Posti hii inahusu zaidi Dalili za Mama mwenye kifafa cha mimba, ili kifafa cha mimba kiweze kutokea lazima kuna dalili ambazo uweza kutokea kwa Mama kama ifuatavyo.
Dalili za kifafa cha mimba.
1.Kwanza kabisa tunapaswa kujua kwamba kifafa cha mimba utokea pale ambapo mama mjamzito Upata degedege wakati wa ujauzito na hana historia ya kuwa na Ugonjwa huo au kuwepo kwa Malaria au Magonjwa yoyote ya akili,kwa hiyo dalili zifuatazo zinaweza kuonekana kwa mjamzito zinatambulika kuwa ni kuwepo kwa kifaa cha mimba.
2. Kuwepo kwa protini kwenye mkojo, hii ni mojawapo ya Dalili kwa sababu panakuwepo na tatizo kwenye kibofu cha mkojo mpaka protini inaonekana kwenye mkojo, kwa hiyo matibabu yanapaswa kufanyika mapema ili kuweza kupunguza kiwango hiki cha protini kwenye mkojo.
3. Kiwango cha shinikizo la damu juwa kubwa kuliko kawaida, kwa kawaida kiwango cha presha kinapaswa kuanzia sitini mpaka tisini kwa presha ya chini na mia ishirini mpaka mia arobaini kwa presha ya juu, utamkuta mja mzito ana presha mia sitini kwa mia na kumi kwa hiyo hii ni Dalili mbaya na inaitaji huduma mara moja ili kuweza kupunguza kiwango hiki.
4. Kuvimba kwa miguu wakati wa ujauzito.
Pia kuna tatizo jingine ambapo Mama anavimba miguu wakati wa ujauzito na pengine anatembea kwa shida, kwa sababu ya kuwepo kwa dalili hii mjamzito anapaswa kuwahi hospitali kwa sababu ya vipimo.
5. Maumivu makali ya kichwa.
Vile vile kuna kipindi mjamzito anahisi maumivu makali ya kichwa kwa hiyo anapaswa kuwahi hospitali mapema ili kuweza kupata huduma mara moja.
6 Kuwepo kwa matatizo wakati wa kuona, kwa wakati mwingine mama mjamzito anaanza kuona kwa shida, au kuona maluwe luwe kwa hiyo anapaswa kuwahi na kupata matibabu mapema.
7. Pengine Wajawazito wanahisi kuwepo kwa kiungulia kisicho cha kawaida, kwa hiyo wanapaswa kutoa taarifa ili kuweza kutibiwa.
8. Kwa hiyo baada ya kuona dalili kama hizi wajawazito wanapaswa kwenda mara moja hospitali ili kuweza kupata matibabu, kwa hiyo Mama maisha ni ya kwako na mtoto wako jaribu kuepuka matibabu yasiyo sahihi yaani kutibiwa kienyeji kwenye matatizo kama haya.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi sababu za ugumba kwa Mwanaume, ni sababu ambazo umfanye mwanaume ashindwe kumpatia mwanamke mimba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hatua ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kutibu uvimbe au kwa kitaalamu huitwa fibroids. Hizi hatua zikitumika uweza kusaidia kupunguza kiwango cha kupata au kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi.
Soma Zaidi...Ni mida gani njamzito ananza kuhisi kuwa tumboni anebeba mtoto.
Soma Zaidi...Mimba hatari iliyotungia nje ya mji wa mimba, ni zipi dalili zake na ni kivipo mimba inatungia nje?
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo chini upande wa kulia
Soma Zaidi...Maambukizi kwenye Njia ya Uzazi kwa kifupi hujulikana Kama PID.ni Maambukizi ya mfumo wa Uzazi yanayoathiri wanawake, Maambukizi haya kwa Kawaida huhusisha sehemu Kama shingo ya uzazi,nyuma ya mfuko wa Uzazi na mirija ya uzazi.
Soma Zaidi...Post huu inahusu zaidi mambo yanayopelekea ugumba kwa wanaume, ni mambo ambayo uchangia au upelekea mwanaume kukosa uzazi.
Soma Zaidi...Makala hii itakwenda kukufundisha dalili za kujifunguwa, hatuwa za kujifunguwa na kuzalisha, pia utajifunza mabo muhimu kabla na wakatii wa kujifungua.
Soma Zaidi...Unaweza kupitiliza siku zako za hedhi kwa sababu nyingi. Post hii itakueleza ni kwa nini umechelewa kupata siku zako.
Soma Zaidi...