Matibabu ya vidonda vya tumbo
Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu matibabu ya vidonda vyatumbo. Pia utajifunza kwa nini kunakuwa na vidonda vya tumbo sugu.
MATIBABU NA DAWA Z VIDONDA VYA TUMBO:
Nini vidonda vya tumbo, na zipi aina zake
Vidonda vya tumbo kitaalamu hufahamika kama ulcers, ni vidonda vinavyotokea kwenye tumbo. Vidonda hivi vimepewa majina mbalimbalu kulingana na aina zake. Vipo ambavyo huitwa gastric ulcers ambavyo ni vile avinavyotokea kwenye tumbo la chakula. Aina nyingine huitwa esophangeal ulcers hivi ni vile vinavyotokea kwenye sehemu inayojulikana kama esophagus, ni sehemu inayounganisha koo la chakula na tumbo la chakula. Na aina ya mwisho hujulikana kama duodenal ulcers hivi hutokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayofahamika kama duodenum.
Kwa siku za mwanzo ni ngumu kugunduwa kama una vidonda vya tumbo. Vipimo vinahitajika kugundua kama una vidonda vya tumbo. Kwa kuwa vidonda vya tumbo vina sababu nyingi na hutokea kidogo kidogo, basi hata matibabu yake yanaweza kuchelewa. Endelea na makala hii hadi mwisho, nitakujuza vipimo vipi hutumika kutibu vidonda vya tumbo na ni matibabu gani yanahitajika kulingana na aina ya vidonda na sababu za kutokea kwake.
Vipimo vya vidonda vya tumbo:
Vipimo vya vidonda vya tumbo vimegawanyika katika makundi mengi. Na hata gharama za vipimo vyake zinatofautiana kulingana na kipimo kilichotumika. Hivyo kaama una dalili za vidonda na umepima huna badili aina nyingine ya kipimo. Aina hizo ni kama:-
- Aina ya kwanza ya kipimo ni ila ambayo lwngo lake kubwa ni kuchunguza kama ndani ya tumbo kuna bakteria aina ya H.pylori. Hawa ndio bakteria ambao wanasababisha vidonda vya tumbo kwa kiasi kikubwa. Vipimo hivi mara nyingi ni kwa njia ya kinyesi. Hata hivyo vinaweza kufanyika kwa njia ya pumzi (hewa) ama damu lakini njia hizi sio sahihi kuliko kwa kutumia kinyesi
- Kwa kutumia kifaa cha kuingiza tumboni kinachojulikana kama endoscope. Hiki hungizwa ndani ya tumbo kisha humulika kama katochi. Kwa msaada wa kifaa hiki vidonda vya tumbbo vinaweza kuonekana kwa macho
- Kwa kutumia x-ray hii ni x-ray aalimu kwa lengo la kuchunguza safu za juu za tumbo. Kipimo hiki pia hufahamika kwa jina la barium swallow.
Matibabu na dawa za vidonda vya tumbo:
Kama ulivyojifunza huko juu kuwa matibabu ya vidonda vya tumbo hutolewa kwa kulingana na aina ya vidonda na kulingana na sababu zake. Kama sababu ni bakteria mgonjwa atapewa dawa za kuuwa bakteria. Kama sababu ni ongezeko la tindikali tumboni mgonjwa atapewa dawa ya kupunguza uzalishaji wa tindikali tumboni. Dawa za vidonda vya tumbo ni kama:-
- dawa za kuuwa bakteria wanaosababisha vidonda vya tumbo. Dawa hizo ni kama
- Amoxicillin (amoxil)
- Cacithromycin (Biaxin)
- Metronidazole (flagyl)
- Tinidazole (tindamax)
- Tetracycline (tetracycline HCL
- Levofloxacin (levaquin)
- dawa za kuzuia uzalishwaji wa tindikali za tumboni. Dawa hizo ni kama:-
- Omeprazole,
- lansoprazole,
- Rabeprazole
- Esomeprazole
- Pantoprazole
- Dawa za kupunguza uzalishwaji wa tindikali tumboni. Hiki ni kama
- Ranitidine
- Famotidine
- Cimetidine
- Nizatidine
- Dawa za kulinda ukuta laini wa tumbo hizi hujulikana kama cytoprotective agent. Dawa hizi ni kama sucralfate na misoprostol
Dawa mbadala za vidonda vya tumbo.
Tofauti na dawa hizo lakini pia vidonda vya tumbo viaweza kutibiwa na tiba mbadala. Kuwa makini sana na tiba hizi kwa sababu hazina vipimo maalumu. Tiba hizi mara nyingi hufanya kazi vyema kama sababu ya vidonda ni bakteria. Lakini kama sababu ni nyingine tiba hizi sio sahihi sana. Tiba hizi hujumuisha
- Karoti, kabichi na bamia (hizi unaweza kutengeneza juisi yake).
- Asali
- Kitunguu thaumu
- Shubiri
Athari za kutotibu vidonda vya tumbo:
Ugonjwa wowote unaweza kuwa na madhara zaidi endapo utachelewa kutibiwa. Hali hii pia ni kwa vidonda vya tumbo. Endapo havitatibiwa badi athari mbaya zaidi inaweza kutokea. Ni kawaida kwa vidonda vya tumbo kusababisha kifo ila kama havitatibiwa mwisho wake unawez akuwa kifo. Hebu tuone athari za kutotibu vidonda vya tumbo:-
- Kuvuja kwa damu ndani ya tumbo. Damu hii unaweza kuiona kwenye kinyesi ama kinyesi kuwa cheui sana amakuwa na damu. Hali kama hii inaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini.
- Chakula kinaweza kupita bila ya kumeng’enywa. Kutokana na kuwepo vidonda kkwenye utumbo mdogo, chakula kinaweza kupita hata bila ya kumeng;enywa na kuingia kwenye damu kwa ajili ya kutumika mwilini. Endapo hali kama hii itatokea mtu anaweza kushiba kwa haraka sana na anaweza kupoteza uzitoto kutokana na kukosa virutubisho.
- Pia vidonda vya tumbo visipotibiwa vinaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa mengine tumboni.
- Vinaweza kupelekea utumbo kukatwa. Yesendapo eneo la jeraha limekuwa kubwa na gumu kutibika tiba mbadala ni kuondoa kipande cha utumbo kilichoharibika.
Mambo hatari kwa mwenye vidonda vya tumbo:
- Kunywa pombe
- Kuvuta sigara
- Kula vyakula vyenye uchachu sana
- Kuwa na misongo ya mawazo
- Kukaa na njaa kwa muda mrefu
- Kula vyakula vyenye pilipili kwa wingi
- Kula vyakula vyenye chumvi sansa
Tukutane makala ijayo tuakapoangalia kuhusu dalili za minyoo na sababu zake.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Kuumwa na mgongo: Matatizo ya disc na jinsi ya kuepuka upasuaji.
​Maumivu ya mgongo ni mojawapo ya changamoto kubwa za kiafya zinazomkabili binadamu wa karne ya 21. Kati ya visababishi vikuu, matatizo ya diski za mgongo (spinal disc issues) yanashika nafasi ya juu. Makala hii inatoa mwongozo wa kina kuhusu namna diski zinavyofanya kazi, nini kinatokea zinapoharibika, na muhimu zaidi, mikakati ya kitabibu na mazoezi yanayoweza kukusaidia kuepuka njia ya upasuaji na kurejesha ubora wa maisha yako.
Soma Zaidi...Mazoezi 5 rahisi ya kupunguza uzito na kuimarisha moyo.
Mazoezi ya moyo (cardio) ni ufunguo wa kuchoma mafuta, kuimarisha misuli ya moyo, na kuboresha mfumo mzima wa mzunguko wa damu. Sio lazima uwe na vifaa vya gharama au kujiunga na ukumbi wa mazoezi ili uweze kufanya mazoezi yenye tija. Makala haya yanakuletea mazoezi 5 rahisi, yanayopatikana, na yenye ufanisi mkubwa ambayo unaweza kuyafanya popote pale ili kuanza safari yako ya kupunguza uzito na kulinda afya ya moyo wako.
Soma Zaidi...Namna ya Kumtunza Mtoto Njiti
​Kumtunza mtoto aliyezaliwa kabla ya muda (mtoto njiti) kunahitaji umakini mkubwa, uvumilivu, na upendo. Post hii inatoa mwongozo muhimu kuhusu huduma za msingi nyumbani, ikiwa ni pamoja na joto, lishe, na usafi, ili kuhakikisha mtoto anakua na kuwa na afya njema.
Soma Zaidi...Dalili na ishara za ugonjwa sugu was Figo.
 Dalili na ishara za ugonjwa sugu wa figo hukua baada ya muda ikiwa uharibifu wa figo unaendelea polepole. Kupoteza utendakazi wa figo kunaweza kusababisha mrundikano wa majimaji au uchafu wa mwili. Kulingana na jinsi ilivyo kali, upotezaji wa kazi ya
Soma Zaidi...Jifunze zaidi mzunguko wa mfumo wa damu kwa binadamu
Posti hii inahusu zaidi mfumo wa mwili ambao huhusika na kusafirisha damu ,virutubisho na takamwili.mfumo huu unajumuisha damu,mishipa ya damu na moyo.moyo husukuma damu kupitia mishipa ya damu na kufika maeneo yote ya mwili.
Soma Zaidi...Dawa za kutibu kiungulia
Somo hili linakwenda kukueleza baadhi ya dawa za kutibu kiungulia
Soma Zaidi...