Aina za kisukari

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu aina za kisukari

AINA ZA KISUKARI

1.Type 1 Diabetes; aina hii huotokea wakati mfumo wa kinga mwilini (immune system) unaposhambulia seli zinazozalisha insulin katika kingosho. Seli hizi zinaposhambuliwa mwili utashindwa kuzalisha insulin. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa aina hii ya kisukari husababishwa na virusi pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.

 

Aina hii ya kisukari pia huitwa insulin-dependent au juvenile diabees. Hii hutibiwa kwa kutumia dawa na mara nyingi huweza kuonekana kabla ya miaka 18. Dalili za aina hii ni za hatari sana na hutokea kwa ghafla. Miongoni mwazo ni kiu kikali, kuchoka sana na kupunguwa uzito.

 

2.Type 2 Diabetes; pia aina hii huitwa noninsulin-dependent diabetes na mara nyingi huwapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 40 na wale watu ambao wana uzito wa kuzidi.

 

Katika aina hii ya kisukari mwili unazalisha insulin lakini seli zinashindwa kuitumia insulin inayozaliwa. Miongoni mwa dalili zake ni kukojoakojoa, kiu kikali, kutokuona kwa ufasaha, kuchelewa kupona kwa majeraha na maambukizi ya mara kwa mara.

 

3.Gestation Diabetes; hii huwatokea sana wajawazito mwishoni mwa mimba na hupotea baada ya mtoto kuzaliwa. Hii huweza kuongeza hatari wakati wa kijifungua na kama mama amerithi kisukari kutoka kwa wazazi hali inaweza kuwa mbaya zaid. Dalili zake ni sawa na zile za hizo aina mbili hapo juu,

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 2058

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Dua za Mitume na Manabii    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 web hosting   

Post zinazofanana:

Je minyoo inaweza kusababisha mmeng'enyo wa chakula kuwa dhaifu?

Mfumo wa chakula unaweza kuwa dhaifu kwa sababu nyingi ikiwepo vyakula vyenyewe, vinywaji ama maradhi. Vipi kuhusu minyoo? Endelea na makala hii utajifunza zaidi.

Soma Zaidi...
Tahadhari za ugonjwa wa UTI

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu tahadhari za kuchukua ili kujikinga na UTI

Soma Zaidi...
Dalili za awali za ugonjwa wa kizukari

ugonjwa wa kisukari ni moja katika magonjwa hatari sana, na mpaka sasa bado hauna matibabu ya kuponya moja kwa moja

Soma Zaidi...
Je daktari hizo dalili zamwanzo za HIV hazioneshi kama mwili kupungua

Dalili za HIV zina utofauti na dalili za UKIMWI. Kwani HIV huwezakuonyesha dalili wiki ya pili hadi ya sita baada ya kuathirika kisha zinapotea, lakini dalili za UKIMWI huwezakutokea baada ya miaka 5 hadi 10.

Soma Zaidi...
Sababu za Kuvimba kwa kope.

Post hii inazungumzia kuhusiana na Sababu zinazopelekea kuvimba kwa kope, kawaida huhusisha sehemu ya kope ambapo kope hukua na kuathiri kope zote mbili. Pia hutokea wakati tezi ndogo za mafuta ziko karibu na msingi wa kope huziba. Hii inasababisha kuw

Soma Zaidi...
Zifahmu Dalili za homa ya ini Kali ya pombe.

Posti hii inaonyesha dalili na Mambo Hatari yanayosababisha homa ya ini Kali ya pombe.

Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa sugu wa Figo.

Ugonjwa sugu wa figo, pia huitwa kushindwa kwa figo sugu, huelezea upotevu wa taratibu wa utendakazi wa figo. Figo zako huchuja taka na Majimaji kupita kiasi kutoka kwa damu yako, ambayo hutolewa kwenye mkojo wako. Ugonjwa sugu wa figo unapofikia hatua

Soma Zaidi...
Njia za kujilinda na kujikinga na UTI

Somo hili linakwenda kukuletea njia za kujilinda na kujikinga na UTI

Soma Zaidi...
Fahamu Ugonjwa wa uchovu sugu.

Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa uchovu sugu ni ugonjwa tata unaoonyeshwa na uchovu mwingi ambao hauwezi kuelezewa na hali yoyote ya matibabu. Uchovu unaweza kuwa mbaya zaidi kwa shughuli za kimwili au kiakili, lakini haiboresha kwa kupumzika

Soma Zaidi...
Koo langu limekauka yaweza kuwa ni muadhirika?

kuwashwa na koo ni katika dalili za kuwa na maambukizi mwilini. Kuwa na maambukizi haimaanishi ni HIV ama UKIMWI laa hili ni neno pana. Hapa nitakujuza kwa ufupi kuhusu swali hilo la muulizaji kuwa anawashwa na koo.

Soma Zaidi...