HOMA YA MANJANO (yellow fever)Homa ya manjano ni maradhi yanayosababishwa na virusi na husambazwa na mbu.
HOMA YA MANJANO (yellow fever)
Homa ya manjano ni maradhi yanayosababishwa na virusi na husambazwa na mbu. Homa hii ipo sana nchi za Afrika na Amerika ya Kusini. Kwa hali ya kawaida homa ya manjano huweza kusababisha homa, maumivu ya kichwa, kichefuchefu na kutapika. Pia homa ya manjano inaweza kuwa mbaya zaidi na kupelekea matatizo kwenye ini, figo na moyo pamoja na kutoka kwa damu yali inayotambulika kitaalamu kama hemorrhaging.
Inakadiriwa kuwa asilimia 50 ya wanaopata homa ya manjano wanafariki kwa maradhi maradhi haya. Tafiti zinaonyesha kuwa mpaka sasa hakuna tiba maalumu ya homa ya manjano, ila ipo chanjo kwa ajili ya kujikinga na virusi wanaosababisha homa hii.
Tafiti zinaonesha kuwa baada ya kungโatwa na mbu na kukuachia virusi hawa wa haoma ya manjano, virusi hivi huchukuwa siku tatu mpaka sita kumomaa. Kipindi hiki kitaalamu hufahamika kama incubation period. Katika kipindi hiki katu hutohisi dalili yeyote. Kisha hatua inayofuatainatambulika kama accute phrase kisha hatua ya meisho ni toxic phrase.
DALILI ZA HOMA YA MANJANO
A.Dalili za homa nya manjano katika hatua ya pili (Acute phrase)
1.Homa
2.Maumivu ya kichwa
3.Maumivu ya misuli hasa ya kwenye mgongo na magoti
4.Kutokufurahia mwanga wa jua
5.Vichefuchefu na kutapika
6.Kukosa hamu ya kula
7.Kuhisi kizunguzungu
8.Macho kuwa mekundu, uso na ulimu pia kuwa na rangi nyekundu
B. Dalili za homa ya manjano katika hatua ya pili (toxic phrase)
1.Macho na ngozi kuwa na rangi ya njano
2.Maumivu yasiyo ya kawaida pamoja na kutapika damu
3.Kuongezeka kukojoakojoa
4.Kutoka na damu kwenye mdomo, pua na macho
5.Kupungua kwa mapigo ya moyo (bradycardia)
6.Ini na figo kushindwa kufanya kazi
7.Ubongo kushinwa kufanya kazi, vyema na kusababisha matatizo kama kifafa (seizure), kupoteza fahami (coma) pamoja na kuchanganyikiwa (delirium)
SABABU ZA HOMA NA MANJANO (YELLOW FEVER)
Kama tulivyokwisha kuona kuwa homa ya manjano husababishwa na virusi wanaoenezwa na mbua aina ya Aedes aegypti. Mbu hawa hukaa karibu na maeneo ambayo watu huwa wanaishi na huzaliana kwenye maji yaliyo safi. Virusi vya homa ya manjano vinaweza pia kuwaathiri manyani.
KUJIKINGA NA HOMA YA MANJANO
Ijapokuwa asilimia 20 mapa 50 ya wanaopata homa ya manjano hufariki, lakini itambulike kuwa mgonjwa anauwezo wa kupona kabisa endapo atawahi kupatiw matibabu. Zifuatazo ni baadhi ya njia tu za kujikinga na homa ya manjano
1.pata chanjo ya homa ya manjano
2.Jikinge na kungโatwa na mbu kwa:
?Kulala kwenye chandarua kizima na chenye dawa
?Kupaka losheni ya kuzuia mbu
?Kuondoa majimaji yaliyotuwama na kukata nyasi
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Madonda ya tumbo ni ugonjwa unaotokana na kuwepo kwa vidonda kwenye Koo, tumboni na kwenye utumbo mdogo
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili na Sababu za Homa ya manjano ya watoto wachanga ni kubadilika rangi kwa manjano katika ngozi na macho ya mtoto mchanga. Homa ya manjano ya mtoto hutokea kwa sababu damu ya mtoto ina ziada ya rangi ya
Soma Zaidi...Karibia fangasi wote hawa wanatibika bila ya ugumu wowote maka mgonjwa atakamilisha dozi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu namna ya kumsaidia mgonjwa aliyepungukiwa na damu kwa sababu ya minyoo.
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu matibabu ya vidonda vyatumbo. Pia utajifunza kwa nini kunakuwa na vidonda vya tumbo sugu.
Soma Zaidi...Mvurugiko katika mfumo wa chakula mwilinivunaweza kusababisha maumivu ya tumbo, kuharisha, kutapika na kuchoka pia. Lakini zipo sababu nyingine kama kuwana ujauzito. Nini ufanye endapo unasumbuliwana hali hii
Soma Zaidi...Makala hii itakwenda kukueleza ni nini hasa hizi figo, na ni yapi maradhi yake na ni kwa namna ggani utaweza kujilinda na maradhi ya figo.
Soma Zaidi...Selulitis ni maambukizi ya ngozi ya bakteria ya kawaida, ambayo yanaweza kuwa mbaya. Cellulitis inaonekana kama sehemu nyekundu ya ngozi iliyovimba na inahisi joto na laini. Inaweza kuenea kwa kasi kwa sehemu nyingine za mwili. Cellulitis haienei kuto
Soma Zaidi...