivu uliyoyappata siku zanyuma, hali hizi zinaweza kupelekea maumivu wakati mwingine.
9.Staili iliyotumika wakati wa kufanya sex. Wakati mwingine mikao ya kufanya tendo la ndoa inaweza kuwa ni sababu ya maumivu. Ni vyema kutumia mikao iliyo rahisi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Posti hii inazungumzia kuhusiana na maambukizi na uvimbe katika mirija ya uzazi. Mara nyingi hutumiwa sawa na ugonjwa wa uvimbe kwenye fupa nyonga (PID), ingawa PID haina ufafanuzi sahihi na inaweza kurejelea magonjwa kadhaa ya njia ya juu ya uzazi
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na nguvu za kiume zinavyopungua na Ni Mambo gani yanayofanya zipungue
Soma Zaidi...Unaweza kujiuliza ikiwa inawezekana kupata dalili za ujauzito mchanga kama siku 7 baada ya kudondoshwa kwa yai (DPO yaani Days Past Ovulation).
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na sababu zinazosababisha kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Kupata ujauzito hufungamana na mambo mengi ikiwepo afya vya wawili yaani me na mume na mengineyo. Unaweza kushiriki sikuvhatari na usiupate mimba. Postivhii ibakwendavkukufahamisha undani wa jambo hili.
Soma Zaidi...PEP Ni dawa ambazo utumiwa na watu wanaojamiiana na watu wenye virus vya ukimwi ila wenyewe hawawezi kupata kwa sababu ya kutumia dawa hizo.
Soma Zaidi...Post hii itakujulidha mambo ambayo hupunguza nguvu za kiume
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi maji ya Amniotic ni maji ambayo uzunguka mtoto na kufanya kazi mbalimbali kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...