SIFA ZA CERVICAL MUCUS
Majimaji haya pia huwenda kuambatana na dalili za mashambulizi ya bakteria na fangani endapo yatakuwa na harufu mbaya na rangi ya kijani.
Majimaji haya yasichananywe na uchafu utokao kwenye uke kwa sababu ya bakteria, fangasi ama saratani ya kizazi.
Baada ya hedhi uke huwa mkavu hivyo majimaji haya yanakuwa ni macgache na si yenye mtelezo wowote. Hayana rangi yeyote na wala huwezi kuyapata kwa wingi. Hii huashiria kuwa muda huu mwanamke hawezi kupata ujauzito.
Siku chache baadaye majimaji yataanza kuonekana yakiwa na muonekano wa kuweza kunatanata, majimaji haya sio mepesi kabisa. Huu ni mwanzo wa kuandaliwa mazingira ya kupevushwa kwa yai.
Baada ya siku chache tu yai linakaribia kutolewa, muda huu majimaji haya yanakuwa mepesi, laini, mengi na yenye rangi nyeupe. Haya maji ni kiashiria kuwa sasa yai lipo njiani kutolewa. Huu ni muda muafaka zaidi kwa wanaotafuta mtoto.
Siku moja ama mbili kabla ya yao kutolewa majimaji haya yanafanana sana na majimaji ya weupe wa yai, yaani kama yale majmaji meupe yanayooekana pindi linapopasuliwa yai. Majimaji haya yanaweza kuvutika kwenye vidole na yanateleza sana. Hii ni ishara kuwa yai limekaribia kutolewa eidha kwa siku moja ama mbili.
Punde baada ya yai kutolewa majimaji haya yanaanza kuwa makavu na kupoteza mtelezo. Ama uke unakauka na kuwa mkavu na kurudi katika hali ya kawaida. Na kama mimba ilitungwa majimaji haya yanakuwa na rangi ya maziwa. Hivyo ni vyema kuchunguza vizuri ili kujuwa kama mimba ilitungwa au laa.
Pia ijulikane kuwa kuna wanawake wengine hawana majimaji haya na pia kuna wengine ambao majimaji haya ni mengi sana zaidi ya kawaida. Hivyo katika kuchunguza hali hizi wanawake wa aina hii ni ngumu sana kwao.