MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU

Maana ya elimuElimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji.

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU


Maana ya elimu
Elimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji. Wanataaluma wamejitahidi kutoa maana ya elimu kuwa ni mabadiliko ya tabia yanayotokana na ujuzi. Kwa maana hii Elimu haiishii kwenye kuijua tu bali elimu hukamilika inapomwezesha mwenye kujua kutenda kwa ufanisi zaidi kuliko yule asiyejua.



Nani aliye elimika?
Kutokana na maana ya elimu tuliyojifunza hapo juu, mtu aliyeelimika ni yule ambaye ujuzi alioupata humuwezesha kutenda kwa ufanisi zaidi kuliko pale alipokuwa hajapata ujuzi huo. Mtu aliyesoma hatachukuliwa tu kwa kirahisi kuwa kaelimika, bali kuelimika au kutoelimika kwake kutathibitika katika matendo na mwenendo wake wa kila siku. Matarajio ni kwamba mtu aliyesoma anapaswa aelimike kwa kutenda kwa ufanisi zaidi kuliko asiyesoma. Ni katika kuzingatia hili Allah (s.w) anatukumbusha katika Qur-an:


β€œ... Sema, Je! wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu.” (39:9)
Jibu la swali hili ni wazi. Mjuzi na asiyejua hawawezi kuwa sawa kiutendaji na kitabia. Endapo mtu atajiita msomi kwa kusoma vitabu vingi au kupewa shahada nyingi lakini kitabia na kiutendaji akawa hatofautiani na wale wasiosoma atakuwa bado hajaelimika na mfano wake ni ule unaopigwa katika Qur-an:



β€œMfano wa wale waliopewa Taurati kisha hawakuichukua (kwa kuitia katika matendo) ni kama punda aliyebeba (mzigo) wa vitabu vikubwa (bila ya kufaidika kwavyo) ni mbaya kabisa mfano wa watu waliokadhibisha aya za Mwenyezi Mungu. Na Mw enyezi Mungu haw aongoi w atu m adhalim u.” (62:5).




                   


Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1457

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰2 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana: