Kondomu ni mpira ambao uwekwa kwenye uke au uume kwa ajili ya kuzuia mimba wakati wa kujamiiana
Mtazamo juu ya matumizi ya kondonu umekuwa ukikabiliwa na imani za kidini. Zipo dini ambazo zinakataza kabisa, lakini zipo ambazo zinakubali endapo kutakuwa na haja ya kiulazima za kiafya. Kwa vyovyote itakavyokuwa haja ya kutumia kondomu ipo kulingana na sababu mbalimbali. Sababu nyingine zinakubaliwa na dini zote kwa mfano kuzuia kizazi endapo itaonekana ni hatari kwa mwanamke huwenda akapoteza maisha pindi akipata ujauzito, ama kulinda ndoa ambazo mmoja wao ameathirika. Zipo sababu nyingine ambazo zinaweza kukubalika katika dini zote.
Sasa kwa kuwa hali ya matumizi ya kondomu yapo kama hivyo basi ipo haja ya watu kuelezwa faida na hasara ambazo unaweza kuzipata kama utaamuwa kutumia kondomu. Faida hizi na hasara zitasaidia kukukumbusha kuendelea kuwa makini hata ukiwa unatumia kondomu.
Aina za kondomu
1. Kondomu ya kike ambayo huvaliwa na mwanamke wakati wa kujamiiana
2. Kondomu ya kiume, hii ni Aina ya kondomu inayovaliwa na mwanaume wakati wa kujamiiana
Faida za kutumia kondomu
1. Kuzuia kuongezeka kwa mimba zisizotarajiwa
2. Kuzuia magonjwa ya ngono
3. Kuzuia kuambukizwa kwa ugonjwa wa Ukimwi
Kati ya njia za uzazi wa mpango kondomu ndiyo njia pekee inayosaidia kupunguza kusambaa kwa magonjwa ya ngono na Ukimwi
Hasara za kutumia kondomu
1. Kondomu hukinga maambukizi ya magonjwa ya ngono, yanayoingia kwa njia ya ngono, lakini upo uwezekano wa kupata endapo kindomu itapasuka, ama itavuka wakati wa tendo. Pia kama kuna mikato iliyosababishwa na kunyoa na ikawa ipo wazi kuruhusu vijidudu kupendya kwa wawili hawa upo uwezekano wa kupata magonjwa. Ama kuvuka kwa kondomu au kupasuka upo uwezekano wa kupata ujauzito. Ijapokuwa hali hizi ni mara chache sana kutokea. hii inakuwa hasara endapo mtu atajiamini kwa asilimoa 100 kuwa yupo salama anapotumia kondomu bila ya kuchukuwa tahadhari nyingine.
2. kondomu kwa baadhi ya watu inawaletea allegi kama miwasho na mapele. Hii inatokana na mafuta yanayowekwa. Kwa baadhi ya watu miili yao haiendani na mafuta hayohivyo kuwasababishia aleji kila wanapotumia. Zungumza na daktari endapo una tatizo hili la aleji unapotumia kondomu.
3. kuna baadhi ya kondomu zinawekwa vilainishi vya Nonoxynol-9 kwa ajili ya kuuwa mbegu za kiume. Vilainishi hivi vinaweza kusababisha madhara kwenye uke kama kuwashwa hivyo kupelekea kuongezeka kwa hatari ya kupata maradhi ya ngono.
Kuwepo kwa hasara hizi inamaanisha kuwa watumiaji wa kondomu wawe makini wasijipe matumaini ya kuwa salama kwa asilimia 100, kwani chochote kinaweza kutokea.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zilijitokeza zinaweza kusababisha ugumba hasa kwa wanawake, kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwa makini kwa Dalili hizi hasa kwa wadada, kama kuna uwezekano wa matibabu tibu mapema ili kuepuka tatizo la kuwa mgumba.
Soma Zaidi...Abali mkuu Nina mdogo wangu anawashwa Sana sehemu ya Siri mpaka anatoka vipele vingi kwenye mapaja korodani zake zimebadilika kuwa nyekundu na zenye kutisha uume wake nao umekuwa unakama mabaka umebabuka aisee nime angaika Sana kumtibia mpaka nakata tamaa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuzingatia kwa Mama mwenye mimba, ni kipindi ambacho Mama uhitahi uangalizi wa karibu zaidi.
Soma Zaidi...Kupata ujauzito hufungamana na mambo mengi ikiwepo afya vya wawili yaani me na mume na mengineyo. Unaweza kushiriki sikuvhatari na usiupate mimba. Postivhii ibakwendavkukufahamisha undani wa jambo hili.
Soma Zaidi...Point hii inahusu zaidi mbinu za kupunguza Kichefuchefu hasa kwa wagonjwa na watumiaji wa madawa mbalimbali yanayoweza kusababisha kichefuchefu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kupasuka kwa mfuko wa uzazi hasa mama anapokalibia kujifungua.
Soma Zaidi...Maumivu ya hedhi (dysmenorrhea) ni maumivu makali au ya kubana sehemu ya chini ya tumbo. Wanawake wengi hupatwa na Maumivu ya hedhi kabla tu na wakati wa hedhi zao. Kwa wanawake wengine, usumbufu huo ni wa kuudhi tu. Kwa wengine, 
Soma Zaidi...Je kuna madhara kwa mwenye virusi vya ukimwi kunyonyesha ama kubeba mimba, na nini afyanye kama ameshabeba mimba ama kama ananyonyesha
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kiufupi kabisa kuhusiana na Dalili za hatari kwa mama aliyejifungua.
Soma Zaidi...