Madhara ya maumivu kwenye nyonga na kiuno.

Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea ikiwa matibabu kwenye nyonga na kiuno hayatafanyika.

Madhara ya kutotibu maambukizi kwenye nyonga na kiuno.

1. Upelekea kushindwa kufanya tendo la ndoa.

Kwa kawaida Ili tendo la ndoa liweze kufanyika ni lazima mwili wote uwe imara na pia kusiwepo na maumivu yoyote, kwa kitendo cha kuwepo kwa maumivu kwenye nyonga usababisha pia kuwepo kwa maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa maumivu hayo uanza taratibu na pia uongezeka na kuwa makali Zaidi endapo matibabu yasipokuwepo.

 

2. Upelekea kupooza kwa baadhi ya viungo vya mwili.

Kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi kwenye kiuno pia usababisha maumivu kwenye baadhi ya viungo vya mwili na pengine usababisha damu isiendelee kupita  kwenye baadhi ya sehemu za mwili na kusababisha baadhi ya viungo kupooza kwa sababu ya kuzuiliwa kwa mzunguko wa damu.

 

3. Usababisha kuwahi kufika kileleni wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Kwa kawaida damu ikishindwa kusafiri vizuri kwenda mwili kwa sababu ya kuwepo kwa mkandamizo wa nevu na hivyo hivyo na baadhi ya mifumo ya mwili nayo upata matatizo mbalimbali kama vile kufika kileleni mapema au kuchoka sana baada ya tendo la ndoa.

 

4. Kwa sababu ya kuwepo kwa maumivu kwenye nyonga na kiuno, Kuna uwezekano wa kushindwa kutembea kabisa kwa sababu ya kuchoka kwa misuli inayosababisha miguu iweze kusimama na mtu kabisa anaweza kufikia huko.

 

5. Kwa hiyo baada ya kujua madhara ya kutotibu maumivu kwenye kiuno pia kwenye nyonga ni vizuri kabisa kutafuta matibabu kwa kuongea na wataalamu wa afya Ili kuweza kupata tiba muhimu na yenye maana kwa kufanya hivyo tutaweza kuepuka matatizo na madhara mbalimbali kwenye mwili.

 

6. Na pia katika matibabu tunapaswa kuepuka na Mila na desturi ambazo zinaponga matibabu ya hospital na kuamini Sana matibabu ambayo hayafai yanayopelekea kuwapoteza wenzetu au kupata matatizo zaidi ya Yale ya mwanzo.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/11/Monday - 12:48:32 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1499


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-