Posti hii inahusu zaidi sababu za moyo kutanuka, Kuna kipindi ambapo moyo utoka kwenye hali yake ya kawaida na kutanuka hali ambayo usababisha madhara kwa mwenye tatizo hilo, ila Kuna sababu ambazo usababisha moyo kutanuka kama tutakavyoona.
1. Kupanda kwa shinikizo la damu.
Kuna wakati ambapo shinikizo la damu upanda na hali hii usababisha moyo kusukuma damu kwa nguvu na kusababisha moyo kupanuka Ili kuruhusu damu iweze kufika kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
2. Ugonjwa wa misuli ya moyo.
Kuna wakati mwingine kunakuwepo na ugonjwa wa misuli ya moyo au maambukizi kwenye misuli ya moyo hali hii ikitokea usababisha moyo kusukuma damu kwa nguvu na hivyo kusababisha kupanuka kwa moyo.
3. Uwepo wa maji maji ambayo yameuuzunguka moyo.
Kwa kawaida moyo unapaswa kuwa kwenye hali yake ya kawaida lakini Kuna wakati kunakuwepo na maji maji yanayouzunguka moyo ambayo usababisha kuleta maambukizi kwenye sehemu mbalimbali za moyo na hivyo kusababisha moyo kutanuka.
4. Upungufu wa damu mwilini.
Kumbuka kwamba damu ndiyo imebeba hewa ya oksijeni kwa hiyo damu ikipungua usababisha na hewa ya oksijeni kupungua kwa hiyo moyo utumiwa nguvu nyingi Ili kuweza kusukuma damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili Ili kukidhi kiwango cha hewa ya oksijeni iliyokosa kwenye mwili.
5. Matatizo ya tezi.
Kuna wakati mwingine tezi zinashindwa kutoa vichocheo vya kutosha Ili kuweza kukidhi mahitaji ya mwili hali ambayo usababisha mwili kukosa virutubisho hivyo tukumbuke kwamba vichocheo hivyo upitia kwenye damu . Kwa hiyo hivyo vichocheo vikipungua mwilini usababisha moyo kusukuma damu kwa nguvu Ili kusafirisha vichocheo hivyo kwenye mwili hali inayosababisha moyo kupanuka.
6 kuwepo kwa madini mengi ya chumu.
Madini ya chuma yakikusanyika kwenye moyo usababisha moyo kukosa nafasi ya kutosha ya kuweza kusukuma damu ipasavyo kwa hiyo moyo utafuta nafasi ya kusukuma damu kwa nguvu kupitia kwenye mlundikano wa madini ya chuma na kwa sababu ya pressure kubwa ya moyo kusukuma damu hatimaye moyo kutanuka.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Psti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Maambukizi ya tezi za mate ambao hujulikana Kama MABUSHA (mumps) ni maambukizi ya virusi ambayo kimsingi huathiri tezi mojawapo ya jozi tatu za tezi za mate zinazotoa mate, zilizo chini na mbele ya masikio
Soma Zaidi...Ujue ugonjwa wa Njia ya mkojo unaoitwa urethra stricture. Ambapo kwenye hii posti inaonyesha dalili na Sababu zinazopelekea Njia ya mkojo kuwa ngumu,nyembamba,na kovu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kaswende wakati wa ujauzito, kaswende inaweza kukaa kwa mtu zaidi ya miaka mingi bila kuleta madhara ya moja kwa moja lakini kadiri ya siku zinavyokwenda madhara utokea hasa wakati wa ujauzito, madhara hayo umwadhiri mtot
Soma Zaidi...Saratani ya uke ni Saratani adimu inayotokea kwenye uke wako mrija wa misuli unaounganisha uterasi na sehemu zako za siri. Saratani ya uke mara nyingi hutokea katika seli zilizo kwenye uso wa uke wako, ambao wakati mwingine huitwa njia ya uzazi. Wan
Soma Zaidi...Ini Ni kiungo kikubwa Sana mwili na hutumika kuondoa sumu mwili ambayo hujulikana Kama detoxification
Soma Zaidi...Kipindupindu ni ugonjwa wa bakteria ambao kawaida huenezwa kupitia maji machafu. Kipindupindu husababisha Kuhara na Upungufu wa maji mwilini.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu Maambukizi kwenye tumbo na kwenye utumbo mdogo,ni Maambukizi ambayo uwa kwenye tumbo na utumbo mdogo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza na kuonyesha kwamba moyo umetanuka.
Soma Zaidi...Maumivu ya tumbo yanaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwemo typhod, vidonda vya tumbo na shida nyingine kwenye mfumo wa chakula.
Soma Zaidi...