SIFA ZA CERVICAL MUCUS
Majimaji haya pia huwenda kuambatana na dalili za mashambulizi ya bakteria na fangani endapo yatakuwa na harufu mbaya na rangi ya kijani.
Majimaji haya yasichananywe na uchafu utokao kwenye uke kwa sababu ya bakteria, fangasi ama saratani ya kizazi.
Baada ya hedhi uke huwa mkavu hivyo majimaji haya yanakuwa ni macgache na si yenye mtelezo wowote. Hayana rangi yeyote na wala huwezi kuyapata kwa wingi. Hii huashiria kuwa muda huu mwanamke hawezi kupata ujauzito.
Siku chache baadaye majimaji yataanza kuonekana yakiwa na muonekano wa kuweza kunatanata, majimaji haya sio mepesi kabisa. Huu ni mwanzo wa kuandaliwa mazingira ya kupevushwa kwa yai.
Baada ya siku chache tu yai linakaribia kutolewa, muda huu majimaji haya yanakuwa mepesi, laini, mengi na yenye rangi nyeupe. Haya maji ni kiashiria kuwa sasa yai lipo njiani kutolewa. Huu ni muda muafaka zaidi kwa wanaotafuta mtoto.
Siku moja ama mbili kabla ya yao kutolewa majimaji haya yanafanana sana na majimaji ya weupe wa yai, yaani kama yale majmaji meupe yanayooekana pindi linapopasuliwa yai. Majimaji haya yanaweza kuvutika kwenye vidole na yanateleza sana. Hii ni ishara kuwa yai limekaribia kutolewa eidha kwa siku moja ama mbili.
Punde baada ya yai kutolewa majimaji haya yanaanza kuwa makavu na kupoteza mtelezo. Ama uke unakauka na kuwa mkavu na kurudi katika hali ya kawaida. Na kama mimba ilitungwa majimaji haya yanakuwa na rangi ya maziwa. Hivyo ni vyema kuchunguza vizuri ili kujuwa kama mimba ilitungwa au laa.
Pia ijulikane kuwa kuna wanawake wengine hawana majimaji haya na pia kuna wengine ambao majimaji haya ni mengi sana zaidi ya kawaida. Hivyo katika kuchunguza hali hizi wanawake wa aina hii ni ngumu sana kwao.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Tunaposema uzazi wa mpango, tunamaanisha ile hali ya kuachanisha muda kutoka mtoto hadi mwingine. Inatakiwa angalau mtoto na mtoto wapishane miaka miwili. Uzazi wa mpango ni maamuzi kati ya mama na baba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi, tunajua kabisa wakati wa hedhi damu inapaswa kuwa nyepesi na ya kawaida ila kuna wakati mwingine inakuwa na mabonge zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sifa za Ute wa ovulation, ni Ute ambao utokea siku za ovulation yaani siku ambazo ni tayari kwa kubeba mimba, yaani siku za upevishaji wa yai.
Soma Zaidi...Idadi ya siku hatari za kupata mimba hutofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja namwinhine. Kinda ambao idadivyavsikuvzao za hatari ni nyingi kuliko wengine.
Soma Zaidi...Inatakiwa angalau nafasivkati ya mtoto na mtoto wapishane miaka miwili.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madhara ya kutumia madawa ya shida ya upumuaji, ni madhara madogo madogo ambayo utokea kwa watumiaji wa matatizo ya kupumua.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito faida na hasara zake
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea kwa sababu ya kuziba kwa mishipa ya uzazi, ni baadhi ya dalili ambazo ujitokeza kwa sababu ya kuwepo kwa tatizo la kuziba kwa mishipa ya uzazi.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza njia za kuongeza nguvu za kiume
Soma Zaidi...