Matatozo katika choo kidogo, maradhi ya figo na dalili zake pia namna ya kujikinga na madhradhi ya figo

Matatozo katika choo kidogo, maradhi ya figo na dalili zake pia namna ya kujikinga na madhradhi ya figo

MATATIZO YA CHOO KIDOGO NA FIGOFigo ni kiungo muhimu sana katika uchujaji wa mkojo, na afya ya mfumo wa utoaji taka mwili.

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Matatozo katika choo kidogo, maradhi ya figo na dalili zake pia namna ya kujikinga na madhradhi ya figo

MATATIZO YA CHOO KIDOGO NA FIGO
Figo ni kiungo muhimu sana katika uchujaji wa mkojo, na afya ya mfumo wa utoaji taka mwili. Figo inakazi ya kuchija damu na kuondoa uchafu usiohitajika. Uchafu hii hukusanyika na kutoka nje kwa kupitia moko. Ndani ya mkojo kumekusanyika uchafu wa kemikali, ikiwemo sumu za vyakula na makemikali mabaya kutoka mwilini.



Endapo mfumo huu wa mkojo ukitetereka unaweza kuaathiri afya ya mtu kwa ujumla. Miongoni mwa matatizo katika mfumo wa mkojo ni kuwepo kwa vijijiwe vidogo. Hivi vinaweza kusababisha maumivu makali na kukosa choo kidogo.



Makala hii inakwenda kukupa ufahamu juu ya tatizo la choo kidogo na kutokea kwa vijijiwe kwenye figo. Pia tutaona sababu za kutokea kwa tatizo hili na vipi tutaweza kujiepusha. Songa nayo makala hii ya afya kwa ni ni muhimu sana kufahamu afya yako na afya ya walio karibu nawe.



VIJIWE VYA KWENYE FIGO NI NINI?
Hivi ni vitu vidogo vigumu kama vijijiwe vilivyotengenezwa ka kemikali zinazopatikana kwenye mkojo kama aina za chumvi na tindikali zilizomo kwenye mkojo. Vijijiwe hivi vinaweza kutokea kwenye figo, kibovu ama mirija ya kusafirisha mkojo. Vijiwe hivi hutengenezwa pale mkojo unapojikusanya kwa muda mrefu hivyo hali hii hutoa nafasi kwa kemikali kujikusanya na kutengeneza vijiwe.



Vijiwe hivi huweza kutoka kwa kupitia njia ya mkojo, kwa maumivu makali sana. Pia endapo hali itakuwa ni mbaya zaidi mgonjwa atafanyiwa upasuaji ili kuweza kuondoa vijiwe hivi. Katika kipindi kama hichi mjonjwa anaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu. Athari ya vijiwe hivi inaweza kupelekea maumivu wakati wa kukojoa.



DALILI ZAKE
Vijiwe hivi mwanzoni havina dalili yeyote lakini endapo vitakuwa vimeshajikusanya vinaweza kuonyesha dalili zifuatazo:-
1.maumivu wakati wa kukujoa
2.Maumivu upande mmoja, kwenye mgongo na chini ya mbavu
Kukojoa mkojo wa rangi ya pinki, nyekundu ama wenye harufu mbaya
3.Kukojoa mara kwa mara
4.Kupata mkojo kidogo unapokwenda kukojoa
5.Homa
6.Kupata kichefuchefu ama kutapika.



SABABU ZA TATIZO HILI NA CHOO KIDOGO NA FIGO
1.vyakula, ulaji wa baadhi ya vyakula kwa wingi unawza kuwa sababu ya kutengenezwa kwa majingira ya kufanyika kwa viji wa vyakula vyenye chumvi hasa calcium unaweza kusababisha vijiwe hivi. Ulaji wa vyakula vya protini kupitiliza pia unaweza kuleta athaji hasi hata kutokea vijiwe hivi.



2.Athari za mashambulizi ya bakteria katika mfumo wa mkojo; mashambulizi kama ya UTI (Urinary track Infection) yanaweza kusababisha vijijiwe hivi. Endapo ugonjwa wa UTI utakaa kwa muda mrefu bila ya kutibiwa na kupona unakuwa UTI sugu, hii inaweza ksababisha kutokea kwa vijiwe kwenye mfumo wa mkojo.



3.nmna ya mtu anavyoishi yaani staili za maisha (life style). mtindo ambao mtu anaishi unaweza kuwa ni hatari kwa afya yako. Kwa mfano kuwa na tabia ya kutokunywa maji mengi, wakati huo huo ukawa unafanya kazi ambazo zinapoteza maji mwilini kwa wingi, kwa mfano kazi ambazo zinaleta jasho sana kisha ukawa haunywi maji ya kutosha. Hii inaweza kusababisha vijijiwe hivi.



4.kurithi baadhi ya matatizo ya kiafya., unaweza kurithi hali ambazo zinaweza kusababisha kwa urahisi kutokea kwa vijiwe hivi. Unaweza kurithi matatizo flani ya kiafya ambayo husababisha figo kuchuja aina maalumu ya asidi za amino itambulikayo kama cystinuria.



MAMBO YAAYOWEZA KUSAIDIA KUTOKEA KWA MATATIZO KATIKA NJIA YA MKOJO NA KUTOKEA KWA VIJIWE VYA KWENYE FIGO
1.familia (kurithi)
2.Kupungua kwa maji mwilini
3.Vyakula
4.Kuzidi kwa uzito
5.Upasuaji



JE UTAZUIAJE MATATIZO KATIKA NJIA YA MKOJO NA VIJIWE VYA KWENYE FIGO?



Wataalamu wa afya wanatueleza baadhi ya njia za kuweza kukabiliana na kujikinga na matatizo ya haja ndogo yaani mkojo. Njia hizi ukizifuata zitakusaidia usiweze kupatwa na vijiwe katika figo:-
1.kunywa maji mengi ya kutosha
2.Punguza kula vyakula vya chumvi kupituliza
3.Punguza ulaji wa baadhi ya vyakula kwa wingi kupitiliza kama bamia, unywaji wa chai kupitiliza, spinachi, viazi vitamu, maharage ya soya, karanga, na chokoleti



JE MADHARA HAYA YA FIGO, NJIA YA MKOJO NA VIJIWE VYE KWENYE FIGO HUWEZA KUTIBIKA?
Ndio matatizo haya yanatibika bila ya tatizo lolote. Mgonjwa atapewa dawa kulingana nna tatizo lake. Kwa hakika atapona kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.







                   



Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 1246

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Zijue dalili za maambukizi ndani ya sikio na madhara yake
Zijue dalili za maambukizi ndani ya sikio na madhara yake

Sikio ni mojawapo ya milango ya fahamu inayotumiwa kwa ajili ya kusikia, Kuna wakati mwingine hushambulia na bakteria na virusi

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa dondakoo
Ugonjwa wa dondakoo

Dondakoo ni ugonjwa mbaya unaosababishwa na sumu inayotengenezwa na bakteria. Husababisha mipako nene nyuma ya pua au koo ambayo inafanya kuwa ngumu kupumua au kumeza. Inaweza kuwa mauti.

Soma Zaidi...
Sababu za Maambukizi kwenye mifupa.
Sababu za Maambukizi kwenye mifupa.

Post hii inahusu zaidi Maambukizi kwenye mifupa ambayo kwa kitaalamu huitwa Osteomyelitis, ni Maambukizi ambayo hutokea kwenye mifupa kwa sababu mbalimbali ambazo usababisha ugonjwa huu.

Soma Zaidi...
Watu walio hatarini kupata UTI
Watu walio hatarini kupata UTI

Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya makunfi ya watu walio hatarini kupata UTI

Soma Zaidi...
   Fahamu Ugonjwa wa kipindupindu.
Fahamu Ugonjwa wa kipindupindu.

Kipindupindu ni ugonjwa wa bakteria ambao kawaida huenezwa kupitia maji machafu. Kipindupindu husababisha Kuhara na Upungufu wa maji mwilini.

Soma Zaidi...
Fahamu sababu za ugonjwa unanipeleka Kuvimba kwa mishipa ya Damu
Fahamu sababu za ugonjwa unanipeleka Kuvimba kwa mishipa ya Damu

posti hii inazungumzia kuhusiana na ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu katika mwili wako wote. Kuvimba kwa Mishipa ya Damu hujulikana Kama Behcet amboyo husababisha dalili nyingi ambazo hapo awali zinaweza kuonekana kuwa hazihusiani. Dalili na ish

Soma Zaidi...
 Dalili na ishara za ugonjwa sugu was Figo.
Dalili na ishara za ugonjwa sugu was Figo.

 Dalili na ishara za ugonjwa sugu wa figo hukua baada ya muda ikiwa uharibifu wa figo unaendelea polepole.  Kupoteza utendakazi wa figo kunaweza kusababisha mrundikano wa majimaji au uchafu wa mwili. Kulingana na jinsi ilivyo kali, upotezaji wa kazi ya

Soma Zaidi...
 Fahamu Ugonjwa wa upungufu wa Adrenali.
Fahamu Ugonjwa wa upungufu wa Adrenali.

Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa upungufu wa Adrenali ni ugonjwa ambao hutokea wakati mwili wako hutoa kiasi cha kutosha cha homoni fulani zinazozalishwa na tezi zako za adrenali. ugonjwa huu hutokea katika makundi yote ya umri na huathiri

Soma Zaidi...
Habari nasumbuliwa na tumbo upande wakilia adi nikikojoa mkojo wa mwisho uwa wa kahawia tiba take nini?
Habari nasumbuliwa na tumbo upande wakilia adi nikikojoa mkojo wa mwisho uwa wa kahawia tiba take nini?

Maumivu ya tumbo yanaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwemo typhod, vidonda vya tumbo na shida nyingine kwenye mfumo wa chakula.

Soma Zaidi...