Posti hii inahusu namna ya kumsaidia mgonjwa aliyepungukiwa na damu kwa sababu ya minyoo.
Namna ya kumsaidia aliyepungukiwa na damu kwas sababu ya kuwepo kwa minyoo.
1. Kwanza tibu tatizo la upungufu wa damu kwa kutumia vyakula vyenye madini ya chuma na vyakula vyenye protini, kwa kutumia vyakula hivi damu inaweza kuongezeka kwa haraka zaidi kuliko kawaida,maana hata kama shida ni minyoo Anemia ndiyo inapaswa kutibiwa haraka kwa sababu damu ikipungua sana inaweza kuleta shida.
2. Kama Kuna dalili zozote za Anemia na zinaonekana wazi, inabidi kuangalia wingi wa damu na kuona kiasi kilichomo kama kiasi Cha wingi wa damu ni zaidi ya 5g/l vyakula na dawa mbalimbali vinaweza kutumika Ili kuongeza damu na mboga mboga za majani zinaweza kutumika Ili kuongeza damu, kama kiwango Cha damu ni Chini ya 5g/l mgonjwa inabidi aongezewa damu mara Moja. Tujue kuwa damu ni muhimu kwa binadamu kwa hiyo ni muhimu kuongeza mara Moja ikiisha.
3. Baada ya kuongeza damu mgonjwa anapaswa kutumia dawa za kuondoa minyoo kama vile mebendazole na albendazole hizi dawa zinapaswa kutumiwa kwa maagizo ya wataalamu wa afya na sio kutumia dawa tu, na tujue mtu akiwa anatumia dawa za minyoo hapaswa kunywa pombe maana ni hatari kwa kuchanganya dawa za minyoo na pombe.
4.Baada ya kumpatia mgonjwa dawa uangalizi unapaswa kuwepo Ili kuhakikisha kuwa mgonjwa anapona kabisa na pia mgonjwa anapaswa kupima wingi wa damu Ili kuangalia kama kiwango Cha damu mwilini kipo kwenye hali ya kawaida kabla hajaruhisiwa kutoka hospitalini, na pia mgonjwa anapaswa kutumia dawa za kuongeza damu na kutumia vyakula vyenye wingi wa protein na vyakula vyenye wingi wa madini ya chuma.
5. Elimu inabidi utolewa kwa mgonjwa na wote waliomzunguka kuhusu namna ya kujikinga na ugonjwa wa upungufu wa damu hasa kuhusu namna ya kupambana na minyoo kwenye mazingira na kuchimba choo, kunywa maji masafi,kuepuka kucheza kwenye maji yaliyotuhama hasa kwa watoto wadogo na kutumia dawa za minyoo kwa mda Ili kama Kuna Aina yoyote ya minyoo itaondoka na kiwango Cha damu kitakuwa kawaida.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi jinsi magonjwa yanavyosambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Soma Zaidi...Mvurugiko katika mfumo wa chakula mwilinivunaweza kusababisha maumivu ya tumbo, kuharisha, kutapika na kuchoka pia. Lakini zipo sababu nyingine kama kuwana ujauzito. Nini ufanye endapo unasumbuliwana hali hii
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za Maambukizi kwenye mifupa, ni dalili ambazo ukionyesha kwa mtu mwenye Maambukizi kwenye mifupa.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya fikra potofu kuhusu vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Swali langu: Ukiwa na areji , afu kupata muwasho korodani unapo jikuna unga kutoka nayo fangasi?
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya gonorrhea endapo haitotibiwa
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dalili za maambukizi kwenye uume, ni dalili ambazo ujitokeza pale maambukizi yanapotokea kwenye uume.
Soma Zaidi...Kama una tatizo la midomo kuchubuka na kuwa myeupe ama kuwa na vidonda. Post hii inakwenda kuangalia swala hili.
Soma Zaidi...