Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa wale wenye tabia ya kutoa mimba mara Kwa mara .
1. Kujifungua mtoto kabla ya mda wake.
Kuna kipindi akina dada wanatoa sana mimba wakati wa ujana wao Kuna mwingine anakwambia kwamba kwa mwaka anatoa mimba kama tano hivi na huyu anayefanya hivyo anategemea kupata mtoto baadae eti mda ukifika, akina dada wa hivi wakifikia ule wakati wa kuhitaji watoto mara nyingi mimba utishia kutoka kwa sababu kizazi kimekwisha zoea kwamba hakiwezi kutunza mtoto kwa miezi tisa kwa hiyo ukifika mda ule ambapo Mama utoa mimba na mimba ujiandaa kutoka kwa kuonyesha dalili zote za kutoka kwa mimba na hatimaye mtoto uzaliwa bila kufika mda wake.
2. Kulegea kwa mlango wa kizazi.
Kwa kawaida kutoa mimba mara Kwa mara usababisha kulegea kwa mlango wa kizazi kwa sababu kila mara kizazi kinachokonolewa uenda kwa vyuma au kwa njia yoyote ile hali ambayo usababisha kizazi kulegea. Na kwa hali hiyo usababisha kizazi chenyewe kushindwa kuhifadhi mtoto pale mama anapohitaji mtoto wa kuzaa kabisa.
3. Kuwepo kwa Saratani ya matiti.
Kwa kawaida mimba ikitungwa kila kitu mwilini ubadilika na kuwa tayari kwa ajili ya kutunza mtoto au kichanga kilichomo tumboni. Kwa hiyo na homoni mbalimbali kwenye matiti kuwepo kwa sababu ya kujiandaa kwa ajili ya kunyongenyesha mtoto atakayezaliwa kwa hiyo kutoa mimba mara Kwa mara usababisha Kansas kwenye matiti kwa sababu ya kuwepo kwa hali ya kuzalishwa homoni za mara Kwa mara.
4. Pengine kupata magonjwa ya akili.
Kwa sababu Kuna hali Ile ya baada ya kutoa mimba nyingi na kuharibu sehemu mbalimbali za via vya uzazi na baadae wakati wa kuhitaji mtoto Kunafika na mama anaishindwa kupata mtoto baada ya kujua ukweli anaanza kufikilia mambo mengi na kusababisha hali ya kuchanganyikiwa hasa pale anapopatwa na masimango kutoka sehemu mbalimbali au kwa wale walioshuhudia mambo yake na pia pale anapofikilia jinsi alivyotoa mimba nyingi au pengine Kuna mimba aliitoa na mtoto akalia na mambo kama hayo umfanya mtu kufikilia mambo mengi na hatimaye kupata magonjwa ya akili.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 3225
Sponsored links
👉1
Kitabu cha Afya
👉2
kitabu cha Simulizi
👉3
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4
Kitau cha Fiqh
👉5
Madrasa kiganjani
👉6
Simulizi za Hadithi Audio
Dalili 10 za kukaribia kujifungua pamoja na uchungu wa kujifungua
Download Kitabu cha elimu ya Ujauzito na malezi ya mimba. Soma Zaidi...
Je dalili ya kuuma tumbo huanza baada ya wiki ngapi Toka mwanamke apate ujauzito?
Maumivu ya tumbo ni moja katika dalili za ujauzito. Maumivu wanawake wengi hushindwa kujuwa kuwa ni ujauzito ama laa. Na hii ni kwa sababu kwa wanawake wengi maumivu ya tumbo ama changu ni jalivya kawaida kwao. Soma Zaidi...
Maji ya Amniotic
Posti hii inahusu zaidi maji ya Amniotic ni maji ambayo uzunguka mtoto na kufanya kazi mbalimbali kama ifuayavyo. Soma Zaidi...
Je, mwanamke anapataje Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi PID?
Posti hii inaelezea namna mwanamke anavyoweza kupata Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi. Soma Zaidi...
ZIJUWE DALILI KUU 5 ZA MIMBA CHANGA
Dalili za mimba, na m,imba changa Soma Zaidi...
Changamoto za ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu changamoto za ujauzito na dalili zake endelevu Soma Zaidi...
Dalili za mimba changa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba changa Soma Zaidi...
Maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa Soma Zaidi...
Je siku ya kwanza kabisa ya ovulation mimba inakuwa ni uhakika kupata mimba?
Watu wengi wanadhania kuwa kufanya tendo la ndoa katika siku hatari ni lazima kuwa utapata ujauzito. Hili sio sahihi kabisa. Post hii itakwenda kuangalia jambo hili zaidi. Soma Zaidi...
Madhara ya sindano za kuzuia mimba kwa vijana.
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya matumizi ya sindano za kuzuia mimba kwa vijana ambao hawajafikilia mpango wa kuanza kujifungua watoto. Soma Zaidi...